Kwa mujibu wa maelekezo ya #Sheikh_wa_Al-Azhar.. kupeleka msafara mkubwa zaidi kutoka kwa #Baiti_ya_Zaka_na_Sadaka ya kimisri kwenda Ukanda wa Gaza
Kwa mujibu wa maelekezo ya Sheikh wa Al-Azhar.. Baiti ya Zaka yapeleka msafara wa misaada unaoundwa na lori 40 kwa watu wa Gaza.
Leo, Jumamosi tarehe 18 Novemba 2023, msafara uliotolewa na Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri ulikwenda kwa bandari kavu ya Rafah kwa mujibu wa maelekezo ya Mheshimiwa #Imamu_Mkuu Profesa/ Ahmad Al-Tayyeb Sheikhi wa Al-Azhar, msimamizi mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri, ikiundwa na lori 40 zilizojazwa na dawa, chakula na vifaa vya misaada kwa ndugu wapalestina kwenye ukanda wa Gaza.
Inatajwa kuwa huo ni msafara wa pili unaopelekwa na Baiti ya Zaka kwa mujibu wa maelekezo ya Sheikhi wa Al-Azhar kwa ndugu zetu huko Gaza, msafara huo ni sehemu ya shughuli za kampen iliyoanzishwa na Al-Azhar Al-Shareif kwa anuani: "Waokoeni Gaza" iliyotangazwa na Mheshimiwa Imamu Mkuu tangu kuanza kwa mashambulizi ya kizayuni dhidi ya familia zetu katika Ukanda wa Gaza, kwa lengo la kutekeleza wajibu wa kidini, kisheria, kibinadamu na kimaadili kwa ndugu zetu huko Gaza, na kuwasaidia mbele ya mazingiwa magumu sana, mashambulizi, mauaji na uhamisho, jambo lililopelekea kuuawa shahidi zaidi ya raia wasio na hatia zaidi ya elfu 11 mpaka sasa huko Gaza, nusu yao ni watoto.
Inakumbukwa kwamba msafara wa kwanza uliopelekwa mwishoni mwa mwezi uliopita uliundwa na lori 18 zinazojazwa na Dawa, na misaada mbalimbali, kama vile maji, vyakula na nguo, na baad ya wiki mbili Al-Azhar ilipeleka msafara huo ambao ni mkubwa zaidi unaokusanya lori 40 zilizojazwa na misaada ya dawa, vyakula, na misaada mbalimbali, kama maji, nguo na blanketi, na hayo ni kwa ajili ya kuwaunga mkono wapalestina na Jamhuri ya Kiarabu ya #Misri kwa mujibu wa jukumu lake la kihistoria kuhusu kuunga mkono ndugu zetu huko Gaza.
Nyumba ya Zaka na Sadaka ya kimisri ilianzishwa mwaka 2014, kwa agizo la Mheshimiwa Imamu Mkuu, Prof/ Ahmad Al-Tayyeb, Sheikhi wa Al-Azhar, na chini ya usimamizi wake; kwa lengo la kutoa mali ya Zaka katika vyanzo vyao halali, na kuendeleza mali ya Sadaka, michango, zawadi, wasia na kuzitoa katika vyanzo vyake, na kwa ajili ya kuongeza ufahamu wa uwajibika wa Zaka na jukumu lake katika maendeleo ya jamii, na hali ya kushikamana na huruma baina ya wana wa jamii.