Taarifa ya Al-Azhar katika siku ya kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina

  • | Wednesday, 29 November, 2023
Taarifa ya Al-Azhar katika siku ya kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina

     Al-Azhar: kumbukumbu ya kuigawanya Palestina ni kumbukumbu chungu zaidi katika historia ya kibinadamu ya kisasa.

Al-Azhar yatoa wito kwa ulimwengu kuunga mkono Wapalestina ili kurejesha ardhi na haki zao.

Al-Azhar katika kumbukumbu ya kuigawanya Palestina: lazima kubainisha na kusambaza jinai za mamlaka ya kizayuni dhidi ya Wapalestina kwa ulimwengu.

Al-Azhar inaukumbusha ulimwengu wote kwa kumbukumbu chungu inayowadia leo; nayo ni siku ya kuigawanya Palestina katika nchi mbili, ikisisitiza kuwa itabakia kuwa kumbukumbu iliyo mbaya na chungu zaidi katika historia ya kibinadamu ya kisasa, na kwamba inakuja mwaka huu katika hali ya ngumu ya maumivu na ukatili ambapo Wapalestina wameteseka tangu zamani na mpaka sasa hivi, kwa zaidi ya siku 50 Wapalestina wanakabiliwa na mauaji ya kimbari na wanalazimishwa kuyahama makazi yao, na kuzuia chakula, dawa na maji, kukata umeme na intaneti, kuwashambulia raia katika hospitali, misikiti, makanisa na vituo vya wakimbizi, na kuwaua zaidi ya watoto elfu sita, na wanawake zaidi ya elfu tano.

Katika kumbukumbu hiyo, Al-Azhar inatoa ahadi ya kuendelea kuwaunga mkono Waplestina katika utetezi wake kuhusu suala lake ambalo ni suala letu na suala la watu huru duniani kote, ikitoa wito wa kutangaza na kubainisha ukatili wa mamlaka ya kizayuni, yaliyozoea kung'oa ardhi, na kutumia nguvu dhidi Wapalestina wasio na hatia, yakipuuza sheria, kanuni na mikataba ya kimataifa yakifumba macho mbele ya sauti yoyote inayotakia kukomesha vitendo hivyo vya kijinai dhidi ya Wapalestina.

Al-Azhar inasisitiza kuwa watu wote walio huru na waadilifu kuungana ili kumaliza ukaliaji ulio mbaya na wa muda mrefu zaidi katika historia ya kisasa, na kutoa juhudi kwa ajili ya kumaliza mateso ya Wapalestina na kuanzisha nchi yao huru ya Palestina na mji mkuu wake ni Al-Quds Al-Shareif, ikitoa salamu za maamkizi kwa wananchi walio huru kama vile Mayahudi, Wakristo, Waislamu na wengineo waliotoka barabarani ili kueleza kukataa kwao kwa vitendo vya mamlaka ya kizayuni dhidi ya Wapalestina, na kuimarisha juhudi kwa ajili ya kukomesha uadui na kuondoa mzingiro, ikitoa wito kwa ulimwengu mzima ili kuongeza misaada na kuchukua hatua zote za kuwalinda Wapalestina na kuunga mkono uvumilivu wao.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
3.0

Please login or register to post comments.