Wanadai .. Tunasahihisha

8

  • | Monday, 13 June, 2016

•    Kuwafanyia urafiki wale wasio waislamu hata wakiwa maadui si ukafiri bali ni uhalifu mkubwa ambao mtawala anapitisha adhabu kulingana na uhalifu huo kwa ajili ya kumzuia mwenye kufanya khiyana asifanye kitendo hicho lakini katika wakati huo huo yule aliyefanya hivyo hubaki mwislamu na wala haijuzu kuhukumiwa ukafiri, dalili ya hayo yaliyosimuliwa na Al-Bukhariy katika kitabu chake cha Sahihi  kwamba Ali (R.A.) alisema: "Mtume (S.A.W.) alinituma mimi na Az-Zubair na Al-Meqdad Bin Al-Aswad akisema nendeni mpaka mkifikia Rawda ya Khakh  ambapo mtakutana na Dhaiina  anaye kitabu (ujumbe) basi chukueni kitabu hicho (ujumbe), akasema Ali basi tukakwenda haraka haraka kwa farasi zetu mpaka tukafika Rawda hiyo tukakutana an yule Dhaiina, tukamwambia utoe kitabu (ujumbe), akasema: sina kitabu (ujumbe), tukasema: utatoa kitabu (ujumbe) au tutakulazimisha kukitoleza kwa nguvu, basi akakitolea kutoka nyewele zake, tukakichukua tukarudi nacho kwa Mtume (S.A.W.) tukagundua kwamba kitabu hiki au ujumbe ule ni: kutoka Hatibu Bin Abi Baltaa kwa baadhi ya washirikina wa Makkah akiwaambia kuhusu habari za Mtume (S.A.W.), hapo ndipo Mtume (S.A.W.) akasema: Ewe Hatib kwa nini umefanya hivyo? Aksema Hatib: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu usinihukumia kwa haraka, hakika mimi nilikuwa mmoja wa waliojiandama kwa Maquraiesh wala sikuwa na uhusiano wo wote na jamaa na ukoo wake kama vile (Muhajirun) maswahaba wako walio na husiano za kifamiliya na Maquraiesh kule Makkah ambapo jamaa zao na mali zao, nikataka kupata sababu ya kujiunga nao ili wawalinde jamaa yangu wanaoishi kule Makkah badala ya kutokuwa na uhusiano wo wote nao, na sikufanya hivyo kwa sababu nimekufuru au kuritadi au kwa kurdhika kwa ukafiri baada ya kusilimu, basi Mtume (S.A.W.) akasema: kwa kweli alisema ukweli, akasema Omar: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unipe ruhusa ya kumwua kwani ni mnafiki, akasema Mtume (S.A.W.) hapana kwani alishuhudia vita vya Badri na wewe hujui pengine Mwenyezi Mungu Aliwaambia waislamu waliopigania katika vita hivyo Akawaambia: fanyeni kama mpendavyo hakika nimekupeni maghufira, basi Mtume (S.A.W.) hakumwua wala hakusema kwamba Hatib Bin Abi Baltaa alikufuru"
Japokuwa alifanya uhalifu mkubwa mno ambapo mtawala anaweza kumpitishia adhabu inayoweza kufikia kunyongwa.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.