Wanadai .. Tunasahihisha

11

  • | Thursday, 16 June, 2016

Vipi haya! Ilhali Mtume (S.A.W.) ameishi na washirikina, Mayahudi na Wakristo, basi hawa wote wamemshuhudia vitendo vizuri vyake na maadili yake mema, hakupigana nao ila baada ya kumpigana na kumwudhu, na kumzuia kuishi akilingania dini yake kwa amani, lakini wasifu wake umethibitisha matendeano yake mema na jamii nyingine zote, bali alikuwa anashirikiana nao katika mambo yanyoifaa nchi? Bali vipi haya ilhali Mtume (S.A.W.) alikuwa akitembea jirani yake wa kiyahudi alipokuwa mgonjwa, na alimjia mwanamke wa kiyahudi aliyemwita kula basi akaenda kwake na akakula chakula alichokifanya? Kwa hakika Mtume (S.A.W.) hakuwasusia wala hakuwaamuru maswahaba wake kuwasusia, japokuwa Mtume (S.A.W.) anaijua zaidi Qurani ya Mwenyezi, na mcha mungu zaidi kuliko wao, kwa hivyo ndivyo namna alivyoifuata kutekeleza dini ya Mola, je tuchukue dini ya Mola kutoka kwa Mtume wake ama kutoka kwa wanaozidisha katika dini ya Mwenyezi Mungu mambo yasiyokuwepo!

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.