Wanadai .. Tunasahihisha

14

  • | Sunday, 19 June, 2016

Mwislamu anayeshuhudia kuwa hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammad (S.A.W.) ni Mtume wake hatoki kutoka Uislamu ila akikataa na kutokiri kwa tawhidi na utume wa Mtume mtukufu. Pia, ni jambo la kimaumbile kuwa Mwislamu ana dhambi kwani Mwislamu ni binadamu sio Malaika, na maumbile ya kibinadamu yanalazimika kufanya baadhi ya makosa na madhambi, na kwa kweli Mwenyezi Mungu ni Mola Mwenye kurehemu Apendaye msamaha na maghufira, ili kubainisha hayo inatosha kutaja kauli yake Mtume (S.A.W.): "Naapa kwa  Mwenyezi Mungu Ambae nafsi yangu iko mikononi Mwake lau hamtafanya madhambi, basi Mwenyezi Munngu Atawaangamizeni, Akawaumba watu wengine wanaofanya madhambi na kutubu wakiombea masamaha kutoka kwa Mwenyezi Munngu, naye huwasamehe" Katika Hadithi hii kuna alama wazi kuwa mwislamu hawi mkafiri kwa sababu ya kufanya hatia hata angekufa katika hali hii isipokuwa akifanya hatia hiyo ni halali.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.