Ramadhani Nchini Tanzania

  • | Tuesday, 12 March, 2024
Ramadhani Nchini Tanzania

 

 

Tanzania: Jina hilo limetokana na kuunganishwa kwa majina mawili ya Tanganyika na Zanzibar, yaliyounganishwa Aprili 26, 1964 ili kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani; Tanganyika na Zanzibar.

Tanzania iko katika eneo la Afrika Mashariki, inapakana na Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki, Kenya na Uganda kwa upande wa kaskazini, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wa magharibi, na Zambia, Malawi na Msumbiji kwa upande wa kusini.

 

Mji mkuu wake kwa sasa ni "Dodoma", ambapo ipo Bunge na baadhi ya ofisi zi kiserikali, hapo awali mji wa "Dar es Salaam" ulikuwa ni mji mkuu wa nchi hiyo, kwa sasa "Dar es Salaam" ni mji mkuu wa kibiashara nchini Tanzania, ambapo ni kituo cha aghalabu ya taasisi za serikali, sarafu rasmi ya Tanzania ni Shilingi ya Tanzania.

Watanzania wanazungumza Kiswahili; nayo ni lugha rasmi ya taifa, na lugha ya elimu katika viwango vyote vya elimu mpaka Chuo Kikuu, pia Kiswahili ni lugha ya mawasiliano kati ya watanzania wenyewe kwa wenyewe na kati ya watanzania na mataifa wengine wa Afrika Mashariki, wakati huu huu Kiingereza kinatumika katika mawasiliano ya kimataifa.

Tanzania ina kilomita 945,000 takriban, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wakazi wa Tanzania ilifika takriban milioni 61.741, kwa ongezeko la kila mwaka la 3.2%, kulingana na data iliyotolewa na Idara ya Takwimu na Hesabu ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Tanzania mnamo mwezi Oktoba 2022.

Hakuna takwimu rasmi kwa kuainisha idadi ya waislamu nchini Tanzania, lakini hali ya kisasa inashuhudia kwamba idadi ya Waislamu ni kubwa mno, hasa katika Zanzibar, ambapo Waislamu ni zaidi ya 95% ya wakazi wake. Kuna jumuiya na taasisi nyingi za Kiislamu nchini Tanzania, za ndani na nje, jumuiya zilizo mashuhuri zaidi ni: “Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania” (BAKWATA), “Baraza la Wanazuoni waislamu katika Tanzania” na taasisi ya “Al-Hikma” ya kuelimisha, kituo cha “Al-Haramain,” taasisi ya “Dhu Al-Nourin”, na taasisi nyinginezo nyingi zinazolenga kuleta mabadiliko mazuri kwa jamii ya Kiislamu nchini humo hasa katika nyanja za elimu, uchumi, afya, huduma na vyombo vya habari.

Watanzania wanaheshimu na kufurahia mwezi wa Ramadhani, ambapo wanaanza kujitayarisha tangu mwanzo wa mwezi wa Shaban, na hayo kupitia kwa kupamba mitaa, maduka na misikiti kwa taa, Watanzania wengi hufunga siku ya Jumatatu na Alhamisi ya kila wiki ya mwezi wa Shaaban mpaka Ramadhani, Watanzania kuanzia watoto wenye umri wa miaka 12 hadi wazee hufunga, pia ziara za kifamilia huongezeka kwa ajili ya kujiandaa kwa mwezi mtukufu, wakizingatia kufuturu mchana wa Ramadhani ni miongoni mwa madhambi makubwa zaidi, ambapo wanamshutumu anayefuturu ndani ya mwezi huu bila ya sanbabu ya kisheria kuwa ni "Mkana-Mungu", na mkafiri; kwa hiyo, magahawa hufunga - hata magahawa ya hoteli - hufunga muda wa Saumu na haifungui ila baada ya sala ya Magharib na wakati wa kufuturu; hata wasio waislamu wanaona aibu kula mchana wa Ramadhani.

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, waislamu wanatekeleza ibada mbalimbali, na husherehekea mnasaba za kidini, wakiwa na uhuru kamili wa kutekeleza ibada zao za kidini, aidha misafara ya Al-Azhar kutoka Misri inaongeza uelewa wa kidini kwa Waislamu wa Tanzania, jambo lililopelekea kuwepo kwa jamii ya Kiislamu inayoshikamana, na kuhifadhi mafundisho ya dini yake.

Na katika mwezi mtukufu huu mashirika ya hisani hutoa misaada ya kifedha kwa wahitaji na familiya maskini, na kuandaa meza za pamoja za futari kwa wasioweza kupata chakula, pia Waislamu wanasema misemo ya kukaribisha mwezi wa Ramadhani na kueleza furaha yao kwa mwezi huu, kama vile “Ramadhani Njema” “Ramadhani Kareem”.

Kuhusu wakati wa Futari, basi misikiti hapo zamani ilikuwa ikiutangaza kwa kupiga madufu, na Waislamu hula tende na maji yaliyotiwa sukari, mchele na mboga, pamoja na samaki, kuku au nyama. Miongoni mwa vyakula mashuhuru nchini humo; Bilau, Biryani, Ugali n.k.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.