Ramadhani nchini Kenya

  • | Thursday, 14 March, 2024
Ramadhani nchini Kenya

     Kenya: Ni nchi iliyoko mashariki mwa bara la Afrika, kwa upande wa kaskazini inapakana na Ethiopia na Sudan, na kwa upande wa Kaskazini-Mashariki inapakana na Somalia, kwa upande wa Kusini-Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi, kwa upande wa Kusini inapakana na Tanzania, kutoka magharibi inapakana na Ziwa la Victoria na Uganda. Kenya ilipata uhuru wake mwezi wa Desemba mwaka 1963. Lugha rasmi ya nchi ni Kiingereza, na Kiswahili ni lugha ya mawasiliano nchini, pamoja na lugha na lahaja nyingine za kinyeji.

Kenya ina eneo la kilomita za mraba 580,367. na idadi ya wakazi wake ni zaidi ya milioni 47.6. Waislamu nchini Kenya wanawakilisha takriban 35% ya idadi ya wakazi, sawa na zaidi ya Waislamu milioni 8, aghalabu yao wanaishi katika ukanda wa pwani katika miji ya "Lamu", "Malindi", na "Mombasa". Pia wanaishi ndani ya Kenya mjini Nairobi na pambezoni mwake, na pia katika ukanda wa Kenya unaopakana na Somalia. Baadhi ya Waislamu nchini Kenya ni wa jamii ya Wahindi na Pakistani, jamii ya Kiajemi, na pia jamii ya Waarabu.

Waislamu nchini Kenya wana vituo na taasisi kadhaa za Kiislamu, wakiongozwa na "Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya" nayo ni taasisi rasmi ya Waislamu mbele ya serikali ya Kenya, na inawasiliana na serikali ili kuunda sera zinazowahusu Waislamu, na kuhakikisha haki zao, na chini ya baraza hili yapo: "Baraza la wazee wa kiislamu" na “Baraza la Maimamu na Walinganiaji wa Kenya", na hizo zinazohusiana na masuala ya kidini na masuala ya misikiti nchini Kenya. Na miongoni mwa taasisi hizo ni "Kongamano la Viongozi wa kitaifa wa Kiislamu nchini Kenya"... na inajumuisha wawakilishi 15 wa mabaraza na taasisi za Kiislamu nchini, na ina matawi 6 katika majimbo ya Kenya, na ina jukumu la "ulinganiaji" wa Kiislamu ambao wanajibika kutetea masuala na haki za Waislamu.

Waislamu nchini Kenya wanajiandaa kupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia mwezi wa Shaaban, ambapo wanatayarisha misikiti, kuwasha taa zake kwa ajili ya sala na kusoma Qur'ani Tukufu, Pia, kuna ongezeko la halaqa za dhikr (Mabaraza ya Dhikri) na kusoma Qur'an, pamoja na kuongezeka kwa sadaka na matendo mema. Kuanzia usiku wa kwanza wa mwezi mtukufu, watu hutoka wakiwa na mienge na kuelekea pwani wakipiga madufu kuashiria kuwasili kwa Ramadhan, na hii inaendelea hadi daku.

Mojawapo ya mambo muhimu yanayoashiria mwezi wa Ramadhan nchini Kenya ni kuandaa futari (Iftar) ya pamoja kila siku za mwezi mtukufu, ambapo kila familia katika eneo au mtaa mmoja hutoa chakula chake na watu wote hukaa pamoja kwenye meza moja bila ubaguzi wa tajiri na maskini, na inazingatiwa kuwa ni aibu kutohudhuria futari hiyo ya pamoja.

Wazazi katika mwezi huu mtukufu wanajitahidi kuwafundisha watoto wao kufunga na kuwapeleka misikitini kuswali sala zote, hasa Taraweeh, na wanawasomesha dua zinazopokewa na Mtume (S.A.W.), na kuanza kwa siku kumi ya mwisho ya Ramadhani, basi wananza kusali sala ya Tahajjud na kukaa misikitini, kwa hakika kuna baadhi ya misikiti ambayo hukamilisha kusoma Qur-an mara tatu kupitia mwezi wa Ramadhani, kwa sababu wanaswali sala ya Taraweeh kila usiku kwa juzu tatu, aidha vikao vya pamoja hufanyika baada ya kumalizika kwa Swalah ya Taraweeh ambapo wafungaji saumu huzungumzia mambo ya dini yao, mbali na kubainisha njia za kutoa zaka zinazokusanywa katika mwezi wa Ramadhani na kuzipeleka kwenye njia zake halali ili kuwapa maskini na  kutomwacha mwenye njaa wakati wa Eid ul-Fitr.

Taasisi nyingi za Kiislamu huanza shughuli zao za kuwasaidia maskini na wenye mahitaji katika mwezi wa Ramadhan, aidha yanafanyika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, pia vituo vya televisheni na redio pia hutangaza programu mbalimbali za kidini ili kueneza dini ya Kiislamu na kujadili kila linalowashughuliwa na watazamaji.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.