Ramadhani nchini Zambia

  • | Saturday, 16 March, 2024
Ramadhani nchini Zambia

 

     Jamhuri ya Zambia: Ni nchi ya kusini mwa Afrika isiyopakana na bahari, ambapo kwa upande wa kaskazini inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kwa upande wa kaskazini mashariki inapakana na Tanzania, kwa upande wa mashariki inapakana na Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Botswana, na kwa upande wa kusini inapakana na Namibia, na kwa upande wa magharibi inapakana na Angola.

Eneo la Zambia ni takriban kilomita 752,618, na mji mkuu wake Lusaka, ambao uko kusini mwa nchi hiyo na unazingatiwa kuwa moja ya miji mikubwa nchini Zambia, nayo ni kituo cha biashara na makao makuu ya serikali.

Idadi ya Waislamu nchini Zambia inafika asilimia takriban 5% tu ya jumla ya wakazi wake, wakati dini ya Kikristo iko katika nafasi ya kwanza kwa asilimia 87%.

Uislamu ulifika Zambia na eneo la Afrika ya kati na kuanzishwa kwa falme za kiislamu maeneo ya pwani hii katika karne ya nne Hijriya, na ushawishi wa falme hizo ulienea hadi Msumbiji, kisha Daa’wa ya kiislamu ilienea barani kote kutokana na wafanyabiashara Waarabu na waislamu miongoni mwa waswahili.

Nchini Zambia zipo taasisi na jumuiya nyingi za kiislamu, kama vile; Jumuiya ya Kiislamu inayosimamia misikiti, Jumuiya ya vijana wa Kiislamu, ambayo wengi wa wanachama wake ni Wahindi na Wapakistani, na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu. Misikiti ya Zambia inaenea katika maeneo ambayo Waislamu wanakoishi, na misikiti hiyo mara nyingi hujengwa kwa gharama za watu binafsi.

Nchini Zambia, Mwezi mtukufu wa Ramadhani unashuhudia kuimarika kwa hisia za huruma, inayojitokeza na kudhihirika kupitia mshikamano kati ya watu, kukusanya michango, na kuwasaidia masikini kupitia kampeni zinazotekelezwa kwa ajili ya lengo hilo.

Waislamu nchini Zambia wanashughulikia sana kutumia wakati wao misikitini ili kuswali na kuabudu, wakishindana kufanya vitendo vya kheri ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu, pamoja na sura mbali mbali za kuutukuza mwezi huu kama vile; kuswali sala ya Tarawihi na kutoa sadaka .

Daku ni chakula muhimu katika mwezi wa Ramadhani, na waislamu wanashughulikia kula vyakula vyepesi kama vile chizi nyeupe mkate, pamoja na kunywa maziwa na vinywaji mbalimbali ili kuhifadhi nishati yao wakati wa kuongezeka kwa joto kupitia siku.

Kwenye meza ya futari nchini Zambia kuna aina kadhaa za juisi, ili kuipa miili kile kilichopotea kupitia siku nzima wakati wa joto, pamoja na aina nyingi za matunda, pamoja na sahani ya "Gollaf", ambayo ni sahani ya wali inayo na aina tofauti za viungo na mboga

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.