Ramadhani nchini Uganda

  • | Monday, 25 March, 2024
Ramadhani nchini Uganda

 

     Mwezi wa Ramadhani nchini Uganda una sifa ya mila nyingi za ajabu ambazo bado zipo leo, mojawapo ya mila hizi ni kwamba wanaume wa kabila la "Lango" la Uganda bado wanadumisha desturi ya kumpiga mke kichwani kabla ya kufuturu ili kumtahadharisha kuandaa chakula, na kama mume hampigi, basi anakasirika na kujizuia kuandaa chakula.

Pia miongoni mwa mila maarufu ya Uganda ni kwamba watoto hukusanyika wakati wa jua kutua kabla ya kufuturu na kuwaita watu wazima wa familia zao kula chakula cha kufuturu nyumbani iliyochaguliwa na watoto. Siku inayofuata, watoto huchagua nyumba nyingine ya kula chakula cha kufuturu, na kadhalika hadi mwisho wa mwezi mtakatifu.

Misikiti ya Uganda pia hupambwa kwa mnasaba wa kuingia kwa mwezi wa Ramadhani, na meza za kufuturu huwekwa humo. Watoto husherehekea kila usiku kwa ngoma, na inapofika wakati wa suhuur hula chakula kisha huswali sala ya alfajiri kwa jamaa, mila hizi hutokea kila siku katika mwezi mzima wa Ramadhani.

Nchini Uganda, ndizi huzingatiwa kwamba chanzo kikuu cha chakula, kwa hivyo watu wanaofunga hula kama ni kiungo kikuu katika chakula cha kufuturu na cha suhuur, na hutumiwa katika mlo maarufu wa ndani unaojulikana kama "matoki" unaozingatiwa ni chakula kimsingi cha kufuturu nchini Uganda.

Kujazwa kwa Msikiti wa "Ondaje" - msikiti mkubwa zaidi katika mji mkuu, Kampala - na waumini katika kufuturu ya pamoja inazingatiwa kwamba moja ya maonyesho muhimu zaidi ya Ramadhani nchini Uganda, hasa kwamba meza kubwa ya Al-Rahman inaandaliwa kwa ajili ya kukusanya Waislamu wa Kampala humo, ili kula chakula cha kufuturu pamoja. Siku kumi za mwisho za Ramadhani ni muhimu sana kwa watu wa Uganda, kwani wanazipokea kwa kusoma Qur-aan, dhikr, na tahajjud.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.