Wanadai .. Tunasahihisha

17

  • | Wednesday, 22 June, 2016

Ukweli kuwa aya za (Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu...) zimeteremshwa kuhusu Mayahudi, kwa hiyo Maulamaa wa tafsiri wameambatana kuwa kutoa hukumu kwa kutegemea yasiyoteremshwa na Mwenyezi Mungu ni hatia lakini haiwi ukafiri ila akitangaza ukafiri wake kwa Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu au kwamba anaamini kuwa zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu hayafai au kusema kuwa sheria za kibinadamu ni nzuri zaidi kuliko sheria za Mwenyezi Mungu.
Vile vile ukafiri uliyotajwa katika aya hizo hazimaanishi kutoka nje ya dini, ambapo neno la ukafiri lina maana kadhaa na  tofauti katika Lugha ya Kiarabu, inaongezeka kuwa Maswahaba walipofasiri aya hizo, wametoa maelezo mbali mbali ambapo baadhi yao wamesema kuwa: “Ni ukafiri usio kamili kwa maana hausababisha kutoka nje ya Uislamu, na baadhi yao  wamesema kwamba aya hizo hazihusiani kabisa na waislamu, na wakaapa kuwa aya hizo zinahusiana na mataifa waliotangulia ambao walikana vitabu vyake wakatunga sheria zinazoafikiana na matakwa yao wenyewe wakadai kuwa ni zile zile hukumu zilizopitishwa na Mwenyezi Mungu bali ni nzuri zaidi!

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.