Kiini cha ujumbe wa Uislamu kinajikita zaidi elimu kwa kuwa elimu ndiyo sababu ya kuendelea na kustawi kwa umma wowote, tena ni sababu ya kushinda na kuvuka changamoto yoyote na njia ya kumfikisha mtu kwa namna sahihi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu na kulazimika kwa maamrisho yake na kuepukana na makatazo yake.
Uislamu ulizingatia sana suala la elimu na kusisitiza kuwa elimu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa jumla. Inatosha kujua kwamba neno la kwanza lililoteremka kutoka Qurani Takatifu ni neno la: “Soma” na kusoma ni ngazi ya kwanza kabisa ya kujifunza na kupata elimu, jambo linalothibitisha kutoka mwanzo wa dini kwamba dini hiyo ni dini ya elimu, uelewa, ufahamu kwa ajili ya kufikia ustawi, maendeleo na mafanikio kwa jumla.
Mwenyezi Mungu (S.W.) katika aya za mwanzo kabisa kuteremka kutoka Qurani Takatifu kwa Mtume (S.A.W.) Amesma: {Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba * Amemuumba binaadamu kwa tone la damu * Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! * Ambaye amefundisha kwa kalamu * Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui} Al-Alaq: 1-5.
Vile vile aya nyingi mno zimehitimishwa kwa kuwahimiza waislamu na watu wote kutafuta elimu na kubainisha kuwa wanao elimu na ambao hawana kwa mtazamo wa Uislamu hawako sawa sawa, bali wale ambao wamepata kiasi cha elimu huwa katika cheo cha juu zaidi na wanategemewa kuwa msingi wa maendeleo kwa umma wao, Mwenyezi Mungu Ametwelezea kuwa wanaojua na wasiojua wako katika vyeo na ngazi mbili tofauti kabisa, ambapo Alisema: {Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu nakusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehemaza Mola wake Mlezi...Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka niwatu wenye akili} Az-Zumar: 9.
Naye Mtume (S.A.W.) aliwafaradhishia waislamu kutafuta elimu akabainisha ubora wa mtaalamu kuliko anayefanya ibada ilhali hana kiasi chochote cha elimu. Uislamu unawaita wafuasi wake kujifunza na kufundisha na ukawapa wataalamu nafasi kubwa katika dini. Kwa kuwa vijana ndio nguzo iliyo muhimu zaidi kwa umma wowote wanatakiwa kuwa na elimu ya kutosha kwa ajili ya waweze kukabiliana na mawimbi ya kuwavutia wajiunge na fikra kali na misimamo ya kigaidi.
Kwa hakika majaribio ya kuwashawishi vijana yako mengi na yanaendelea kwa kutambua nafasi yao kujenga au kuangusha umma wowote, jambo linalotulazimisha kuwahimiza vijana wetu hawa wajiknga na majaribio ya ushawishi haya na kupambana na shughuli za kuwavutia kwa njia mbaya hii. Kinga hiyo haitapatikana isipokuwa kwa yule anaye elimu ya kutosha kumwelekeza kwenye njia iliyo sawa na kumjulisha namna ya kuepukana na njia isiyo sahihi. Kwa kuwa wafisadi wanao jitahitahidi sana kuzichafua akili za vijana na kuwatumia vibaya kuziharibu jamii na kusababisha maangamizi mabaya, kwa ajili ya hali hii tunatakiwa kufanya jitihada kubwa zaidi kuliko kwa ajili ya kuwakinga na kulinda vijana wetu kutoka shari na fitina hizo.
Inafahamika kuwa elimu ni msingi mojawapo misingi ya maendeleo ya umma na sababu ya mafanikio, kwa hiyo, jamii isiyo na elimu ya kutosha huwa jamii rahisi kushawishiwa na kuharibika, huku jamii inayohimiza wananchi wake kujifunza fani mbalimbali za elimu ya sheria, dini na sayansi za kiutendaji.
Kwa hakika makundi ya kigaidi yanakusudia kuwavuta vijana ambao akili zao ziko tupu hazina elimu wala mafunzo yoyote yanayoweza kuwasaidia kutambua yaliyo sahihi na yaliyo kosa. Japokuwa baadhi ya waliovutwa na makundi haya walikuwa wameshapata kiasi cha elimu lakini si kiwango wala aina ya elimu kinachowalinda kutoka kwa hatari ya kushawishiwa na kuathirika kwa fikra hizo.
Inafahamika kwamba wafisadi wanaotaka kueneza vurugu na ugaidi duniani wanakusudia kuwatumia vijana kwa kuwa vijana hawa wana nafasi kubwa zaidi kuliko katika umma wowote ambao wana uwezo wa kubadilisha hali halisi ya mambo, jambo linalosisitiza ukweli wa kwamba vijana hawa ndio silaha muhimu zaidi kwa umma wowote. Kwa hivyo, kuwaelimisha vijana hawa na kuwakinga kutokana kwa fikra mbaya na maoni yanayowaelekeza kwenye njia za ukatili, vurugu na ugaidi.
Inatajwa pia kwamba vijana ndio msingi wa maendeleo ya umma na tegemeo la mwamko wake, kwa sababu vijana ni ukwasi ulio ghali wa umma, maana umma wowote huwa na hazina mbalimbali .. hazina za kiuchumi, kijeshi, kijiografia, na za kibinadamu, lakini hazina iliyo muhimu zaidi kwa umma ni hazina ya kibinadamu, ile hazina ambayo inaundwa na kuimarika sana kwa vijana.
Kama ungetaka kujua mustakabali wa taifa lolote, basi usiuliza juu ya dhahabu yake na hazina yake ya kifedha, lakini unaweza kuangalia vijana wake na mambo gani wanayoshyghulikia nayo,basi ukiwakuta vijana hao wanashikilia Dini, basi utambue kuwa ni taifa kubwa lenye hadhi nzuri na ujenzi nguvu, ama ukiwakuta vijana hao ni wamepoteza maadili wakawa na tabia mbaya wakishughulikia mambo duni na maovu, basi ujue kuwa ni taifa dhaifu (nyonge), litakaoanguka kwa haraka mbele ya madui wake, kwa hivyo basi vijana ni msingi wa umma na sababu ya kuimarika au kuanguka kwake.
Vile vile, shughuli ya kupambana na ugaidi wa kifikra ingalianza mapema, ingalikuwa na manufaa makubwa, pamoja na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo na kushauriana kama ni suluhisho lenye athari kubwa kumaliza hali hiyo, ambapo mazungumzo ni mtindo na mbinu unaofaa kuunda dhana sahihi na kubainisha haki na kudhihirisha ufisadi wa baadhi ya itikadi, tuhuma na fikra, pamoja na kunufaika na wanavyuoni wa sheria, wataalamu wa kisaikolojia na kijamii, kwani wana elimu, maarifa na uzoefu.
Kwa hiyo, wanaweza kuwakinaisha wale walioathirika kwa fikra za kigaidi, na kurekebisha istilahi potofu na maoni mabaya waliyo nayo kuhusiana na familia, jamii na nchi nzima. Mashirika, Taasisi na mamlaka watakiwa kupambana na magaidi hawa, kwa lengo la kufanya hivyo ili wale ambao wameshawishiwa kuharibu nchi, kufanya vurugu na mauaji, kusababisha ghasia na uharibifu wa aina yoyote waelewe kuwa wanafanya hatia kubwa zilizokatazwa katika sheria ya kiislamu.