Mheshimiwa Imamu Mkuu, Profesa/ Ahmad Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar, amempokea leo Jumatatu, katika makao makuu ya Al-Azhar, Bwana Denis Bashirovic, Rais wa Bosnia na Herzegovina; ili kujadili masuala muhimu na changamoto zinazoukabili ulimwengu wetu wa kiislamu.
Imamu Mkuu alimkaribisha Rais wa Bosnia katika Al-Azhar, akisisitiza kwamba ziara hii ni muhimu sana kwani ilikuja sambamba na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na wazayuni dhidi ya ndugu zetu katika Ukanda wa Gaza, yanayofanywa fedheha kwa ubinadamu, yanatukumbusha kwa mauaji ya kimbari yaliyotokea dhidi ya waislamu wa Bosnia, na yanatukumbusha sisi Waislamu kwa ulazima wa kuungana pamoja, kwani hiyo ndio suluhisho na njia ya pekee ya kutoka nje ya machafuko hayo yanayofuatana.
Sheikh wa Al-Azhar ameongeza kuwa, tatizo la kweli la kila kinachotokea dhidi yetu linatokana na udhaifu wa majibu ya kiislamu na Kiarabu, na msingi wa tatizo hilo ni hali ya udhaifu unaotokana na kutawanyika na kugawanyika vipande vipande kwa umma wetu, ambao Qur’ani Tukufu ilituonya kutoka kwake aliposema ALAAH: {wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu} yaani: kudhoofika na nguvu zenu kupotea, akaongeza Imemu Mkuu: "tunahuzunika sana tunapogundua kuwa sisi tunamiliki vyanzo vingi vya nguvu, na tunahuzunika sana tunapojua kwamba viwanda vya Amerika na Magharibi vinategemea juu ya rasilimali za wananchi wa ulimwengu wetu wa Kiarabu na kiislamu.”
Imamu Mkuu alieleza utayari wa Al-Azhar wa kuanzisha kituo cha kufundisha lugha ya Kiarabu katika mji mkuu wa Bosnia, Sarajevo; ili kuwafundisha watoto wa waislamu huko lugha ya Qur'ani Tukufu na kuwasaidia kushikamana na utambulisho wao wa kiislamu, na utayari wa Al-Azhar wa kutoa fursa isiyo ya mipaka ya kusoma kwa watoto wa Bosnia na Herzegovina ya kujifunza katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na kupokea maimamu wa Bosnia na kuwapa mafunzo, na kuinua ujuzi na uwezo wao katika kukabiliana na masuala ya kisasa, pamoja na kufunguliwa kwa ofisi ya kikanda ya Baraza la waislamu wenye hekima huko Sarajevo, ili kuwahudumu watoto wa waislamu katika Bosnia na Herzegovina na kutoa msaada kwao.
Kwa upande wake, Rais wa Bosnia alielezea furaha yake kwa kukutana na Mtukufu Imamu Mkuu, akisisitiza kuwa, kinachotokea Gaza ni fedheha kwa binadamu, nayo ni mgogoro wa kimaadili, akiashiria umuhimu wa hati ya udugu wa kibinadamu, ambao ulitiwa saini na Imamu Mkuu na Baba Francis, na kwamba ni kama hati muhimu zaidi ya kimaadili iliyotiwa saini katika zama hizi, basi lazima kuzingatia kanuni zake na kueneza masharti yake, hasa wakati huo.
Rais wa Bosnia amekaribisha kuanzishwa kwa kituo cha kufundisha lugha ya Kiarabu katika mji mkuu wa Sarajevo na alitoa mwaliko rasmi kwa Sheikh wa Al-Azhar ya kutembelea Bosnia na Herzegovina, na kwa upande wake Imamu Mkuu alikaribisha mwaliko huo, akisisitiza kwamba ataitikia mwaliko hiyo haraka iwezekanavyo.