Vidhibiti vya Kazi ya Mwanamke kwa Mtazamo wa Kiislamu

Imeandaliwa na Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Monday, 24 June, 2024
Vidhibiti vya Kazi ya Mwanamke kwa Mtazamo wa Kiislamu

 

      Hakika Mwenyezi Mungu Ameviumba viumbe kwa kila aina, umbo, jinsia na maumbile, Akahsuisha kila kiumbe na kazi na jukumu maalum, ambayo hakuna mtu mwingine anaye uwezo wa kuyafanya isipokuwa yeye, na hilo ni jambo lililojulikana kwa wataalamu  wa vitu hai kwa jina la (Uwiano wa Mazingira). Miongoni mwa viumbe hivyo mwanadamu aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu akiwa na jukumu lililo tukuka zaidi la kumwabudu Mwenyezi Mungu kutokana na Aliyoyasema Mwenyezi Mungu: {Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi} [Adh-Dhariyaat: 56]. Pia, inajulikana kuwa Mwenyezi Mungu Alipoviumba viumbe vyenye uhai Amevigawanya katika jinsia mbili; vya kume na vya kike, Akiainisha sifa, majukumu na kazi maalum kwa kila jinsia, kwa mujibu wa maumbile na tabia yake.

Maumbile ya kibinadamu yanawajibika kuwa mwanamme yeye ndiye anayetakiwa kutoka nyumbani kwa ajili ya kutafuta riziki kupitia kazi, ama mwanamke kazi yake humo humo nyumbani, kwani nyumba ni mahali pa kawaida kwa mwanamke ambapo sifa zake za kike na pia matokeo yanayotarajiwa kutoka yule mwanamke, licha ya kumlinda kutokana na mabaya yanayoweza kumpata akitoka nje ya nyumba yake (aghalabu). Kwani mwanamke kwa kukaa nyumbani huepukana na maovu, fitina na ushawishi, na kuweza kuzingatia urembo wake na hali yake kwa jumla bila ya kusumbuliwa na yeyote. Vile vile, mwanamke kwa kukaa ntymbani huwa na utulivu wa kiroho na wa kiakili, jambo linalomsaidia kutunza nyumba na kutekelez majukumu yake humo.

Kwa kweli kuunda na kutunza famili ni kazi kubwa mno, inayotegemea mwanamme na mwanamke ambao ni mume na mke, wanaasisiwa nyumba na familiya, kila mmoja ana wajibu zake anazotakiwa kufanya, ambapo mwanamme anatakiwa kugharamika matumizi ya fedha ya kuendesha maisha ya familiya yake kwa hiyo huwajibika kufanya kazi ili apate fedha za kutosheleza mahitaji ya familiya yake. Wakati huo huo, mwanamke ana wajibu wa kutunza nyumba na kuwalea watoto na kutekeleza majukumu mengine nyumbani mwake.

Inafahamika kwamba wajibu ambazo mwanamke anatakiwa kuzitimiza kwa nyumba na familiya ziko nyingi na nzito kwa kiasi ambacho kinambidi atumie wakati wake wote na juhudi zake kufanya kazi zake hizo. Kwa kuwa mwanamke anatakiwa kuwatunza watoto, nyumba, vyakula na mengine mengi, basi mazingira yanayofaa kwa mwanamke kupata mafanikio na ufanisi ni nyumba yake, kwa hiyo akifanikiwa katika kazi yake hii akitekeleza wajibu zake barabara huwa sababu ya msingi kuunda familiya yenye furaha, amani na utulivu ambayo huwa msingi mzuri wa kizazi kizuri kwa jamii.

Lakini tukihusisha mwanamke kazi ya nyumbani bila ya kumruhusa kuatoka na kufanya kazi nje ya nyumba tutapata shida kubwa, kwani kuna baadhi ya kazi zinazomtegea mwanamke si mwanamme kama vile matibabu ya uzazi kwa wananwake, kuwafundisha watoto na wananwake. Kwa hiyo, umma wanatakiwa kuandaa baadhi ya wanawake wanaoweza kushughulikia mambo haya, kwa ajili ya kukidhi haja ya jamii kuhusu mambo haya. Kama kwamba kuna baadhi ya majukumu ambayo yanafanywa na baadhi ya watu kama vile katika vita na kuitetea nchi, aidha kazi kama hizi zinazohusishwa zaidi kwa wanawake huwa hali hiyo hiyo, kwa kuainisha baadhi ya wanawake wanaoshughulikia mambo hayo kutokana na uwezo wao.

Kwa hakia, Uislamu imezingatia sana masuala yanayomhusu mwanamke, ikabainisha kazi inayofaa zaidi kwake ambayo ni kutunza nyumba kama tulivyoeleza hapo juu, akiamrishwa kuwa na heshima wala asifanye mambo yanayovunja heshima yake na kusababisha ulaghai. Mwenyezi Mungu Amesema: {Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani} [Al-Ahzab: 33]. Inaonekana kuwa aya hii ina ishara ya kibalagha ambayo ni: kwamba Mwenyezi Mungu (S.W.) Amezihusisha nyumba kwa wanawake kwa maana ya kubainisha kuwa nyumba hizo ndizo makazi ya wanawake na makao yao ambayo hawana mahali popote pengine pa kwenda isipokuwa hizi nyumba zao, kwani nyumba kwa mwanamke ni kazi, malazi na makazi, ila akitoka kwa kazi kwa ajili ya dharura.

Vile vile, Uislamu imemwondoa mwanamke baadhi ya wajibu na majukumu ambayo mwanamme anatakiwa kulazimika nayo kwa sababu ya maumbile na hali yake. Miongoni mwa wajibu hizo; Swala ya Jamaa na Swala ya Ijumaa. Ambapo mwanamke hana budi kutoka kuswali msikitini wala pamoja na waumini wengine. Bali sheria ya kiislamu imebainisha kwamba bora kwa mwanamke aswali nyumbani mwake. Ibnu Omar (R.A.) alisimulia kwamba Mtume (S.A.W.) alisema:"Msiwazuieni wake zenu kwenda misikitini na kusawli majumbani ni bora kwao". Hata hivyo, Uislamu haikuwakataza wanawake kutoka kwa ajili ya Swala msikitini lakini iliwaruhusia hivyo na kuwashauri wanaume wasiwazuie wake zao kwenda misikitini sharti mwanamke atoke kwa idhini ya memewe akijisitiri kwa mavazi ya kiislamu (Hijab) wala wasisababisha kuwashawishi watu.

Uislamu kama ilivyompa mwanamke haki ya kutoka ilimpa mumewe haki ya kuombwa idhini, hilo linaelezwa katika hadithi iliyosimuliwa na Ibn Omar (R.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) alisema: "Yeyote kati yenu mke wake aliomba ruhusu ya kwenda msikitini asimzuia". Inatajwa kuwa sababu ya kuwa swala ya mwanamke nyumbani ni bora kuliko msiktini ni kuepukana na fitina na ushawishi, wakati huo huo kwa ulaini wake Mtume (S.A.W.) hakuwakataza kutoka kwa ajili ya Swala msikitini, bali alimruhusia mwanamke kusali msikitini sharti amwombea mumewe ruhusa yake na kuwajibika adabu za msikiti kuhusu mavazi n. k.

Sheria ya kiislamu ilipokuwa inatambua haki za mwanamke kuwa na kazi hasa katika shughuli ambazo zinabidi kufanywa na mwanamke, iliainisha vidhibiti na masharti maalum kwa kazi ya mwanamke kwa mtazamo wa kiislamu, vidhibiti hivyo na masharti haya ni pamoja na:

  1.   Kazi iwe inafaa kwa mwanamke kimwili, kimaumbile na kiroho kama vile kufanya kazi katika sekta ya elimu, kuwatunza watoto na kutoa huduma za matibabu kwa wanawake.
  2. Kazi isipingane na jukumu lake la msingi la kutunza nyumba  na familiya yake (mume na watoto), maana nyumba yake isiathiriki vibaya kutokana na kazi yake hiyo.
  3. Kazi iwe baada ya kuomba ruhusa ya waliy yake ambaye ni wazazi au mume akiwa ameolewa.
  4. Kazi iwe haina maovu wala vitu vilivyo haramu kisheria kama vile uasherati n. k.
  5. Atoke akiwa mcha Mungu na kuwajibika mwenendo wa kiislamu na tabia zilizo bora kimaneno na kivitendo na aepukana na kuwa sababu ya kuwashawishi wengine wala hakubali kushawishika na wengine.
  6. Awajibike kwa mavazi ya kiislamu na adabu Alizozieleza Mwenyezi Mungu (S.W.) katika kauli yake: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao,na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao} [An-Nuur: 31].

    Hivyo ni baadhi ya vidhibiti na adabu za kisheria ambazo mwanamke anatakiwa kulazimika nazo wakati wa kutoka kwa kazi (akiwa amedharurika) ili apate ridhaa ya Mwenyezi Mungu na afanikiwe duniani na Akhera, na kwa lengo la aweza kutimiza kazi yake ipasavyo kama ilivyopitishwa ksheria.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.