Waziri wa Mambo ya Nje afungua toleo la nne la kongamano la Aswan la amani na maendeleo endelevu barani Afrika

  • | Wednesday, 3 July, 2024
Waziri wa Mambo ya Nje afungua toleo la nne la kongamano la Aswan la amani na maendeleo endelevu barani Afrika

 

     Bwana Sameh Shokry, Waziri wa mambo ya nje, alifungua Jumanne asubuhi, Julai 2, shughuli za toleo la nne la kongamano la amani na maendeleo endelevu barani Afrika mjini Aswan, nchini Misri, ambapo kongamano hilo litachukua muda wa siku mbili na 2,3 Julai 2024, chini ya anuani ya “Afrika katika ulimwengu Unaobadilika...

Kikao cha ufunguzi kilihudhuriwa na Bw. Moussa Faqih, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Ahmed Abo El-Gheit, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu, baadhi ya mawaziri wa Afrika na wajumbe wa ngazi za juu wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, maafisa, pamoja na wawakilishi wa mashirika muhimu zaidi ya kikanda na kimataifa yanayohusika na masuala ya amani na usalama, pamoja na idadi kubwa ya watu wakuu wa Misri, kikanda na kimataifa, washirika wa maendeleo, wanafikra, waandishi wa habari, wanahabari na watafiti.

Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Umma, alisema kuwa Bwana Sameh Shoukry alisisitiza katika hotuba yake ya ufunguzi kwamba mkutano huo ambao linafanyika chini ya uangalizi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, umeimarishwa tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2019 wakati wa urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika, na katika matoleo yake mfululizo, kama mkutano unaochangia kufikia maono ya pamoja ya njia za kukabiliana na changamoto hizo, kupitia kuunga mkono juhudi za kuzuia migogoro, kujenga amani, na kuimarisha uhusiano kati ya amani endelevu na maendeleo, pamoja na kuimarisha thamani ya ushirikiano, kwa kuzingatia misingi kadhaa, hasa kuheshimu kwa umiliki wa kitaifa, na manufaa ya pande mbili.

Balozi Abu Zeid aliongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje alisema kwamba mkutano huo unafanyika katika wakati eneo hilo na duniani nzima, inashuhudia changamoto kubwa na kuongezeka kwa vita, migogoro mikubwa isiyo na kifani ambayo inahitaji haja ya nchi za Afrika kupitisha maono ya kina ili kukabiliana na changamoto za Amani, usalama na maendeleo.

Bwana Sameh Shoukry pia alibainisha katika hotuba yake kwamba toleo la nne la mkutano huo utashuhudia uzinduzi wa mipango inayoimarisha umiliki wa Afrika katika juhudi za amani na usalama, na kuzinduliwa kwa mtandao mpya wa Kiafrika wa kuzuia fikra kali zinazosababisha ugaidi. Pia alitangaza kuwa Tuzo la "mkutano wa Aswan" ili kujenga tena na maendeleo, ambalo litatolewa kwa mara ya kwanza kwa mmoja wa wanamitindo wa Kiafrika ili kuthamini juhudi zake katika kujenga amani katika bara la Afrika.

Pia, Waziri wa Mambo ya Nje alizungumzia machafuko kadhaa yanayotokea katika nchi za kiafrika, na umuhimu wa juhudi za pamoja za kikanda na kimataifa za kusaidia uimarishaji wa usalama na utulivu katika bara hilo, akisisitiza kuwa Misri inaona umuhimu wa kutumia msingi wa suluhisho za Kiafrika kwa matatizo ya kiafrika, mbali na nchi za nje ambayo inachangia kuleta hali ngumu katika baadhi ya nchi za Kiafrika. Ama kuhusu mzozo wa Sudan, Shukri alitaja juhudi za Misri zinazoendelea ili kumaliza vita nchini Sudan.

 

Chanzo: Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri

Tafsiri: Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra potofu

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.