Rais wa Indonesia Ampokea Sheikh wa Al-Azhar Mwenyekiti wa Baraza la Wakuu wa Waislamu katika Ikulu ya Rais Mjini mkuu wa Indonesia Jakarta

  • | Tuesday, 9 July, 2024
Rais wa Indonesia Ampokea Sheikh wa Al-Azhar Mwenyekiti wa Baraza la Wakuu wa Waislamu katika Ikulu ya Rais Mjini mkuu wa Indonesia Jakarta

Rais Joko Widodo, Rais wa Indonesia, alimpokea mheshimiwa Imamu Mkuu profesa. Ahmed Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, kwenye ikulu ya Merdeka katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta, ili kujadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja.

Rais wa Indonesia alimkaribisha Sheikh wa Al-Azhar nchini Indonesia, akisisitiza umuhimu wa ziara hii kwa watu wa Indonesia, kwa sababu ya nafasi kubwa ambayo Sheikh wa Al-Azhar anamiliki kwenye Waindonesia, Azhar Al-Sharif ni marejeo ya kwanza kwa Waislamu wa Indonesia katika sayansi ya Kiislamu na Kiarabu, kwa hivyo tunatafuta kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma katika Al-Azhar; Kwa sababu wao ndio ni kama ngome imara inayosaidia kulinda nchi yetu na vijana wetu kutoka mawazo ya fikra kali.

Rais wa Indonesia pia alisema kwamba Indonesia inataka kuimarisha uhusiano wake na Al-Azhar, hasa katika uwanja wa kutoa mafunzo kwa maimamu na walinganiaji katika Chuo cha Kimataifa cha Al-Azhar, na kuimarisha ushirikiano kati ya Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali na vituo vya Indonesia vinavyofanya kazi katika uwanja huo huo.

Rais wa Indonesia alimshukuru mheshimiwa Imamu Mkuu kwa sababu ya kuwakaribisha wajumbe wa wataalamu wa Indonesia, akibainisha furahi ya Indonesia kwa tangazo la Al-Azhar kuhusu mpango wake wa kimataifa wa kueneza lugha ya Kiarabu, na akaeleza hamu ya Indonesia ya kuanzisha vituo kadhaa vya Al-Azhar vya kufundisha Kiarabu katika majimbo mbalimbali ya Indonesia.

Rais Joko Widodo amesisitiza kwamba Indonesia inafuata misimamo yote ya Imamu Mkuu kuhusu kuunga mkono masuala ya ulimwengu wa Kiislamu, hasa misimamo yake ya heshima katika kuunga mkono Ghaza na kukataa hujuma dhidi ya raia wasio na hatia, akisifu msimamo wa Misri katika kurahisisha kuingia misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza tangu mwanzo wa uadui,  akithibitisha kwamba msimamo wa Sheikh wa Al-Azhar unaafikiana na msimamo wa Indonesia.

Kwa upande wake Sheikh wa Al-Azhar alielezea furaha yake kwa kuzuru Indonesia, na shukrani zake kwa upendo mkubwa na shukrani alizopata kwa Al-Azhar nchini Indonesia, akibainisha kwamba hii ni mara ya tatu kwake ya kuzuru Indonesia. Nchi kubwa zaidi ya Kiislamu kutoka idadi ya watu, na alielezea kushukuru kwake kwa juhudi za rais wa Indonesia katika kuihudumu nchi yake, akisisitiza kwamba uhusiano kati ya Indonesia na Al-Azhar ni uhusiano wa kihistoria, na kwamba wanafunzi wana jukumu kubwa katika kuimarisha uhusiano huu.

Sheikh wa Al-Azhar alithibitisha pia jitihada za Al-Azhar za kukidhi mahitaji yote ya Indonesia kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokuja ili kusoma katika Al-Azhar, kuongeza kozi kwa maimamu wa Kiindonesia huko Al-Azhar, kuanzisha vituo vya kufundisha lugha ya Kiarabu nchini Indonesia, na kufungua mlango wa ushirikiano kati ya vyuo vikuu na vituo vya utafiti vya Indonesia.

Sheikh wa Al-Azhar akasisitiza pia ulazima wa kukusanya juhudi za kimataifa ili kukomesha uadui dhidi ya Gaza, umuhimu wa mshikamano wa Kiaarabu na Kiislamu, na kuleta msimamo mmoja na madhubuti ili kukomesha umwagaji damu wa kila siku huko Gaza. Akisifu msimamo wa Indonesia wa kuunga mkono Gaza kwa kuimarisha misaada na misafara ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza kwa ushirikiano na Al-Azhar.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.