Wanadai .. Tunasahihisha

30

  • | Tuesday, 5 July, 2016

Kwa hakika haya ni madai batili ni uongo mkubwa, ambapo Mtume Muhammad (S.A.W.) alikuwa anawahimiza maswahaba wake kusimulia hadithi zake kimatamshi kama walivyozisikia kutoka kwake (S.A.W.), na alikuwa akiomba kufanya hivyo mara kwa mara, Mtume (SAW) amesema: "Mwenyezi Mungu ampe nuru yule mtu ambaye amesikia baadhi ya maneno yangu akayaambia kwa wengine kama alivyoyasikia, pengine anayeambiwa kupata ufahamu mzuri zaidi kuliko aliyesikia binafsi”.
Na miongoni mwa dalili zilizosisitiza  kuhimiza kwa Mtume (S.A.W.) kusimulia hadithi zake kimatamshi ni ile iliyonukuliwa na Al-Bukhariy toka hadithi ya Al-Baraa Bin Aazib (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) amesema; utakapofika wakati wa kulala, basi tawadha kama unapokwenda Swala, kisha lala upande wako wa kulia, kisha sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nimejikusalimisha nafsi yangu, nimekuachia mambo yangu, na nimeuweka mgongo wangu karibu nawe, nikikutarajia na kukuogopea, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa isipokuwa kwako, nimekiamini kitabu chako Ulichokiteremsha na Mtume wako Uliyemtuma, basi ukifa katika usiku huo basi umekufa ukiwa na maumbile ya mwanzo kabisa – kidini – na uyahifadhi maneno haya daima ukiyafanya ni maneno ya mwisho kwa kila siku maishani mwako. Al-Baraa alisema: nikasema maneno haya kutoka kwa Mtume (S.A.W.) hata nilipofika kauli yake: na nikaamini kitabu chako ulichokiteremsha na Mtume wako uliyemtuma, nilisema: Mtume, akasema: hapana bali sema: na Nabii wako uliyemtuma."
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.