Imeandaliwa na Dkt., Hossam Mostafa
Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinaendelea kutoa sehemu ya pili ya mfululizo wa makala zinazohusu baadhi ya mifano angavu katika tarehe ya mafanikio ya bara la Afrika ya wanawake mashuhuri ambao wako hai au walioaga dunia, lakini kumbukumbu zao zimesalia katika kina cha historia. . Miongoni mwa mifano hii angavu:
Ilhan Omar
Jina lake halisi ni “Ilham Omar,” alizaliwa siku ya 4 ya mwezi wa Oktoba mwaka 1981. Yeye ni mwanasiasa wa Marekani mwenye asili ya Kisomali, alianza kupata umaarufu nchini Marekani tangu mwaka 2016 alipochaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha Kidemokrasia, jambo ambali lilimfanyia kuwa mwakilishi wa kwanza wa Kiislamu aliyejifunika kwa hijabu kushinda uchama wa Baraza la Wawakilishi la Marekani la Jimbo la “Minnesota” katika jiji la “Sao Paulo”; bali, anazingatiwa kuwa ni mmoja wa wanawake wa kwanza wa Kiislamu waliochaguliwa kwenye “Congress”, mbali na kuwa ni mwanamke wa kwanza ambaye si mzungu kuwakilisha jimbo la “Minnesota” katika Baraza la Wawakilishi. Yeye ni mkurugenzi wa Mtandao wa Wanawake wa Sera na Mipango ya Wanawake.
Ni vyema kutambua kwamba “Ilhan Omar” alikuwa ameishi mwanzo wa maisha yake katika kituo moja cha ukimbizi pamoja na familia yake nchini Kenya kabla ya kuelekea Marekani na kuifanya makazi huko mwaka wa 1995 AD, na alianza kuvutiwa na siasa katika jimbo la “Minnesota” alipokuwa na umri wa miaka 14.
Hivyo basi, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu ilisifu hatua hii ambayo inathibitisha kiwango cha maendeleo katika kiwango cha imani ya jumuiya za Magharibi kwa ujumla na hasa jamii za Marekani kwa Waislamu, kwa kuwapa fursa ya kushika nyadhifa za kutunga sheria na uongozi, na kutambua wajibu wao katika kuhudumia jamii wanaoishi humo ndani, na Kukanusha taswira mbaya iliyotolewa na makundi ya kigaidi yenye uhusiano wa uongo na Uislamu.