Usamehevu unamaanisha kusameheana, ulaini na wepesi pamoja na kufanya mema na kuzuia mabaya katika mwenendo na miamala licha ya mahusiano yetu na wengine. Kwa hakika jamii ya kisasa inahitaji sana tabia ya kusameheana kwa kuwa ni msingi wa rehma, amani na utulivu.
Usamehevu wa Uislamu na wanadamu wote, bali na viumbe vyote ni dhahiri katika sheria na hukumu zote za dini hiyo, ambapo uhuru wa kuchagua imani na dini ni sifa mojawapo sifa za dini hiyo tukufu, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): {Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu} 2:256.
Sheria ya kiislamu imekataza kikali kuwadhulumu watu wanaoishi nchi za kiislamu ambao si waislamu, kwani kutofautiana kiitikadi si sababu ya kupigana wala kugombana, bali ni hekima ya Mwenyezi Mungu ambaye Aliwajaalia watu wawe katika makundi na mataifa mbalimbali kwa ajili ya kukamilishana na kusaidiana si kugombana wala kuuana.
Kwa hiyo, waisalmu wanatakiwa kuitetea tabia ya kusameheana na kueneza utamaduni wa kupendana na kuishi pamoja kwa amani na utulivu wakiwa wanawajibika kwa sifa na maadili ya dini hiyo kama vile, upole, ulaini, rhema na undugu. Mtume (S.A.W.) amesema: “Yeyote ambaye ni mpole na mwepesi Mwenyezi Mungu Atamkinga kutokana na adhabu ya moto Akhera”.
Kwa kweli, Uislamu ndiyo dini ya usamehevu, upendo na tabia njema. Usamehevu ni mojawapo tabia takatifu zilizosisitizwa na Uislamu ambao ni umbile lililopitishwa na Mwenyezi Mungu kuanzia mwanzo wa uumbaji mpaka siku ya mwisho. Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu na ardhi, akaumba viumbe vya kila sura na aina, akawatukuza wanadamu na kuwatumia Manabii na Mitume kuwaongoza kwenye njia yake iliyonyooka. Ujumbe wa mbinu kwa Manabii na Mitume wote ulikuwa unajulikana kwa jina la "Hanifiyya Samhaa" jambo linalothibitisha kuwa usamehevu ni msingi muhimu wa jumbe za Mitume wote (A.S.), kwa hiyo, usamehevu, husiano nzuri na upendo huwa sifa kuu za wito wa Manabii na Mitume wote.
Mtume wetu (S.A.W.) ambaye ni Mtume wa mwisho alikuja kukamilisha na kufikisha ujumbe huo huo, bali zaidi ya hayo, kusisitiza kuwa sifa hizo na misingi hiyo hazihusishwi na waislamu tu bali ni misingi ya miamala na watu wote waislamu na wasio waislamu, kwa ajili ya kutimiza maadili ya kibinadamu na kukuza ushirikiano wa kistaarabu. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amebainisha kwamba wasilamu wanatakiwa kutendeana na watu wote kwa mujibu wa misingi hiyo ya msamaha na uadilifu Aliposema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [Al-Mumtahinah: 8].
Kwa kuangalia kwa makini aya hii, tunafahamu kuwa Mwenyezi Mungu Amewaamrisha waislamu kufanya wema na uadilifu na watu wote bila ya kujali dini yao, uraia wao wala kabila lao sharti kutowaudhu waislamu au kuwafanyia khiyana, jambo ambalo linatubainishia msamaha wa dini hii adhimu.
Aidha, Mtume (S.A.W.) amesawiri tabia hii nzuri ya usamehevu kivitendo katika vipindi vyote vya Da'awa na katika hali zote. Pia, Mtume amehimiza sana kueneza tabia hii ya usamehevu baina ya watu wote; waislamu na wasio waislamu, wenyeji wa jamii moja wenyewe kwa wenyewe na wenyewe kwa mataifa wengine, akizingatia usamehevu ni mojawapo maadili mema. Katika maisha yake, Mtume (S.A.W.) alikuwa mwenye msamaha kwa watu wote hata maadui wake waliomuudhi, mpaka akawapa mateka wao msamaha akawaamuru maswahaba wake wawe pole na huruma na mateka hao. Fauka ya hayo, Mtume wakati wa kurudi kutoka At-Taif akiwa na majeraha mabaya na mateso mengi kutokana na aliyoyafanyiwa na watu wa mji huu, akajiwa na Malkia wa Majabali na kusema: "Ewe Mohammed! Hakika Mwenyezi Mungu Amejua waliyoyafanya watu hawa nawe na mimi ni Malkia wa Majabali Amenituma kukuuliza unataka niwafanyie nini, ungekubali niwaangamize kwa kuporomosha milima hiyo miwili wakafa wote ningefanya hivyo. Lakini Mtume (S.A.W.) akakataa kuwaangamiza akisema: Hapana kwani nataraji waongoke au wazae wanaoamini dini hiyo na kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake" imesimuliwa na Muslim.
Kwa hiyo tunaona kwamba Malkia wa Majabali alikuwa anasubiri agizo la Mtume (S.A.W.) kuwaangamiza wale makafiri, lakini rehma yake na msamaha wake ulimfanya akataa kuwafanyia madhara wala adhabu.
Hali hikutofautiana sana aliposhinda washirikina wa Makkah akawa na fursa nzuri ya kulipiza na kuwaadhibu kutokana na uadui wao na mateso waliyosababisha kwa waislamu, ambapo wamewafanyia mabaya na maangamizi makubwa, na kuwalazimisha kutoka na kuacha mali na makazi yao, ingawa haya yote Mtume alipoingia Makkaha akishinda washirikina katika mwaka wa Al-Fat-h, aliwahotubia maqureish waliokusanya wakihofia hatima yao ambayo Mtume ataipitisha akasema Mtume: "Enyi Watu wa Qureish! Je mnadhani kazi gani nitafanya kwenu?! Wakajibu: Labda heri kwani wewe ni mtu mwenye rehma na ukarimu kama ulivyolelewa. Akawaachilia huru na kusema: Mpo huru" Imesimuliwa na Al-Twabariy.
Hivyo, inaonekana wazi namna msamaha na rehma ni sifa za msingi za dini hii na Mtume (S.A.W.), na kwamba dini hiyo adhimu ndiyo dini ya uadilifu, usamehevu na kuhurumiana baina ya wanadamu wote, inayohimiza wafuasi wake wafanye wema na watu wote bila ya kujali dini zao wala uraia wao wala makabila yao. Dini inayohifadhi heshima ya mwanadamu na kuzingatia uhuru wa imani.
Qurani Takatifu kupitia aya kadha wa kadha imesisitiza kuwa waislamu wanatakiwa kuwa na mahusiano mazuri na watu wa dini na itikadi mbalimbali kwani kuna mambo ya pamoja yanayostahiki kuchungwa na wote waislamu na wasio waislamu kwa msingi wa kushirikiana na kukamilishana kwa ajili ya manufaa ya ulimwengu kote. Kwa kweli Uislamu ulikuja ili kuimarisha mahusiano baina ya watu siyo kwa kuyakata yale mahusiano na kupigana nayo.
Jambo la kusisitiza hilo ni alilolifanya Mtume (S.A.W.) katika Suluhu ya Al-Hudaybiya ambapo alifunga mkataba wa amani wa kwanza kabisa baina ya waislamu na washirikina kwa msingi wa kuheshimiana na kuamiliana kwa wema kwa lengo la kuisha pamoja kwa amani na utulivu na kuendeleza jamii na kuilinda nchi. Ingawa masharti ya mkataba huo yalionekana yanawadhulumu waislamu na kupendeleza washirikina lakini Mwenyezi Mungu Aliuita ushindi kama ilivyokuja katika kauli yake (S.W.): { Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri * Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, naakuongoe katika Njia Iliyo Nyooka * Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu} [48/1-3].
Hali hii inathibitisha kuwa Uislamu ndio dini ya amani na utulivu siyo dini ya ugaidi na vurugu, tena baada ya suluhu hilo ilitokea vita vya Khaybar baina ya waislamu na mayahudi na Mtume ameweka mkataba mwingine na mayahudi kwa ajili ya kuzilinda nafsi na damu za pande mbili, pia kuanzia mwaka wa saba baada ya hijra ya Mtume misafara ya mabalozi wa waislamu waliokuwa wanatumwa na Mtume huku na huku ili kueneza ujumbe wa amani na kuanzisha mahusiano na mataifa mbalimbali kwa lengo la kuthibitisha kuwa dini hiyo ni dini ya amani na upendo.
Mtume (S.A.W.) alikubali zawadi alizozipata kutoka wafalme wa umma nyingine kama vile; Al-Najashiy mfalme wa Uhabashi akawafanyia wajumbe wa mfalme yule ukarimu mkubwa akisema: "Hakika watu hawa waliwafanyia maswahaba zetu ukarimu mkubwa". Inatajwa pia kwamba Uislamu unawahimiza waumini wahifadhi mahusiano yao wenyewe kwa wenyewe na kuwafananisha kwa mwili mmoja kama ilivyokuja katika hadithi ya Mtume: "Kwa kweli mfano wa waumini katika upendo na huruma wao wenyewe kwa wenyewe ni kama mwili mmoja kama kiungo kimoja kinauma basi mwili mzima huumwa na kutaabika kwa maumivu ya kiungo hicho".