Kuwauwa raia wasio na hatia ni msingi katika itikadi ya kizayuni

Imeanaliwa na Bw. Said El-Sayed Moshtohry

  • | Thursday, 26 September, 2024
Kuwauwa raia wasio na hatia ni msingi katika itikadi ya kizayuni

     Kuwaua raia wasio na hatia katika itikadi ya kizayuni kunategemea msingi wa kuwadharau wengine, na kuwanyang'anya haki zao bila ya kujali, wakijizingatia kuwa wamechaguliwa na Allah na waliumbwa ili kuihukumu dunia, kwa hivyo kila anayepigana nao hastahiki ila kuuliwa na kuhamishwa kutoka makazi yao.

Na tukitazama aya za Taurati zinazozingatiwa kuwa marejeo ya kihistoria ya wazayuni, tutazikuta kwamba zinaeleza wazi mkakati wa kivita unaopaswa kufuatwa wakati wa kuivamia nchi fulani, kama vile aya isimayo: “Unapokaribia kutoka mji ili kuupiga vita, waite wananchi wake kwa kufanya mkataba wa amani, wakikubali na kufungua mji kwenu, basi wananchi waliomo ndani yake ni watumwa wenu, na wakikataa na kupigana nanyi basi wawazingira na uweni wanaume kwa upanga, ama wanawake, watoto na wanyama ni zawadi kwenu kutoka kwa mungu”.

Na mfano wa hivyo ni kwamba wazayuni baada ya kuingia mji wa Ariha katika mwaka wa 1967 “walifanya mauaji ya kimbari dhidi ya wanaume, wanawake, watoto, hata ng'ombe, mbuzi na punda kwa upanga na kuuchoma moto mji kamili kwa walio ndani yake”.

Pia tukiangalia kilichotokea kwa sababu ya Al-Nakba iliyoanzishwa juu ya itikadi safi ya kizayuni, tutagundua kwamba ilikusudia kuharibu mahali, kama ilivyofanywa katika vijiji 418 vilivyoharibiwa kikamilifu, nayo ni idadi kubwa inayozingatiwa kuwa nusu ya idadi ya vijiji vyote vya kipalestina wakati huo, na kwamba vijiji 292 viliharibiwa vibaya, wakati vijiji vingine 90 viliharibiwa isipokuwa theluthi ya nyumba zake zilibaki salama, huku vijiji vinane aghalabu ya nyumba zake zilibaki salama bila ya kuharibiwa, na vijiji saba walividhibiti kikamilifu na wameishi ndani yake.

Mawazo hayo yote yanabeba kila aina ya fahari inayopelekea vurugu kwa wanaowaita “wakaliaji wa Kiarabu” nayo ni mawazo yaliyokutwa baada ya kuwabagua mayahudi huko Ulaya kupitia historia, jambo lililowapelekea kuibua kauli mbio ya kwamba wao wanadhulumiwa, kauli hiyo waliisema ili kuomba huruma ya nchi za Magharibi, walifanya hivyo pamoja na Uingereza ili kuanzisha dola yao katika Palestina na walifanya hivyo na Marekani sasa hivi katika uadui wao dhidi ya Gaza kupitia ushawishi wa kizayuni uliopo kwenye mishipa ya dola na jamii ya kimarekani, jambo lililopelekea Marekani kutetea jinai za kizayuni, bila kujali idadi ya wapalestina wanaouwawa au kuadhibiwa kutoka raia wasio na hatia, nayo ndiyo mafundisho ya itikadi ya kizayuni katika mitaala ya kielimu na sheria zao za kibaguzi.

Mwishoni, lazima tutambue kwamba suala la kipalestina halitatatuliwa ila kwa nguvu, na kama Alivyosema Sheikh wa Al-Azhar katika mkutano wa kuunusuru Al-Quds katika mwaka wa 2018 “ikiwa, katika wakati wetu huu, tumelazimishwa kuishi baina yetu adui mgeni asiyeelewi ila lugha ya nguvu tu, basi hatuna hoja mbele ya ALLAH na historia tukibaki na dhaifu, ilhali tuna - tukitaka – elementi zote za nguvu na nyenzo zake zote.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.