Dkt. Mohamed Gad, Balozi wa Misri nchini Ethiopia na Mwakilishi wake wa kudumu katika Umoja wa Afrika, amesema kuwa Misri itachukua uenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la kiafrika kuanzia kesho, tarehe 1 Oktoba 2024.
Mwakilishi huyo wa kudumu alibainisha kuwa uenyekiti wa Misri unaotarajiwa utalenga kuimarisha jukumu la baraza hilo kama chombo kinachohusika na kulinda amani, usalama, na utulivu, pamoja na kutatua changamoto za kiusalama na kimaendeleo zinazokabili bara la Afrika, uenyekiti huo wa Misri unakuja katika muktadha tata wa kimataifa na kikanda ambapo changamoto za kiusalama zinaongezeka, jambo linalohitaji juhudi za pamoja na kushauriana kwa wazi kuhusu njia za kukabiliana nazo kwa lengo la kuimarisha utulivu na usalama barani Afrika na kuhakikisha malengo ya Ajenda ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika 2063.
Balozi Mohamed Gad ameongeza kuwa, wakati wa uenyekiti wa Misri kwa baraza hilo, shughuli mbalimbali zitapangwa, ikiwemo ziara ya baraza hilo kwa Cairo ili kufanyika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhamiaji kuhusu masuala ya amani na usalama barani Afrika, na mashauriano pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, na kufanyika kikao cha baraza hicho katika ngazi ya wawakilishi wa kudumu kuhusu uhusiano kati ya amani, usalama, na maendeleo, kwa kuzingatia uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Misri kwa suala la ujenzi mpya na maendeleo baada ya migogoro, mbali na kuzuru kituo cha mafunzo juu ya operesheni za kulinda amani cha Misri cha Wizara ya Mambo ya Ndani.
Balozi Mohamed Gad pia alieleza kuwa Baraza la Amani na Usalama chini ya uenyekiti wa Misri litafanya ziara ya kwanza kwa mji wa Port Sudan inayozingatiwa ya kwanza tangu kuzuka kwa mgogoro wa Sudan tarehe 15 Aprili 2023, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Misri za kuimarisha mshikamano na wananchi wa Sudan, kunga mkono taasisi za serikali ya kisudan, na kuwezesha baraza na Umoja wa Afrika kutambua hali ya kweli na kuchukua jukumu lake katika kuimarisha juhudi za kufikisha suluhisho ya amani kwa mgogoro.
Balozi Dkt. Mohamed Gad alieleza kuwa programu ya uenyekiti wa Misri itajumuisha kufanyila mashauriano kila mwaka kati ya Baraza la Amani na Usalama la Afrika na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na Kamati ya Ujenzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa. Pia, kufanyika kikao cha pamoja kati ya Baraza la Amani na Usalama na Kamati ndogo ya Wawakilishi wa kudumu kuhusu usimamizi wa jumla, uratibu wa bajeti, na masuala ya fedha na utawala –inayoongozwa na Misri – kwa lengo la kuchunguza ufadhili wa operesheni za amani barani Afrika, na kikao cha kuhusu maendeleo ya hali nchini Somalia baada ya kuondoka kwa Ujumbe wa Mpito wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kuunga mkono taasisi za serikali ya Somalia katika kupambana na ugaidi na kudumisha amani. Mwakilishi wa kudumu pia alibainisha kufanyika vikao vingine kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi barani Afrika, hali ya kibinadamu, masuala ya wanawake, amani na usalama, na masuala ya tabianchi, amani na usalama.
Inatajwa kukumbuka kwamba Misri ilichaguliwa kuwa na kiti cha miaka miwili katika Baraza la Amani na Usalama kwa kauli moja wakati wa mkutano wa Baraza la Mtendaji la Umoja wa Afrika mnamo Februari 2024, kama mwakilishi wa kanda ya Afrika kaskazini, jambo linaloonyesha heshima na imani ya nchi za kanda ya Afrika kaskazini pamoja na nchi zote za bara hilo kwa juhudi za Misri na kujitolea kwake kwa kuimarisha amani, usalama, na utulivu barani Afrika.
Imefasiriwa na Bw., Said El-Sayed Moshtohry