Baada ya mwaka mzima...takwimu za wahanga wa mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza

  • | Tuesday, 8 October, 2024
Baada ya mwaka mzima...takwimu za wahanga wa mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza

 

Tangu 7 Oktoba, 2023, utawala wa Kizayuni umeanzisha vita kamili vya mauaji ya kimbari ambavyo vimeacha idadi za kutisha zinazoonyesha ukubwa wa maafa ya kibinadamu yanayowakumba Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, kutokana na kutumia wavamizi silaha zilizopigwa marufuku kimataifa. na kulenga kwake kimakusudi maeneo yanayojazwa  na watu, vituo vya ukazi, mahema ya wakimbizi, Shule, hospitali, na nyumba za ibada za Kiislamu na Kikristo, kwa aina hatari zaidi za vilipuzi. Labda nambari zifuatazo zinaonyesha ukubwa wa maafa ambayo watu wetu huko Gaza waliishi kwa mwaka mzima chini ya ukimya kamili wa ulimwengu:

  • Kufanya kwa uvamizi zaidi ya mauaji 3,654 dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza.
  • Idadi ya vifo imefikia takriban mashahidi 41,870 (hadi sasa) kwa mujibu wa sajili za Wizara ya Afya ya Palestina, ambao wengi wao ni wanawake na watoto.
  • kujiandikisha watu 10,000 waliopotea wakiwa bado chini ya vifusi na barabarani. Ambapo wavamizi walizuia vikosi vya uokoaji na vya ulinzi wa raia kufikia waliojeruhiwa na waliopotea.
  • Watoto 16,927 waliuawa kishahidi.
  • Watoto wachanga 171 waliuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari.
  • Kuuawa shahidi kwa familia 902 za Wapalestina, ambao wanachama wao wote waliuawa na uvamizi huo, hivyo wakaondolewa kwenye sajili ya raia.
  • Watoto 63 waliuawa kishahidi kutokana na njaa iliyopiga - na bado inaendelea - Gaza mzima, na kaskazini hasa.
  • Wanawake 11,487 waliuawa kishahidi.
  • Wafanyikazi wa matibabu 986 waliuawa kishahidi.
  • Wanachama 85 wa ulinzi wa raia waliuawa kishahidi.
  • Waandishi wa habari 175 waliuawa kishahidi.
  • Watu 520 waliuawa kishahidi wakati wa kuwatolewa kwenye makaburi saba ya pamoja ndani ya hospitali.
  • Uvamizi ulilenga vituo 187 vya makazi; ambayo ina maana kwamba hakuna mahali salama katika Gaza.
  • Kuwepo kwa watoto 25,973 wa Kipalestina huko Gaza ambao wanaishi bila ya mzazi mmoja au wote wawili.
  • Majeruhi 97,166 walifika katika hospitali za Wizara ya Afya.
  • Watoto 3,500 walikufa kutokana na utapiamlo.
  • Kuwepo kwa majeruhi 12,000 wanaohitaji kusafiri kwa matibabu nje ya Ukanda wa Gaza.
  • Kuwepo kwa wagonjwa 350,000 wenye magonjwa sugu walio hatarini kutokana na kuzuia kuingiza kwa dawa
  • Raia 5,000 wa Ukanda wa Gaza walikamatwa ndani ya mwaka mmoja wa vita vya mauaji ya kimbari.
  • Idadi ya watu waliokimbia makazi yao ndani ya Ukanda wa Gaza ilifikia milioni mbili kwa mwaka, na uhamisho bado unaendelea.
  • Kuwanyima elimu wanafunzi 785,000 wa Tilal.
  • Uvamizi huo ulidondosha tani 85,000 za vilipuzi kwenye Ukanda wa Gaza.
  • Uharibifu wa zaidi ya 85% ya nyumba, majengo na miundombinu.
  • Nyumba 150,000 ziliharibiwakikamili.
  • Hospitali 34 ziliondolewa huduma.
  • Vituo 80 vya afya viliondolewa huduma.
  • Uvamizi huo uliharibu kabisa misikiti 814 kati ya misikiti 1,245 ya Ukanda wa Gaza.
  • Uharibifu wa makanisa matatu.
  • Uharibifu wa maeneo 206 ya kiakiolojia na urithi.
  • Hasara za awali za vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza zilifikia zaidi ya dola bilioni 35.

Licha ya uchungu unaoziumiza nyoyo, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kinathibitisha kwamba damu hii safi iliyotakasika haikuwa bure, na kwamba njia ya uhuru na kurejesha haki zilizoibiwa lazima iwe na bei, na kwamba Wapalestina hatashindwe kwa sababu wana haki wazi na ya kweli, hivyo kupinga uvamizi ni haki ya Kisheria, ya kibinadamu, na ya kiustaarabu, na ni wajibu wa kidini unaotambulika, bali ustahmilivu wao kwa muda wa mwaka mzima mbele ya silaha hiyo ya kijeshi ya Kizayuni inayoungwa mkono na ulimwengu wa kinafiki wa Magharibi unazingatiwa kuwa ni muujiza kwa viwango vyote.

Vile vile, Kituo cha Al-Azhar kinaomba ulimwengu mzima kufanya marekebisho kwa kile kilichopoteza, kuokoa ubinadamu huko Gaza na Lebanon, kutetea thamani ya mwanadamu na haki yake ya kuishi, na kukomesha wazimu huu wa Kizayuni ambayo imekaribia kuburuta eneo zima katika vita kubwa vya kikanda, vinavyoharibu yote yaliyosalia katika njia yake, na ulimwengu kote unalipa gharama yake.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.