Kwa vijana wa Ummah

Khiyana na kuvunja ahadi katika Uislamu

  • 8 November 2017

1- Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewaamrisha waja wake waumini watekeleze ahadi zote na kulazimika kwa majukumu yao yote, zikiwa ahadi hizo na Mwenyezi Mungu au na watu, Mwenyezi Mungu Amesema: "Enyi mlio amini! Timizeni ahadi".
2- Hakika kuheshimu ahadi na mikataba ni wajibu wa kiislamu kwa sababu athari zake nzuri na umuhimu mkubwa katika kuihifadhia jamii na pia kuyatatua matatizo na migogoro mbali mbali.
3- Kwa hakika kuvunja ahadi hakukubalika kuwa miongoni mwa sifa za waumini, bali hiyo ni miongoni mwa sifa za wapotofu na wanafiki, Mwenyezi Mungu Amesema: "Wala hatukuwaona wengi wao kuwa wanatimiza ahadi; bali kwa hakika tuliwakuta wengi wao ni wapotofu".   
4- Hakika kuvunja ahadi husababisha matokeo mabaya kwa watu na jamii, ambapo husaidia kuzuka hitilafu, ugomvi, aidha kunatia wasiwasi kati ya watu wa jamii.
5- Mwenyezi Mungu Amewakataza Waumini kuvunja ahadi, Amewalazimisha watekeleze ahadi, basi Mwenyezi Mungu Amesema: "Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa".
6- Mtume (S.A.W) Amewaonya waumini kuvunja ahadi, Akisema: "Mambo (sifa) manne mwenye kuwa nayo atakuwa ni mnafiki safi, na atakayekuwa ana mojawapo katika hayo, atakuwa ana jambo (sifa) moja katika unafiki mpaka aliache; anapoaminiwa hukhini, akizungumza husema uwongo, akiahidi huvunja na hufanya ubaya".
7- Hakika minongoni mwa adhabu za haraka inayoistahiki jamii kutokana na kuenea sifa ya kuvunja ahadi ni wengi wa kuua na hii imedhihiri kwa wazi katitka kauli yake Mtume (S.A.W): "Hakika watu wakivunja ahadi basi mauaji yatatenea sana kati yao".

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:

Please login or register to post comments.