Kwa vijana wa Ummah

Kufanya upya katika Dini ya Uislamu

  • 20 November 2017

-    Sio maana ya kufanya upya au luleta mageuzi mapya katika dini kuziporomosha nguzo za dini hiyo au kupuuza misingi yake, bali inamanisha kujaribu kuboresha ufahamu wa matini za dini na kutekeleza mafunzo yake kwa mujibu wa mabadiliko ya zama tuliyo nayo.

-    Uislamu ni dini nyepesi kwani hukubali kuambatana na kila mahali na wakati, sio dini ya wakati maalumu au mahali hasa.

-    Mtume (S.A.W.) ni wa kwanza kufanya upya katika dini ya kiislamu alipogundua mifumo mipya katika dola ya kiislamu akizingatia misingi ya dini, zaidi ya haya aliwaelekeza maswahaba wake (R.A.) na waislamu wote kutokaa kimya, bali lazima wafungamane na mahali na wakati walioishi humo ndani, wakagundua njia mpya za ulinganiaji na kujenga dola la kiislamu bila ya kupoteza nguzo za dini na misingi yake.

-    Anayefanya mageuzi mapya lazima atambue vizur umuhimu wa utamaduni wa kufikiri katika pande zote za maisha, na kutoka katika mazingira yaliyoshaandaliwa na njia zilizoganda na kuelekea katika muono wenye sifa ya kufikiri na kuitumia akili ipasavyo.

-    Ni lazima kwa wanavyuoni na wahenga wanaoeneza maana sahihi ya kuleta mageuzi mapya iliyotafitwa vyema na iliyo ndani ya wigo unaolinda misingi ya kisheria isiyotetereka.

-    Kwa kweli watu wenye kufuata mfumo wa mgando, ukufurishaji, uhainishajia na kuwatuhumu watu pasipo na dalili thabiti, basi hao ndio watu hawana elimu wala fiqhi; kwani wameghafilika kuwa Uislamu ni dini yenye urahisi na kwamba dini hii ni dini mwafaka wa zamani zote na mahali kote.
 
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:

Please login or register to post comments.