Kwa vijana wa Ummah

Maadili ya kibinadamu

  • 27 November 2017
Maadili ya kibinadamu

     1- Sheria zote za mbinguni zimekusanya kiasi kikubwa cha maadili na misingi ya kibinadamu. Na muhimu kati ya misingi hiyo ni; kuhifadhi roho ya kibinadamu, mali yake, heshima yake na uhuru wake.
2- Mtume wetu S.A.W. alitilia mkazo kuihifadhi roho ya binadamu, na lilipopitia na jeneza la myahudi, Mtume akasimama kwa ajili ya jeneza hilo. Na alipoambiwa kuwa hilo ni jeneza la myahudi, Mtume S.A.W. akajibu kwa kusema: "kwani huyo si binadamu?!"
3- Huenda sheria zikahitilafiana katika ibada na njia za kuzitekeleza ibada hizo kutokana na hali ya zama na mahala, lakini tabia na maadili ya kibinadamu ambayo ni msingi wa kuishi pamoja hayahitilafiani katika sheria yoyote miongoni mwa sheria Alizoziteremsha Mwenyezi Mungu.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:

Please login or register to post comments.