Kwa vijana wa Ummah

Uislamu huharamisha kushambulia Nyumba za Ibada

  • 1 December 2017
Uislamu huharamisha kushambulia Nyumba za Ibada

     1.    Uislamu umeita kuhifadhi nyumba za ibada na umezipa utakatifu wa hali ya juu, kwani hizo ndizo Nyumba za Mwenyezi Mungu ardhini, na kuzishambulia ni kitendo kibaya kinachokataliwa katika Uislamu hata zikiwa Nyumba hizo za wasio waislamu, kwa hiyo yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama vile ISIS, Boko Haram na mengineyo kati ya kuvunja huruma na utakaso za Nyumba hizo huwa mbali sana na mafundisho ya kiislamu.   
2.    Kwa Hakika kuzishambulia Nyumba za ibada sawa kwa kuziharibu au kuwazuia watu kufanya ibada zao humo ndani Nyumba hizo kwa raha ni kitendo ambacho hakihusiani na Maadili ya kibinadamu licha ya kupingana na mafundisho ya kiislamu.
3.    Kwa kweli Uislamu unawaita wafuasi wake kuzitakasa Nyumba za ibada hata zikiwa kwa wasio Waislamu, ukawahimiza kuzihifadhi Nyumba hizo pamoja na waja wa Mwenyezi Mungu waliyomo ndani yake wanaozitumia kwa ajili ya kupata utulivu wa kiroho na kumwabudu Mola wao.
 
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikira Kali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:

Please login or register to post comments.