Kwa vijana wa Ummah

Ukweli wa Uislamu

  • 16 December 2017
Ukweli wa Uislamu

     1- Kwa hakika hali ya makundi yanayojinasibisha na Uislamu kwa njia ya dhuluma, inaonyesha uhalisi mchungu, ambapo tunauona mauaji na umwagaji damu ambao unafanywa eti! kwa jina la Uislamu na chini ya bendera ya Quraani, ilhali Uislamu na Quraani vyote havina uhusiano wo wote na jinai hizi zote.
2- Tunakuta pia kuwa kuna ukiukaji wa wazi katika Nyanja za maadili mema kwa ujumla unaofanywa na baadhi ya wale wanaojinasibisha na Uislamu. Wakati ambapo Uislamu unatuamrisha kusema ukweli na kutekeleza ahadi. Kwa bahati mbaya, tunakuta katika baadhi ya waislamu wanakwenda kinyume kabisa na mafunzo ya dini. Jambo ambalo lintufanya tuongeza juhudi zaidi kwa ajili ya kurekebisha na kusahihisha makosa haya.
3- Pia, tunawaona kuwa baadhi ya nchi za kiislamu zimechelewa na kuwa nyuma mno kwa kulinganisha na mataifa yaliyoendelea kwa kazi na uzalishaji, kinyume na dini yetu takatifu inavyotuamrisha! Na hali iliyo hapo zamani katika vipindi vya historia ya kushangaza ya kiislamu.  


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:

Please login or register to post comments.