- Uislamu umeharamisha kufanya adha kwa maneno au vitendo kwa kila mwenye kuahidiwa au mwenye kuaminiwa aliyeingia ardhi za Uislamu, ukakataza sana kuwaudhi watu pasipo na sababu sahihi ya kisheria na pasipo na kurejelea mtawala anaye haki ya kuamua adhabu juu ya yeyote.
- Uislamu umeamrishia Ihsan kwa wasio waislamu ambao hawakufanya adha dhidi ya waislamu wala hawapigani nao kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: (Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu), bali zaidi ya hapo, umeamrisha kuwasiliana na kuwalipa mali kwao.
- Uislamu umeharamisha kuudhi wasio waislamu hata wakati wa kufanya vita madamu hawakushambulia waislamu wala hawakufanya uadui dhidi yao, ama wakiwashambulia waislamu au kukalia ardhi zao au kuwafanyia uadui basi waislamu wameruhusiwa kupigana nao kwa mujibu wao vidhibiti maalum vya vita katika Uislamu ambavyo vinachangia sana huruma na ubinadamu hata pamoja na maadui, mfano wa kutosha kuwa Uislamu umeharamisha kuua mtu asiyeshiriki katika vita kama vile; wazee, wanawake, watoto, na wafanyao ibada katika nyumba zao za kumwabudu Mwenyezi Mungu (kutokana na itikadi zao) wala kuziharibu nchi, wala kuikata miti, wala kuchafusha maji n.k.
- Uislamu umewajibikia waislamu wafanye uadilifu na wasio waislamu, Mwenyezi Mungu amesema: (Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda).
Kituo cha Al-azhar cha Kupambana na Fikira Kali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika