Mkiuliza historia juu ya msikiti wa Al-Quds na umuhimu wake, bila shaka itajibu kuwa:
Katika historia ya Uislamu tunasoma kuwa Mtume (S.A.W.) katika tukio la Miiraj alisali katika maeneo mbalimbali kama vile; Mlima wa Sinai (Al-Toor) mahali ambako Mwenyezi Mungu alikomzungumzia Nabii wake Mussa (A.S) na vile vile Baitu Lahm mahali alikozaliwa Nabii Issa (A.S). Baada ya hapo Mtume (S.A.W.) aliingia Msikiti wa Al-Aqsa na baada ya kusali katika Mihrabu ya Mitume watukufu, alipaa na akaelekea mbinguni. Kwa hiyo Msikiti wa Al-Aqsa ukawa msikiti mwenye umuhimu mkubwa kwa waislamu wote.