Kwa vijana wa Ummah

Uliza Historia kuhusu utambulisho wa Al-Quds Enyi, wasomaji waheshemiwa!!

2

  • 25 December 2017
Uliza Historia kuhusu utambulisho wa Al-Quds Enyi, wasomaji waheshemiwa!!

     Mkiuliza historia juu ya mji wa Al-Quds (Jerusalem) na uhusiano wake na Uarabu na Uislamu, bila shaka itajibu kuwa:
•Katika riwaya za Kiislamu tunasoma kuwa, Nabii Adam (A.S.) baada ya kujenga Msikiti wa Al-Haram huko Makka, aliamrishwa na Mwenyezi Mungu kuweka misingi ya Msikiti wa Al-Aqsa.
•Mji wa Baitul Maqdis au Al-Quds, ni mji mmojawapo miji muhimu ya kihistoria duniani, kwani huzingatiwa utambulisho wa kidini sawa kwa waislamu au wakristo. Kwa mujibu wa baadhi ya maandishi ya kihistoria, mji huu ulianzishwa tangu zaidi ya miaka elfu nne iliyopita.
•Mitume na Manabii wengi wa Mwenyezi Mungu walizaliwa au kuishi katika mji huo mtukufu. Ni kwa sababu hii ndio maana mji huu ukazingatiwa kituo cha kuwavutia wafuasi wa dini tatu; Uyahudi, Ukristo na Uislamu.
•Kwa hiyo tunasisitiza kwamba majaribio yanayojiri siku hizi ya kulengea kubadilisha utambulisho wa mji huu hayatafanikiwa kabisa wala wanaotaka kuupora kutoka wamiliki wake wa kikweli hawatapata nafasi ya kufanya hayo.

 

Print
Tags:

Please login or register to post comments.