Enyi, wasomaji waheshemiwa!! Mkiuliza historia juu ya mji wa Al-Quds (Jerusalem) bila shaka itajibu kuwa:
Msikiti wa Al-Aqsa ndio Qibla ya kwanza ya Waislamu. Kwa miaka kadhaa, Waislamu walisali wakielekea Msikiti wa Al-Aqsa. Katika mwaka wa pili wa Hijria, Mwenyezi Mungu Mtukufu Alitoa amri kwa Mtume wake Mohammed (S.A.W.) na Waislamu kubadilisha Qibla yao kutoka Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds na kuelekea Msikiti wa Al-Haram katika mji wa Makkah. Aya za 142 hadi 150 katika Suratul Baqara zimezungumzia tukio hili. Katika sehemu moja ya aya ya 150 Mwenyezi Mungu Anamwambia Mtume Mohammed (S.A.W.) na Waumini kwa kusema: "Na popote wendako elekeza uso wenu kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo..."