Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

WARAKA WA AZHAR
Anonym
/ Categories: Main_Category

WARAKA WA AZHAR

 

WARAKA WA AZHAR

 

  1. Waraka wa mustakabali wa misri.
  2. Tamko la kusaidia matakwa ya raia wa Kiarabu.
  3. Tamko la mfumo wa misingi ya uhuru.
  4. Tamko kuhusu ukamilishaji wa malengo ya mapinduzi.
  5. Tamko la Quds Al-Sharif.

 

 

 

Haki ya uchapishaji imehifadhiwa

Chapa ya kwanza

1433. H – 2012. AB

 

 

 

 

 

 

BiSMILLAH RRAHMAN RRAHIM.

MWANZO WA WARAKA

Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, na kumtakia amani Mtume wake: kwa hakika Al-Azhar Al-Sharif ni jukwaa la uongozi wa taifa la Misri kwa muda mrefu wa historia, pia ndio dhamira ya Umma wa Kiislamu, inahisi maumivu ya Umma, inaelezea matarajio yake, inatetea haki zake, kisha Azhar ni ngome ya utamaduni wa Kiarabu na Kiislamu kwa urithi wake wa muda mrefu na miyonzi yake ya misingi ya kati na kati: ndani kikanda na kimataifa.

Na kwa kuanza na mazingatio yote haya, Azhar ilitoa wito wa mazungumzo ya kiistaarabu kati ya Umma wa Kiislamu na mataifa mengine, lengo ni kubadilishana mafanikio, na kufikia masilahi makuu ya ubinadamu, na kwa ajili pia ya kutekeleza haki ya kufahamiana kwa mataifa mbali mbali kama ilivyoelezewa hilo kwenye surat al hujraat ndani ya qurani tukufu (Enyi watu, hakika tumekuumbeni wanaume na wanawake, na tukakufanyeni mataifa na makabila ili mpate kufahamiana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mcha Mungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na mwenye habari).

Isipokuwa Azhar wakati huo huo inapinga kwa kila anaeugusa Umma wa Kiislamu au kugusa sheria zake, inafanya juhudi pia ya kusahihisha vitendo visivyo jenga, kupitia ufuatiliaji wa mazungumzo na pande mbali mbali. Kisha Azhar imeweka makubaliano yote ya mazungumzo yaliyofikiwa huko nyuma kati yake na baadhi ya taasisi mbali mbali sehemu ya kuyapitia na kusahihisha pamoja na kuyajenga tena katika wigo wa vipimo hivi.

Imefanya haraka Azhar ndani ya zama zake hizi mpya kurekebisha mtazamo wake wa mazungumzo na pande zake sharti zake na misingi yake… na kujikita hapo mwanzo na mazungumzo ya Azhar kwa pande zake zote, pande za Kimisri / Kimisri, Kiarabu / Kiarabu, Kiislamu / Kiislamu … baada ya kuwa mazungumzo yakiendeshwa kutokana na hali ya matatizo ya nje, hivi sasa Azhar imekuwa na muswada wake mwenyewe wa mazungumzo ambayo unaegemea kwenye misingi ya qurani na hadithi takatifu, pamoja na muundo wa ustaarabu wa Kiislamu ndani ya kipindi chake cha kukuwa na kuendelea.

Na pindi elimu ilipokuwa ni nguzo ya ujumbe wa Azhar, hivyo Azhar imeanza tokea miaka miwili iliyopita kufanya marekebisho mitaala yake kutokana na hali ya kutokuwa na mpangilio nzuri, ikaanza marekebisho ya mitaala ndani ya Azhar na kuanzisha kitengo maalumu katika hatua ya masomo ya sekondari za Azhari cha masomo ya Kiislamu na Kiarabu, kina mwandaa mwanafunzi ili kuweza soma masomo ya vyuo vikuu vya masomo ya sheria na lugha ya Kiarabu, kwa mitaala mikongwe ya Azhari inayofahamika kusimamia misingi ya kati na kati uadilifu na kimaudhui ambayo imetengeneza wasomi wake na nyota wake maarufu, mfano wa hao ni Shaltout, Al-maraaghy, Diraaz, Abdulrazik, Abdul halim, Al-shaarawy na Mohammad Al-ghazaly – Mwenyezi Mungu awarehemu wote.

Hayo yalikuwa kabla ya mapinduzi ya tarehe ishirini na tano Januari 2011, kisha ikaja hali ya mapinduzi na kuwa ni msaada wa kufanya marekebisho zaidi na maendeleo, maeneo ya kazi yakapanuka na kuwepo duru nyingi za kazi, lakini yote hayo yanalenga katika malengo makuu mawili: kurekebisha nyumba ya Azhar kwa ndani – kupitia marekebisho ya mitaala ya masomo ya chuo kikuu na hatua ya kabla ya chuo, nalo ni lengo la lazima na bora zaidi kwa wana Azhar na Wamisri wengine – kisha kuinua duru ya taifa na Uislamu ambao unasubiriwa na wote kutoka kwenye taasisi yao kongwe, kwa ngazi mbili ya ndani na kimataifa, baada ya nchi kwanza ki uasilia wa mambo.

Makao Makuu ya Azhar yalipata makaribisho makubwa kwa fikra hii toka kwa wadau wengi, Azhar ikaendesha mijadala ambayo ilijaza kumbi na kufurahisha wananchi, Azhar iliwaita wasomi mbali mbali wa Kimisri ambao wanawakilisha makundi mbali mbali ya kitaifa kwa pande za kifikra, ili wakae pamoja na jopo la wanachuoni wa Azhar wale maarufu, kwa pamoja ili wawezi kudurusu hali ya mambo na kufuatilia maendeleo ya mapinduzi na mahitaji yake, na wanakutana kwa misingi yenye kukubalika kisheria na kukubalika mbele ya jopo la wasomi na wana fikra, na pia kuitikia mahitaji ya hali iliyopo nchini, na huwenda ukapatikana mfano wa kuigwa na baadhi ya jamii za Kiislamu sawa na matakwa yao na matatizo yao.

Na ikawa katika matunda ya juhudi hizi za kielimu na kifikra za pamoja, na mazungumzo ya kina yaliyoendelea kwa muda wa miezi kadhaa ni kupatikana waraka huu ambao leo tunautoa kwa msomaji wa Kiarabu:

Maelezo ya Kwanza: waraka wa msingi wa utawala nchini, ambao unajenga mahusiano kati ya kiongozi na anaeongozwa, na kuweka haki na wajibu, na unaweka nidhamu ya demokrasia ya ushiriki wa wananchi katika uongozi, unachora sura ya nchi itayoridhiwa na watu wetu, kuridhiwa na sheria yetu na kukidhi mahitaji ya wakati wetu.

na uliishia mzunguko wa kifikra kuwa, nchi hii ni “Nchi ya kiraia, kidemokrasia, kikatiba, kisasa” na kusudio la kisasa ni kuhifadhi vipindi vya kati ya mihimili mitatu ya kimamlaka: serikali tendaji, bunge na mahakama. Waraka huu ulitolewa mnamo mwezi 17/07/1432.H sawa na tarehe 19/05/2011. AB, Waraka huu ulikubalika na pande mbali mbali za wasomi na wanasiasa, na kuleta matumaini kwa baraza la wazee la kikatiba litakapo undwa kuuweka waraka huu katika katiba ya nchi.

Maelezo ya Pili: ilikuja baada ya hapo na kuonekana ipo haja kwa Azhar kutoa tamko la marejeo litakalo toa mchango katika kulinda misingi ya uhuru ambayo itaandaa masuala ya jamii huru ambapo Wamisri wengi wanapenda kuishi katika mazingira hayo, na yanayotokana na uhuru huu miongoni mwa mambo ya wajibu na yanayozunguka uhuru, katika wigo wa kisheria inayotokana na malengo ya sheria na makusudio yake. Hapo ndipo ulipokuja waraka wa pili baada ya ule wa kwanza uliopita kwa kiasi cha miezi miwili tu, ili kukidhi hayo mahitaji katika mahitaji ya mapinduzi nchini, baada ya kuwepo muitikio usio wa kawaida katika waraka ule wa kwanza.

Waraka huu wa pili ulikuwa umekusanya asili ya kisheria kifalsafa na kikatiba kwa ajili ya uhuru wa imani, uhuru wa utafiti wa kielimu, na uhuru wa ubunifu wa kifasihi na kisanaa, na kila chenye kulinda uhuru wa maoni na kujielezea, hiyo ndio katika misingi mikubwa ya uhuru wenye kubeba pembezoni mwake majukumu mbali mbali.

Kisha hali ilikuwa tete kwa kusambaa “mapinduzi ya Kiarabu” na kuchemsha joto la kisiasa ndani ya nchi za Kiarabu zengine zisizo kuwa nchi za Misri na Tunisia, kama vile nchi za Yemen Libya na Syria, na kuenea kwa joto la kisiasa kwa nchi nyingi za Kiarabu nadhani lililo sahihi pamoja na hali waliyonayo wananchi juu ya ukaidi wa watawala, ikawa ni lazima kwa Azhar kuweka wazi msimamo wake kuhusiana na raia wa kimapinduzi, jopo la wanafikra na wanachuoni wa Azhar walirudi tena katika kutengeneza waraka wa tatu unaofungamana na kuunga mkono matakwa ya wananchi wa Kiarabu, Azhar ikatangaza kuwa kiongozi ambaye anamwaga damu ya wananchi wake uhalali wake wa kuwa kiongozi unaondoka, pindipo tu mapinduzi yaliyopo ni mapinduzi ya kiraia yaliyo salama, yenye kuonesha matarajio ya raia na wala sio tamaa za pande zenye kunyemelea Waarabu na Waislamu, waraka huu ulitolewa mnamo mwezi tatu mfungo tatu mwaka wa 1432.H sawa na tarehe 30/12/2011. AB

Na pindi ilipoibuka mijadala mikali pande mbali mbali za kitaifa za Misri, na kutishia ubaguzi mkali kutokea kati ya pande mbali mbali nchini, na mapinduzi yalikaribia – kutokana na kuingilia kati pande zisizo husika – kuporwa na kuwa mapigano, pindi yalipotokea hayo Azhar ilitoa tamko muhimu sana kuhusu (ukamilishaji wa malengo ya mapinduzi na kurejesha roho yake) ya usalama, alishiriki katika kutoa tamko hilo akiwa pamoja na sheikh wa Azhar ni Papa Chnuda, Papa wa Alexandria aliefariki pamoja na Waziri Mkuu na wawakilishi toka vyama mbali mbali na makundi ya kidini ya kifikra na ya kisiasa, na hilo lilikuwa mnamo mwezi 17/02/1433.H  sawa na tarehe 11/01/2012. AB hali ikatulia, na makundi ya kitaifa yakanusurika kuingia katika mtafaruku mkubwa, na kupora mapinduzi na kuwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na tunamshukuru Mungu Mola wa viumbe vyote kwa hilo.

Na ikawa tamko la tano na lamwisho ni kuhusu (Al-Quds Al-Sharif) wakati ambapo adui mporaji alipozidisha kasi na hatua za kuufanya Uyahudi katika mji mtakatifu, ni msikiti ambao umekuwa ndio kibla ya kwanza ya Waislamu, na ni msikiti wao mtakatifu wa tatu, ni sehemu aliyopelekwa usiku Mtume wao S.A.W. na ni sehemu pia ilipoanzia safari ya Mtume wa Waislamu ya kwenda mbinguni katika safari yake tukufu ya Miiraji, na kuthibiti kuwa Quds ni ya Kiarabu tokea karne sitini zilizopita, tamko likabainisha kuwa vitendo vinavyoendelea katika mji wa Quds (Jerusalemu) mtakatifu ikiwa ni pamoja na uadui,  Waislamu na Waarabu wana shime ya kuviondoa, na kubakia eneo hilo liwazi na ruhusa kwa dini zote na madhehebu yote chini ya utawala wa Kiarabu na Kiislamu, waraka ukabainisha kuwa uzayuni wanahatarisha mustakabali wa nchi yao, iliyowekwa katika eneo hili kwa nguvu ya silaha, hii ni kutokana na siasa za uadui kuhusiana na mji huu mtakatifu wa Jerusalemu, tamko hili lilitolewa mnamo mwezi ishirini na nne mfungo tatu mwaka 1432. H sawa na tarehe ishirini mwezi November mwaka 2011 AB.

Makao Makuu ya Azhar wameona kuwa kuandika maneno ya waraka huu wa tano wa historia ni kuhifadhi urithi wa mapinduzi ya Misri kwa upande mmoja, na faida kwa ajili ya kizazi kijacho ambao hawakushiriki katika kutoa waraka huu kwa upande wa pili, lakini pia hautokosa kuwa na faida kwa msomaji wa Kiarabu ambaye ana mtazamo wa kuwepo marekebisho ya kweli yanayothibitisha nguzo za jamii na sehemu zake, na kuhifadhi utamaduni na dini, na kupingana na wale wenye tamaa ya masilahi ya hichi hii na kunyemelea kwa ukaribu, kwenda sawa na roho inayoongoza ulimwengu mzima, inayofungamana na Umma wa tauhid (upwekeshaji) wa kiisalamu, nayo ni kuwa kwenye kilele kama ilivyokuwa katika theluthi ya kwanza ya karne ya kumi na tano ya Hijria.

(Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kushinda katika jambo lake lakini watu wengi hawafahamu) yusouf: 21

 

Imetolewa na Ofisi Kuu Azhar

4 /mfungo nane/ 1432 H.

27/03/2012 AB.

 

                                                                                                                                          Ahmad Tayyib

Sheikh wa Azhar

 

 

 

 

WARAKA WA AZHAR

  1. Waraka wa mustakabali wa Misri.
  2. Tamko la kusaidia matakwa ya raia wa Kiarabu.
  3. Tamko la mfumo wa misingi ya uhuru.
  4. Tamko kuhusu ukamilishaji wa malengo ya mapinduzi.
  5. Tamko la Quds Al-Sharif.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  1. WARAKA WA AZHAR NA JOPO LA WASOMI

KUHUSIANA NA

MUSTAKABALI WA MISRI.

kwa pendekezo zuri la Dk. Ahamad Tayyib sheikh mkuu wa Azhar, lilipelekea kukutana kwa wasomi wa Misri wenye mitazamo na mielekeo mbali mbali ya kifikra na kidini pamoja na idadi ya wanachuoni wakubwa na wanafikra wa Azhar, kupitia kikao chao waliweza angalia kwa pamoja mambo mbali mbali ambayo yanaendelea nchini baada ya mapinduzi ya tarehe ishirini na tano januari, na umuhimu wake katika kuelekea mustakabali wananchi na malengo yake matukufu, na haki za raia wake katika uhuru heshima usawa na uadilifu wa kijamii.

Wajumbe wa kikaos walikubaliana juu ya umuhimu wa kuanzisha mchakato wa kitaifa unao simama kwa kufuata misingi yote na sheria zote unaojadiliwa na pande mbali mbali za jamii ya Misri na kuangaza hatua zilizo bora kuelekea kwenye kuimarisha mifumo ya kifikra yenye kusimamia misingi ya jamii na usalama wa mwelekeo wake.

Na kukili kwa wajumbe wote duru ya Azhar katika kueneza fikra za misingi ya kati na kati na nafasi yake ya kuwa ni chombo cha marejeo, wajumbe walisisitiza umuhimu wa Azhar na kuizingatia ni mnara wenye kuongoza ambao unaangazia, na unasimamia katika kuweka uhusiano wa nchi na dini, na kuweka misingi ya siasa halali na sahihi ambayo yapaswa kufuatwa, kwa kuangalia zaidi kutokana na uzoefu wake na historia yake ya kielimu na kitamaduni ambayo imejikita katika pande zifuatazo:

  1. Upande wa kifiqihi katika kuleta uhai wa elimu za dini na kujenga mitazamo mipya kwa mujibu wa madhehebu ya watu wa sunna na jamaa mitazamo ambao inakusanya kati ya akili na maandiko, na kuelezea misingi ya tafasiri sahihi ya maandiko ya qurani na hadithi.
  2. Upande wa historia ya nafasi ya Azhar katika kuongoza harakati za kitaifa kuelekea uhuru na ukombozi.
  3. Upande wa ustaarabu katika kurejesha uhai wa elimu mbali mbali asilia fasihi na sanaa kwa aina zake mbali mbali.
  4. Upande wa kielimu katika kuongoza harakati za jamii na kutengeneza jopo la wanataaluma katika maisha ya Kimisri.
  5. Upande wa chuo kikuu kwa ajili ya elimu maendeleo na utamaduni wa ulimwengu wa Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu.

Wajumbe wa kikao walikuwa na shime kubwa kuanza mjadala wao kwa kuangalia urithi wa wasomi wenye fikra na mitazamo ya harakati za maendeleo na marekebisho ndani ya Azhar Al-Sharif, kuanzia kwa sheikh wa Uislamu sheikh Hassan Al-Attaar na mwanafunzi wake sheikh Rifaat Al-ttahtawiy, Imam Mohammad Abdul na wanafunzi wake katika wanachuoni wa Azhar na Maimamu wake mfano wa Imam Al-Maraghiy, Mohammad Abdallah Daraz, Mustafa Abdulraziq, Shaltuot na wengineo katika masheik wa Uislamu, na wanachuoni wa Azhar.

Wakati huo huo walianza pia kuangalia mafanikio yaliyofikiwa na wanachuoni wakubwa wa Kimisri ambao walishiriki katika kazi za maboresho ya kimaarifa na kiubinadamu, na kutoa mchango mkubwa katika kutengeneza mitazamo mipya ya Kimisri na Kiarabu, wakiwemo wasomi wa mambo ya sheria, falsafa, fasihi, sanaa na mengineyo katika maarifa ambayo yalitengeneza fikra na mwamko wa jamii, walijitahidi katika kufanya yote hayo na kuangalia zaidi katika kuweka mgawanjo wa pamoja kati yao wote, mgawanyo ambao unalenga kufikia lengo kuu ambalo lenye ridhaa kwa wote kuanzia wasomi wa Umma na viongozi wake, malengo ambayo yapo kama ifuatavyo:

Kuandaa misingi ya kufahamu mahusiano ya Uislamu na Dola ndani ya kipindi hiki, na hiyo ni katika wigo wa mkakati wa makubaliano, kuchora sura ya taifa la kisasa linalohitajika na mfumo wa utawala, na kuwasukuma wananchi katika njia ya kuelekea kwenye maendeleo na ustaarabu, ili kufikia mchakato wa mabadiliko ya kidemokrasia na kudhamini hali ya usawa wa kijamii, na kuingia nchi katika zama za uzalishaji maarifa, elimu, na kufikia mafanikio na amani, pamoja na kuhifadhi misingi ya kiroho kibinadamu na urithi wa kitamaduni,  na hiyo ni kwa lengo la kulinda misingi ya Kiislamu ambayo imejikita katika mwamko wa Umma na dhamiri ya wanachuoni na wanafikra kutokana na kukumbwa na ujinga upotoshaji au siasa kali na tafasiri mbaya, kuilinda kutokana na kutumiwa vibaya na pande mbali mbali zenye kukiuka ambazo zinaweza inua alama za ubaguzi wa kidini kikabila au kiimani zinazo pingana na misingi thabiti ya Umma wetu na yale yanayoshirikisha Waislamu wengine, na kwenda kinyume na mfumo wa kati na kati, na kupingana na sura ya Uislamu katika mambo ya uhuru uadilifu na usawa, na kuwa mbali na misingi ya kuvumiliana katika dini zote za mbinguni.

Kutokana na hilo tunatangaza makubaliano yetu – sisi wajumbe tuliokutana – katika misingi ifuatayo ili kuonesha asili ya marejeo ya Kiislamu, ambayo inakusanya misingi katika kadhia mbali mbali, itokanayo na maandiko ya kisheria yaliyo thibiti na dalili, kwa sifa yake kuwa ni kivuko cha uelewa sahihi wa dini, na tunaikusanya katika maudhui zifuatazo:

Maudhui ya Kwanza: kuanzisha nchi ya kisasa ya kiraia kikatiba na kidemokrasia, ambayo inategemea katiba inayoridhiwa na wananchi, inatenganisha kati ya mamlaka za nchi na asasi zake za kisheria zinazoongoza, inapangilia wigo wa utawala, inadhamini haki na wajibu wa kila mtu kwa usawa ambapo mamlaka ya kutunga sheria inakuwa ndani yake ina wawakilishi wa wananchi (wabunge) katika sura ambayo inakubaliana na uelewa sahihi wa Uislamu, ambapo Uislamu haujapatapo kufahamu si katika sheria zake ustaarabu wake wala historia yake kile kinachofahamika katika tamaduni zengine kuwepo kwa dola ya kidini ya kikuhani ambayo inatawala watu kwa nguvu, na watu kuishi katika hali ya matatizo kwa baadhi ya wakati, lakini Uislamu umewaachia watu kusimamia na kuendesha jamii zao pamoja na kuchagua vyombo na asasi vitakavyo leta masilahi yao, kwa sharti ya kuwa misingi ya sheria ya Kiislamu ndiyo msingi mkuu wa kutunga sheria, na kutoa dhamana kwa wafuasi wa dini zengine za mbinguni kusimamia sheria zao za kidini katika sheria za hali za kifamilia kama vile mambo ya ndoa talaka na mengineyo.

Maudhui ya Pili: kutegemea nidhamu ya kidemokrasia, inayosimama kwa utaratibu wa uchaguzi huru na wamoja kwa moja, ambao ndio mfumo wa kisasa ili kufikia misingi (shura) mashauriano ya Kiislamu, jambo ambalo litadhamini mfumo wa vyama vingi na mzunguko wa madaraka kwa njia salama, na kupanga vitengo mbali mbali, kusimamia utekelezaji, kufikishwa kwenye vyombo vya sheria maafisa wawakilishi wa raia, kuchunga manufaa na masilahi ya Umma katika sheria zote na maamuzi yote, kuendesha idara ya mambo ya dola kisheria, kuthibiti ufisadi, kufikia hali ya uwazi na uhuru wa kupata maelezo.

Maudhui ya Tatu: kulazimika na mfumo wa misingi ya uhuru katika fikra na rai, pamoja na kuheshimu kikamilifu haki za binadamu mwanamke na mtoto,   kuheshimu dini za mbinguni, na kuzingatia uraia ni suala la wananchi wote.

Maudhui ya nne: kuheshimu kikamilifu maadili ya mazungumzo na umuhimu wa kuepukana na kukufurisha uhaini kuitumia dini kutengeneza makundi na uadui kati ya wananchi, pamoja na kuzingatia kueneza fitina za makundi na miito ya ubaguzi ni uhalifu dhidi ya haki za wananchi, na ulazima wa kutegemea mazungumzo na kuheshimiana na kutegemeana katika mashirikiano kati ya makundi mbali mbali ya kiraia, pasi ya kuwepo mgawanyiko wowote ule katika haki na wajibu kati ya wananchi.

Maudhui ya Tano: kuwajibika na makubaliano pamoja na maamuzi ya kimataifa, na kushikamana na mafanikio ya kistaarabu katika mahusiano ya kibinadamu, yanayokubaliana na misingi ya kuvumiliana katika tamaduni za Uislamu na Kiarabu, yanayokubaliana hayo na uzoefu wa ustaarabu wa raia wa Misri wa muda mrefu kwenye zama zake mbali mbali, na kile kilichooneshwa miongoni mwa mifano mizuri ya kuishi pamoja kwa usalama na kuleta kheri kwa wanadamu wote.

Maudhui ya Sita: shime kamili ya kutengeneza heshima kwa Umma wa Kimisri na kuhifadhi nguvu yake kitaifa, kuimarisha ulinzi kamilifu na heshima zote kwa duru ya ibada kwa wafuasi wa dini tatu za mbinguni, kudhamini vitendo vyote huru vya alama zote za kidini pasi ya ukwamishaji wa aina yeyote, kuheshimu sura zote za ibada kwa aina zake tofauti pasi ya kupuuza utamaduni wa wananchi au kuchafua uasili wa desturi, pia shime ya kutengeneza uhuru wa kujieleza ubunifu wa kisanaa na kifasihi katika wigo wa mfumo wa misingi yetu thabiti ya ustaarabu.

Maudhui ya Saba: kuzingatia elimu na utafiti wa kielimu na kuingia katika zama za maarifa kuwa ni nukta ya maendeleo ya ustaarabu nchini, kukusanya juhudi ili kufahamu yale yaliyotupita katika mambo ya elimu na kushirikisha nguvu ya jamii yote ili kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika, na kuwekeza kwenye rasilimali watu, na kufikia miladi mikubwa ya hapo baadaye.

Maudhui ya Nane: kuifanyia kazi fiqihi ya vipaombele vya kufikia maendeleo na uadilifu wa kijamii, kupambana na ukandamizaji, kupambana na ufisadi, kupambana na ukosefu wa ajira, jambo ambalo litalipua nguvu ya jamii na ubunifu wake katika pande za uchumi na mpango wa kijamii na kitamaduni, hayo yanakuja katika vipaombele ambavyo vinajengwa na wananchi wetu katika maendeleo yao ya hivi sasa, pamoja na kuzingatia huduma za afya za dhati na za kweli ni wajibu wa nchi kwa wananchi wote.

Maudhui ya Tisa: kujenga mahusiano ya Misri na ndugu zake Waarabu na maeneo ya Kiislamu Afrika na dunia, kutetea haki za Mpalestina, kuhifadhi uhuru wa utashi wa Misri, kurejesha duru ya uongozi wa historia kwa Misri juu ya msingi wa mashirikiano ya pamoja, na kufikia masilahi ya raia katika wigo wa usawa na uhuru kamili, kufuatilia ushiriki katika juhudi za kibinadamu kwa ajili ya maendeleo ya watu, kuhifadhi mazingira na kufikia amani kati ya mataifa.

Maudhui ya Kumi: kuunga mkono uhuru wa taasisi ya Azhar, kurejesha “jopo la wanachuoni wakuu wa Azhar” na kulihusisha kutoa mgombea na kuteua Sheikh Mkuu wa Azhar, kufanya kazi ya kuboresha mitaala ya elimu ya Azhar, ili kurudisha duru asili ya Azhar ya kifikra, na athari zake kimataifa ndani ya maeneo mbali mbali.

Maudhui ya Kumi na Moja: kuzingatia Azhar ndiyo upande husika wa kurejewa katika mambo ya Kiislamu, elimu zake urithi wake na juhudi zake za kifiqihi na fikra za kisasa, bila kuondolewa haki ya wananchi katika kutoa rai wakati ambapo masharti ya kielimu ya lazima yatakapofikiwa, na kwa sharti la kuwajibika kufuata adabu za mazungumzo, na kuheshimu yaliyofikiwa na wanazuoni wa Umma.

Wanachuoni wa Azhar na wanachuoni wengine wenye kushiriki katika kuandaa matamko haya wanatoa wito kwa vyama vyote na pande mbali mbali za kisiasa nchini kuwajibika kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Misri kisiasa kiuchumi na kijamii, katika wigo wa vigezo vikuu ambavyo vimo kwenye waraka huu.

           Mwenyezi Mungu Mwezeshaji kwa yale yenye kheir kwa Umma

 

            Imetolewa Makao Makuu Azhar

17/Mf.Kumi/1432 H.

       19/June /2011

 

              Wanachuoni wa Azhar

                 Jopo la wasomi

                 Sheikh wa Azhar

 

 

 

 

 

2. TAMKO LA AZHAR NA JOPO LA WASOMI

            ILI KUSAIDIA UTASHI WA RAIA WA KIARABU.

Kuanzia na ufahamu wa wanachuoni wakubwa wa Azhar, na jopo la wasomi wanaoshiriki na wana Azhar juu ya mahitaji ya hatua ya kihistoria ambayo wanapita wananchi wa Kiarabu katika mapambano kwa ajili ya uhuru uadilifu na demokrasia, na kuanza mchakato wa ustaarabu, na kuhamasisha roho ya ukombozi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na kanuni za kifiqihi kwa ajili ya utawala, na duru yake katika marekebisho na kufikiwa kwa makusudio na masilahi makuu ya Umma, yakienda sambamba na msimamo wa Azhar Sharif, na viongozi wa Misri na ulimwengu wa Kiarabu, katika kusaidia harakati za ukombozi toka mikononi mwa mkoloni katili na mkandamizaji dhalimu, ni imani kwa wote juu ya umuhimu wa kuamka kwa umm ili kuchukuwa sababu za kuinuka na maendeleo, na kuweka wananchi katika usawa wa kijamii, kwa kuwa na misingi madhubuti katika misingi ya sheria, jambo ambalo litadhamini kuhifadhi akili dini nafsi heshima na mali. Na kuziba njia kwa serikali ambayo inayozuia jamii ya Kiarabu na Kiislamu kuingia kwenye zama kufanya vizuri kiustaarabu na maendeleo ya kimaarifa, kutoa mchango katika kufikia ustawi wa kiuchumi na maendeleo kwa ujumla: hakika ya jopo ambalo limetoa waraka huu wa Azhar limewakilisha makundi mbali mbali ya wasomi ndani ya jamii ya Kimisri, jopo hili lilifanya mazungumzo kadhaa yenye kujenga kuhusiana na yale yaliyofikiwa na mapinduzi ya Kiarabu miongoni mwa matumaini, na muitikio mzuri kati ya makundi mbali mbali, na kukubaliana misingi yote inayotokana na fikra ya Kiislamu, na matarajio ya baadaye kwa raia wa Kiarabu, na kumalizikia kwa usimamizi wa Azhar Sharif kutangaza juu ya kuheshimu makubaliano yafuatayo:

Ya Kwanza: kutegemea serikali tawala mitazamo ya kidini na kikatiba kwa ridhaa ya wananchi, na kuchaguliwa kwake kuwe huru kupitia upigaji kura kunakofanyika kwa uwazi na kidemokrasia, kwa kuzingatia kuwa ndio njia mbadala ya kisasa ukilinganisha na ile iliyopita ya desturi ya Kiislamu iliyobora ya uungaji mkono, na kutokana na mabadiliko ya mifumo ya utawala na hatua zake ndani ya nchi za kisasa, na katika yale yaliyokubalika na desturi za kikatiba miongoni mwa mgawanyo wa mamlaka ya bunge mahakama na mamlaka ya utendaji, na mtengano uliopo kati ya mamlaka hizo, na katika udhibiti wa njia za usimamizi na uwajibikaji, ambapo wananchi wanakuwa ndio chanzo cha mamlaka zote, viongozi wengi walipanda daraja na viwango katika kuimarisha serikali zao wakishikilia na kung`ng`nia uelewa wao wenye mapungufu wa aya tukufu ya quran pale Mwenyezi Mungu aliposema katika aya 59 ya surat – Annisaa. (Enyi mulioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mumtii Mtume pamoja na wale wenye madaraka kwenu) wakiwa hawafahamu mtiririko wa wazi wa kauli yake Mwenyezi Mungu kabla ya hapo katika aya ambayo imekuja kabla ya aya hii moja kwa moja, pale Mola mtukufu aliposema: (Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni nyinyi kurejesha amana za watu kwa wenyewe, na pindi munapo hukumu “kuongoza” watu basi hukumuni “ongozeni” kwa kufuata misingi ya uadilifu) jambo ambalo linapelekea pindi inapokosekana sharti la uaminifu katika kutoa hukumu au katika  kuongoza na pia kuto kusimamishwa uadilifu ndani yake, basi kunapatikana haki ya kisheria kwa wananchi kuwataka viongozi wao kusimamisha uadilifu na kupambana na dhuluma pamoja na ukandamizaji, na mwenye kusema katika wasomi wetu kuwa ni wajibu wa kusubiri kwa watawala wakandamizaji waliopo madarakani ili kuepuasha fujo ndani ya nchi pamoja na kuchunga usalama wa wananchi, basi wakati huo huo msomi huyo atakuwa ameruhusu kutengwa mkandamizaji dhalimu wakati wowote atakapokuwa na uwezo wa kufanya ukandamizaji huo, na kutoangalia athari za uwezekano wa kutokea uharibifu na madhara kwa usalama wa Umma na jamii zake.

Ya Pili: pindi zinapopaza sauti za upinzani wa kitaifa wa kiraia na kupinga kwa kufuata njia za kiusalama, ambapo jambo hilo ni haki asili kwa wananchi katika kuwatathmini viongozi wao na kuwaongoza, kisha viongoizi wakawa si wenye kuitikia wito wa wananchi wao, na wala kutofanya haraka kufanya marekebisho yanayotakiwa, isipokuwa ni kufanya ufedhuli na kujitia ujinga juu ya matakwa halali ya wananchi ambayo yanalingania uhuru uadilifu na usawa, basi hawa wapinzani wa kitaifa hawatozingatiwa katika watu waovu, bali waovu ni wale ambao zimeelezewa sifa zao kifiqihi kwa kumiliki miba na kuutenga Umma, kuinua silaha katika kupambana na wale wanaowapinga, pamoja na kufanya uharibifu ndani ya nchi kwa nguvu, ama kwa upande wa harakati za kitaifa zilizo salama za upinzani, nazo ni katika haki asili za binadamu ndani ya Uislamu kama vile ilivyoelezewa pia katika makubaliano mengi ya kimataifa, lakini pia ni wajibu wa raia kurekebisha jamii zao na kuwatathmini viongozi wao, kuitikia utashi huo wa wananchi ni jambo la lazima kwa viongozi na watu wenye mamlaka, pasi ya kupiga chenga au kuleta ubishi.

Ya Tatu: inazingatiwa kupambana kwa nguvu na kutumia silaha dhidi ya maandamano yeyote ya kitaifa yaliyosalama, na kumwaga damu za wananchi waliosalama, ni kwenda kinyume na mikataba ya utawala kati ya raia na viongozi wao, hapo unaondoka uhalali wa serikali iliyopo madarakani, na kupoteza haki ya kuongoza kwa njia ya ridhaa ya wananchi, na serikali ikiendelea na ukiukaji wake na kuendesha vitendo vya dhuluma ubaya uadui na kumwaga damu za wananchi wasio na hatia ili kuendelea kubakia madarakani kinyume na uhalali – hata kama watakaa kwa utashi wa raia wao – serikali itakuwa ipo hatiani kwa uhalifu, na inakuwa ni haki ya wananchi waliodhulumiwa kuwatenga watawala wa  kimabavu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, lakini pia kubadilisha mfumo wote wa utawala, kwa nyudhuru zozote zitakazokuwa, hii ni kutokana na umuhimu  wa kuwepo kwa utulivu ndani ya nchi au kupambana na fitina pamoja na njama za viongozi, kukiuka uharamu wa umwagaji damu ni msitari unaotenganisha kati ya utawala halali na kuporomoka kwake katika dhambi na uadui, ni jukumu la jeshi – katika nchi zetu zote -  katika hali hii kulazimika na wajibu wake wa kikatiba katika kulinda nchi kutokana na uadui wowote utokao nje, na wala halipaswi kuwa ni chombo cha uminyaji kutisha wananchi na kumwaga damu zao ndani ya nchi, kwani Mola mtukufu anasema:(Mwenye kuuwa nafsi pasi na nafsi au kufanya uharibifu nchini  basi kana kwamba ameua watu wote, na mwenye kuiacha hai nafsi, basi ni kana kwamba ameacha hai watu wote) Al-maaidat: 32.

Ya Nne: inatakiwa kwa wana mapinduzi wajenzi wapya na warekebishaji kujitenga moja kwa moja na kila chenye kupelekea umwagaji damu, na kutafuta nguvu za ziada toka vyanzo vya nje ya nchi vyovyote vile vitakavyokuwa vyanzo hivyo, na vyovyote itakavyokuwa sababu ambayo itapelekea kuingilia kati masuala ya nchi yao, kinyume na hivyo watakuwa ni waovu wamekwenda kinyume na wananchi wao na pia sheria za nchi yao. Hapo mamlaka ya nchi italazimika kuwarejesha kwenye umoja wa safu ya nchi ambayo ni ulazima wa kwanza na niwajibu katika wajibu mkubwa. Na pande za mapinduzi na marekebisho wanalazimika kuungana katika kufikia ndoto yao kwa njia ya uadilifu na huru, na kuepukana na mivutano ya makundi ukabila madhehebu au dini, ili kuhifadhi umoja wao wa kitaifa, na kuheshimu haki za uraia, pamoja na kukusanya nguvu kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa masilahi ya wote, katika wigo wa makubaliano na mashirikiano ya kitaifa, na katika hali ambayo hayatobadilika mapinduzi na kuwa masilahi ya kikundi au madhehebu fulani, au kuibua hisia za kidini, lakini inatakiwa kwa wanamapinduzi na wajenzi wapya pamoja na warekebishaji kuhifadhi asasi za nchi yao, na kutopoteza mali zao kuziachia kwa masilahi ya wale wenye kunyemelea nchi, na kujiepusha kuingia kwenye tofauti na ushindani, pamoja na kutafuta nguvu zenye tamaa na nchi zao au kuhamisha kheiri za nchi yao.

Ya Tano: kutokana na misingi hii ya Kiislamu na kikatiba, inayoelezea mwamko wa kiustaarabu, wanachuoni wa Azhar na viongozi wanataaluma, wanatangaza utetezi wao kamili wa matakwa ya wananchi wa Kiarabu katika marekebisho, na jamii huru na uadilifu wa kijamii ambao umepatikana nchini Tunisia Misri na Libya, lakini bado haujapatikana nchini Syria na Yemen, wanalaani vitendo vya uminyaji, na wanatoa wito kwa jamii ya Kiarabu na Kiislamu kuchukuwa mapendekezo makali na yenye kufanya kazi ili kulinda mafanikio yake kwa kiwango kidogo cha hasara, kusisitiza haki ya raia katika kuchagua viongozi, na wajibu wao katika kuwatathmini ili kuzuia uovu uharibifu na matumizi mabaya ya madaraka, uhalali wa serikali yeyote upo rehani kwa matakwa ya wananchi, na haki ya wapinzani wa kitaifa wasiobeba silaha inasimamiwa na sheria ya Kiislamu katika wajibu wa kuondoa madhara, kuongezea pia kuwa ni katika misingi ya haki za binadamu kwenye mikataba yote ya kimataifa.

Ya Sita: wanatoa wito wanachuoni wa Azhar na wasomi wanaoshiriki nao juu ya mifumo ya kiarabu na Kiislamu inayotawala, wanatoa wito juu ya shime ya mapendekezo ya kufikia marekebisho ya kisiasa kijamii na kikatiba kwa hiyari, na kuanza hatua za mabadiliko ya kidemokrasia, muwamko wa wananchi wanaoteswa unakuja bila ya wasi wasi wowote, na wala si katika uwezo wa kiongozi hivi sasa kuzuia miyale ya uhuru, ni katika aibu eneo la Kiarabu na baadhi ya nchi za Kiislamu kuwa tofauti na nchi zengine, zimekuwa katika hali ya kuchelewa kudhulumiwa na uovu, na kunasibishwa hayo ya dhuluma na uzushi ni katika Uislamu na tamaduni zake, wakati Uislamu upo mbali kabisa na uzushi huu, kama zinavyotakiwa nchi hizi kufanya haraka kuchukuwa sababu za maendeleo ya kielimu na kiteknolojia na uzalishaji wa maarifa, na kuwekeza nguvu yake ya rasilimali watu na mali zake asilia ili kuhudumia wananchi wake, na kufikia furaha kwa watu wote.

Hii, wala asije dhania yeyote katika wale wanye kulea ukandamizaji na upotovu kuwa ni mwenye kuokoka na mwisho wa madhalimu, au kwa nafasi yake kupoteza wananchi, kwani ni zama za mawasiliano ya wazi na milipuko ya maarifa, mifano ya kujitoa muhanga na kupigania ukombozi unashuhudiwa wazi kabisa katika ulimwengu wa Waarabu, yote hayo yamefanya mwamko wa watu ni kizinga cha moto chenye kutoa cheche, na katika uhuru ni bendera iliyopandishwa, na katika matumaini ya wananchi wenye kudhulumiwa kuna msukumo ukiongozwa na mapambano ya uhuru mpaka upatikane ushindi. Na waache wale wajinga wa dini, wachafuaji wa mafunzo ya dini, na walinganiaji wanaounga mkono upotofu dhuluma na ukandamizaji waache huu mchezo wa kipuuzi ambao usio na manufaa yeyote nyuma yake.

(Na Mwenyezi Mungu ni mshindi juu ya jambo lake, lakini watu wengi hawajui) surat Yousuf – 21.      

Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba huruma itakayoongoza nyoyo zetu, kukusanya mambo yetu, na kutuondolea fitina ewe Mola wa viumbe vyote.

 

                       Imetolewa na Makao Makuu Azhar:

                      03 /Mf: tatu/1432 H.

                       30/ Oct / 2011 AB.

 

    Ahmad Tayyib

  Sheikh wa Azhar  

 

 

 

 

Tamko la misingi ya mfumo wa uhuru

3 – TAMKO LA AZHAR NA WASOMI

(KUHUSU MISINGI YA MFUMO WA UHURU)

Wamisri, Umma wa Kiarabu na wa Kiislamu wanakusudia baada ya mapinduzi ya ukombozi ambayo yameanzisha uhuru na kuchochea roho ya mwamko wa kina kwa pande mbali mbali ikiwa pamoja na pande za wasomi wa Umma na wanafikra wao kujenga uhusiano wa kati ya misingi ya sheria za Kiislamu zenye usamehevu na misingi ya mfumo wa uhuru ambao imekusanywa ndani ya makubaliano ya kimataifa, na kupelekea misingi hiyo jaribio la ustaarabu wa raia wa Misri, ni mwendelezo wa misingi hiyo, na kuelezea uthibiti wake, kuweka masharti yake ambayo yanalinda harakati za maendeleo na kufungua peo za mustakabali. Misingi hiyo ni uhuru wa Imani uhuru wa mawazo na kuelezea uhuru wa utafiti wa kielimu na uhuru wa ubunifu fasihi na sanaa, juu ya msingi thabiti wa ustawi wa makusudio ya sheria na kuelewa roho ya sheria ya katiba ya kisasa na yanayopelekea maendeleo ya maarifa ya kibanadamu, jambo ambalo linapelekea nguvu ya kiroho ya Umma kuwa ni nishati kwa ajili ya maendeleo msukumo wa kusonga mbele na njia ya kuinuka ki hali na kimali, katika juhudi za kuunganisha hutuba za kitamaduni na hutuba za kidini na kuungana pamoja kwa mustakabali wenye kuzaa matunda, yanaungana ndani yake malengo na makusudio ambayo yanakubalika na wote.

Kutokana na hilo jopo la wa wanachuoni wa Al-Azhar na wasomi wengine nchini Misri ambao wametoa waraka wa kwanza wa Al-Azhar chini ya udhamini wa Al-zhar Al-sharif, na kufuatiwa na tamko la kuunga mkono harakati za raia wa Kiarabu ndugu kuelekea katika uhuru na demokrasia – harakati zao ziliendelea na kufundishana wenyewe kwa wenyewe mambo ya fikra za pamoja katika mifumo ya uhuru na haki za binadamu, na wakamalizia kwa kufikia misingi na uthibiti wa uhuru huu, kulingana na mahitaji ya historia ya hivi sasa, na kuhifadhi utangamano wa kijamii, kuchunga masilahi ya Umma katika hatua ya mabadiliko ya kidemokrasia, ili Umma uelekee katika kujenga asasi zake za kikatiba kwa amani na uadilifu na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na kwa kuto ruhusu kuenea miito yenye malengo ambayo inapandikizwa kwa hoja za kuamrisha mema na kukataza maovu ili kuingilia uhuru wa mtu au wa Umma, jambo ambalo haliendani na maendeleo ya kistaarabu na ya kijamii ndani ya Misri ya hivi sasa, ndani ya wakati ambao nchi inahitaji kuwa na tamko moja na uelewa sahihi wa kati na kati wa dini ambao ndio ujumbe wa kidini wa Al-Azhar na ni jukumu lake kwa jamii na Taifa.

Msingi wa Kwanza: Uhuru wa Imani.

Unazingatiwa uhuru wa imani na yanayofungamana nayo, ni katika haki kamili ya raia wote, inayosimama katika misingi ya usawa katika haki na wajibu ni jiwe la msingi katika ujenzi wa jamii ya kisasa, nao unasimamiwa na matamko thabiti ya dini na uwazi wa msingi wa kikatiba na kikanuni, Mwenyezi Mungu mtukufu anasema {hakuna kulazimisha katika dini, kwani uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu} suratul Baqarah – 256.

Na anasema tena Mwenyezi Mungu {basi atakae na aamini na takae basi akatae} suratil Kahfi – 29}.

Na katia yanayofungamana na kitendo cha jinai, kwa maana kufanya kitendo cha kulazimisha katika dini, au kutesa kubagua kwa sababu ya dini, kwani mtu yeyote kwenye jamii ana haki ya kufuata fikra aitakayo pasi ya kugusa haki ya jamii katika kuhifadhi imani ya mbinguni, dini za mbinguni tatu mtu ana uhuru wa kusimamisha alama za dini hizo pasi ya kufanya uadui kwenye hisia za wengine au kugusa utukufu wake kwa kauli au kitendo na pasi ya kukiuka mfumo wa umma.

Na wakati ulipokuwa ulimwengu wa Kiarabu ndio mafikio ya wahyi (ufunuo) toka mbinguni na chimbuko la dini za Mungu – basi ulikuwa ni wenye kuwajibika kuchunga utakatifu wa dini kuheshimu alama zake na kulinda haki za waumini katika uhuru hadhi na undugu,

Na yanayofungamana katika haki ya uhuru wa imani ni kukubali uhalali wa uwepo wa dini nyingi na kuchunga haki ya kutofautiana kiitikadi na wajibu wa kuchunga kila raia hisia za wengine na usawa uliopo kati yao, wenye kusimama katika misingi imara ya uraia ushirikiano na fursa sawa katika haki zote na wajibu.

Kama vile yanayofungamana katika kuheshimu uhuru wa imani, ni kupinga mielekeo ya kibaguzi na kukufurisha, lakini pia kupinga mielekeo ambayo inalaani imani za watu wengine na jaribio la kupembua dhamira za waumini katika imani hizi, hili ni kwa mujibu wa yaliyofikiwa katika mifumo ya kikatiba bali yaliyofikiwa – kabla ya hapo – na wanachuoni katika hukumu za wazi kabisa zilizokubalika na sheria za usamehevu katika athari za mtume mtukufu: (je ulifungua kifua chake?) na katika yele yaliyopitishwa na Imam wa watu wa Madina Munawwarah Imam Malik pamoja na Maimam wengine kauli yake: “inapotolewa kauli ya mwenye kusema, pande mia moja inachuliwa ni kufuru, lakaini upande mmoja tu ndio unazingatiwa ni katika iman, lakini hata hivyo unazingatiwa upande wa imani na wala haifai kuzingatiwa upande wa ukafiri” Maimam wa jitihada na mambo ya sheria wameipa nafasi kubwa sana akili katika Uislamu, na wakatuachia msingi wao wa dhahabu ambao unasema kuwa: “pindi kunapotokea mgongano kati ya mtazamo wa kiakili na andiko, basi kwanza huangaliwa mtazamo wa kiakili na hutolewa maelezo na tafasiri juu ya andiko”  ni katika kuchunga maslahi yanayozingatiwa na kufanyiwa kazi malengo ya sheria.

Msingi wa Pili: Uhuru wa Maoni na Kujieleza.

Uhuru wa maoni ni uhuru mama wa wote, na kunajitokeza katika kuelezea maoni, uhuru wa kujielezea kwa njia mbali mbali za kujielezea kuanzia njia ya uandishi hutuba uzalishaji sanaa mawasiliano ya kidijitali na zenginezo, nayo ni sura ya uhuru wa kijamii ambao unavuka kwa mtu mmoja mmoja na kwenda kwa wengine mfano kama vile kuanzisha vyama na mashirika ya kiraia, pia uhuru wa vyombo vya habari vya sauti vya kuona na vya dijitali, pia unazingatiwa uhuru wa kupata maelezo ya lazima ili kuweza toa rai, na lazima uhuru uwe unasimamiwa na vipengele vya kikatiba ili kuziinua kanuni za kawaida zenye kubadilika kwa haraka. Mahakama kuu ya katiba nchini Misri imepanua uelewa wa maana ya uhuru wa kueleza ikiwa ni pamoja na kauli za ukosoaji zenye kujenga hata kama zitakuwa na maneno makali na imetamka mahakama kuwa: “haifai kuufunga uhuru wa kuelezea katika kadhia za jamii pasi na ukiukaji lakini kinacho angaliwa ni kuvumiliana” lakini kuna umuhimu wa kuzinduana juu ya ulazima wa kuheshimu imani za dini tatu za Mungu pamoja na alama zake na hii ni kutokana na hatari juu ya umoja wa kitaifa na usalama wake. Wala sio haki ya mtu yeyote kuibua fitina za kikabila au ugonvi wa kidini kwa jina la uhuru wa kueleza, na ikiwa haki ya jitihada ya rai ya kielimu na kisayansi inafungamanishwa na dalili na kwa kupitia watu wenye weledi na kuwa mbali kabisa na kuibua hisia kali za watu kama ilivyoelezewa katika uhuru wa utafiti wa kielimu.

Wanachuoni wanatangaza kuwa uhuru wa maoni na kuelezea ni muonekano wa kweli wa demokrasia, wanatoa wito wa kuanzisha kwa kizazi kipya na kukilea katika utamaduni wa uhuru, haki ya kutofautiana na kuheshimu wengine, na kutoa wito kwa wanaofanya kazi za hutuba za kidini kitamaduni kisiasa kwa kutumia vyombo vya habari kuangalia sana upande huu katika kazi zao, na kuwe na hekima katika kujenga maoni ya umma yenye kubeba sehemu kubwa sifa ya kuvumiliana pamoja na kuwa na utamaduni wa mazungumzo na kupinga utumiaji nguvu, na inapaswa ili kuyafikia hayo ni kuwa na ustaarabu wa fikra ya Kiislamu ambayo imesemwa na maimamu wakubwa kuwa: “maoni sahihi yanakadiriwa kuwa na makosa ndani yake, na maoni yasio sahihi yanakadiriwa kuwa na usahihi” kutokana na hivyo basi hakuna njia ya kuukinga uhuru wa maoni isipokuwa ni kupambana hoja kwa hoja kwa kufuata adabu za mazungumzo na njia za kiistaarabu za jamii zilizo staarabika.

Msingi wa tatu: Uhuru wa tafiti za kielimu.

Unazingatiwa utafiti wa kina wa kielimu katika elimu za kibinadamu elimu za kiasili na zenginezo ndio msingi wa maendeleo ya mwanadamu, na ni njia ya kugundua mfumo wa ulimwengu na kufahamu kanuni zake ili kurahisisha upatikanaj wa kheir zake kwa binadamu, na wala haiwezekani kwa utafiti huu kukamilika na kuleta matunda yake ya kinadharia na vitendo pasi ya kuhusisha nguvu ya umma na kukusanya uwezo wa umma kwa ajili hiyo, kwa hakika kumekuwa na maandiko mengi ndani ya qurani tukufu yakihimiza na kusisitiza juu ya kuangalia kwa mtazamo wa kina na wakufikiria kungundua kupima na kuzingatia matukio ya kilimwengu  na kibanadamu ili kugundua mifumo yake na kanuni zake, na imeandaa njia ya kuyaelekea maendeleo makubwa ya kisayansi katika historia ya Mashariki, na kufikiwa maendeleo hayo na yalifurahisha pande zote za mashariki na magharibi, wanawachuoni wa Kiislamu waliongoza maendeleo hayo na kubeba mwenge wake ili upate angaza zama za maendeleo ya magharibi kama vile inavyofahamika na kuthibiti. Na ikiwa swala zima la kufikiri kiakili na kimazingatio katika pande mbali mbali ni jambo la lazima katika Uislamu kama wanavyosema wenye kujitahidi kuwa, utafiti wa elimu ya kinadharia na ya majaribio ndio chombo cha hii fikra. Na katika mashariti yake muhimu ni kumiliki taasisi za utafiti na wasomi wenye weledi uhuru wa kamili katika kufanya majaribio mbali mbali na kuweka maangalizo ya kielimu na makadario ya uwezekano na kuyapima kwa vipimo vya kina vya kielimu, na katika haki za taasisi hizi ni pamoja na kumiliki mawazo ya ubunifu na uzoefu ili kufikia kwenye matokeo mengine mapya yataongeza uelewa wa kibanadamu, kwa hakika walikuwa wasomi wa kubwa wa Kiislamu mfano wa Al-raziy Ibn Haitham Ibn Al-nnafis na wengineo ni mabwana wa maarifa ya kielimu na mwanga eneo la mashariki na magharibi kwa karne nyingi, umefika wakati sasa kwa Umma wa Kiarabu na Kiislamu kurudi kwenye ushindani mkubwa na kuingia katika zama za maarifa, kwani elimu imekuwa ndio msingi wa nguvu za kijeshi kiuchumi lakini ni sababu ya kusonga mbele maendeleo na ustawi, na utafiti uhuru wa kielimu umekuwa ndio siri ya maendeleo ya elimu fikra na kuboreka kwa vituo vya uzalishaji tafiti ambavyo vinatengewa bajeti kubwa ya fedha, na kutengenezewa timu za kazi na kupendekezewa miradi mikubwa, yote hayo yanahitaji dhamana ya utafiti mkubwa wa kielimu na kibanadamu. Nchi za magharibi zimekaribia kukamata kwa mikono yao maendeleo yote ya kisayansi na kumiliki nyenzo za elimu, lau yasingekuwa mapinduzi ya maendeleo ya Japan China India na maeneo ya kusini mashariki mwa Asia ambazo zimeonesha mfano wenye mwanga wa kuonesha uwezo wa eneo la mashariki wa kuvunja ukiritimba huu wa kielimu, na kuingia katika zama za elimu na maarifa kwa kupitia mlango mpana zaidi, na wakati umefika hivi sasa wa kuingia Wamisri Waarabu na Waislamu katika uwanja wa mashindano ya kielimu na kimaendeleo, kwani wanayo nguvu kubwa ya kiroho kiari watu na zenginezo katika mashariti ya kuendelea kwenye ulimwengu usio heshimu watu dhaifu wala wajinga.

Msingi wa nne: Uhuru wa ubunifu wa kifasihi na kisanaa.

Ubunifu unagawanyika katika ubunifu wa kielimu unaofungamana na utafiti wa kielimu kama tulivyoelezea, ubunifu wa kifasihi na kisanaa ni sehemu ya aina ya fasihi mbali mbali kama vile za kishairi nyimbo michezo ya kuigiza visa na riwaya, sanaa ya uchongaji na sanaa ya sinema na muziki, na aina zengine za kisasa katika aina zote hizi.

Fasihi na sanaa kwa ujumla wake vinalenga kukuza muamko wa uelewa, na kuamsha mawazo, kuinua hisia za uzuri kusafisha hisia za mwanadamu kupanua uelewa wake kuongeza uzoefu wa mwanadamu wa maisha na jamii, kama vile fasihi na sanaa vinafanya kazi ya kukosoa jamii wakati mwengine kutoa yale yaliyo mazuri zaidi, yote hayo ni kazi ya thamani inayopelekea kuinua viwango vya lugha utamaduni kuchangamsha mawazo na kukuza fikra, pamoja na kuchunga misingi mikuu ya kidini na maadili bora.

Lugha ya Kiarabu imechukuwa sifa pekee kutokana utajili wake wa kifasihi na fasaha yake inayoshuhudiwa, mpaka qurani tukufu imekuja kwa kiwango cha juu cha ufasaha na miujiza, ikaongeza uzuri wa lugha na kuonesha kipaji chake, na kulisha sanaa ya ushairi na lugha isiyo ya kishairi na hekima, vikaanza kuonekana vipaji vya washairi na waandishi – kwa watu wote ambao umewafika Uislamu na kuongea lugha ya Kiarabu – wanabuni katika sanaa zote kwa uhuru mkubwa ndani ya kipindi kirefu pasi ya matatizo yeyote, isipokuwa wanawachuoni wengi wanao jihusisha na utamaduni wa Kiarabu na Kiislamu kuanzia masheikh maimamu, wamekuwa ni waandishi wa mashairi visa kwa aina zake zote, kanuni kuu ambayo inasimamia mipaka ya uhuru wa ubunifu ni kukubali jamii kwa upande mmoja na uwezo wake wa kuelewa urithi na ubunifu mpya wa kifasihi na kisanaa kwa upande mwengine, na kutojiingiza uhuru huo katika yale yanayogusa hisia za kidini na misingi ya kimaadili iliyopo, ubunifu wa kifasihi na kisanaa utaendelea kuwa ni katika alama muhimu za kukuwa kwa mfumo wa misingi ya uhuru na kuwa na nguvu kubwa ya kuinua mwamko wa jamii na utajiri wa hisia zake, na kila unapojikita uhuru bora, hiyo inakuwa ni dalili ya maendeleo yake, fasihi na sanaa ni vioo vya dhamira ya jamii na kielelezo cha kweli cha mabadiliko yake, na inatoa sura inayoangaza matarajio yao ya maisha bora ya baadae. Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwezesha kwa yale yenye khier na malipo.

 

Imetolewa Makao Makuu ya Azhar:

                                                                                                                       Mwezi 14/mfungo tano/1433

                                                                                                                          Sawa na tarehe: 08/Jan/2012.

               Sheikh wa Azhar

        Ahmad Tayyib 

 

 

Tamka kuhusu ukamilishaji wa malengo ya mapinduzi

4- TAMKO LA AZHAR SHARIF

KUHUSU

KUKAMILISHA MALENGO YA MAPINDUZI YA MISRI NA KURUDISHA ROHO YAKE

Kwa pendekezo la kitaifa toka Azhar Sharif na kwa ushiriki nzuri wa baraza la mawaziri, kanisa la kitaifa la Misri, viongozi wa kiraia, na katika siku hii ya historia, sikuu ya kwanza ya mapinduzi ya Misri, mapinduzi ambayo yameibua hisia ulimwenguni kwa sifa zake ambazo hazijawahi tokea, na uhalisia wake wa kiusalama, shime yake ya kukutana pande za kitaifa kwa ajili ya Misri wake kwa waume, na kufahamu silaha za kisasa zaidi katika mapinduzi ya mawasiliano ya kimataifa, ili kufanikisha malengo yake ya kwanza ya mapinduzi, nayo ni: kuisafisha Misri na kipindi kilicho fahamika kwa ufisadi na udhaifu, unyonyaji na dhuluma, katika siku hii ya leo Misri yote inarudi sehemu hii ambayo imeshuhudiwa kuzaliwa kwa mapinduzi, na kushuhudiwa kujitoa muhanga kwa vijana wenye nia safi na nchi, katika wale waliotanguliza roho zao kwa ajili ya Misri, Misri inarudi – leo – katika “Uwanja wa Tahrir” ambao umeingia kwa herufi zake za Kiarabu kwenye lugha zote ulimwenguni, na kuathiri kwa roho yake ya kidemokrasia raia wengi mingoni mwa raia wa eneo la mashariki na magharibi.

Leo: Misri ya tahrir Misri ya bunge, Misri ya jeshi Misri ya raia, Misri ya serikali, Misri ya Azhar, Misri taifa na Misri ya Kiarabu, Misri ya Kiislamu Misri ya kikristo, Misri ya historia na urithi, Misri ya sasa na baadae, Misri yenye asili ya dini na Misri yenye uhuru kamili wa kiraia, leo Misri inaangalia ulimwengu wote kwa mtazamo wake wa kimapinduzi, ikitangaza wajibu huu wa kitaifa:

  1. Kuhifadhi roho ya uwanja huu wa Tahrir kama ilivyokuwa wakati wa siku kumi na nane ambazo zilibadilisha mapito ya historia ya Kimisri, na kuwakusanya wananchi wake wote kwenye tamko moja sawa.
  2. Ahadi ya kitaifa – kwa jina la misingi yote iliyopita – juu ya kukamilisha malengo ya mapinduzi ya tarehe ishirini na tano Januari.
  3. Makubaliano ya kitaifa juu ya kusimamia mambo ya nchi hii pasi ya kupendelea au kutawala au kutengwa kwa ajili ya watu fulani au kuegemea upande mmoja.
  4. Kuelezea wajibu wa mwananchi kikatiba ya kushitakiwa, na haki ya kuzuiliwa mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za wananchi wa kawaida, pamoja na kuachiwa huru wafungwa wote wa kisiasa.
  5. Kufanya haraka kufikishwa mahakamani wale wote ambao ni alama za ufisadi na uovu, ili isipotee haki hukumu ya uadilifu na ulazima wa kuwa wazi.
  6. Kukamilisha utekelezaji wa haki za familia za mashahidi na wale waliojeruhiwa katika mambo ya matibabu kulipwa fidia na kuangaliwa kikamilifu.
  7. Kuendelea na ujenzi wa demokrasia kwenye asasi za serikali na kukamilisha zoezi la kukabidhi serikali ya kiraia ndani ya wakati wake uliopangwa pasi ya kucheleweshwa.
  8. Kuwajibika na yale yaliyofikiwa na uchaguzi huru na wawazi miongoni mwa matokeo, na kushirikiana kati ya vijana wote wa mapinduzi na wawakilishi wa wananchi waliochaguliwa katika kazi za ujenzi wa mustakbali wa Misri chini ya mwanvuli wa demokrasia na msingi wa uhalali wa bunge na makubaliano ya kitaifa.
  9. Kupambana na athari za siasa za unyonyaji na ufisadi, pamoja na kufanya kazi katika kujenga uchumi wa Misri wenye nguvu unawekezwa na nguvu zote za Misri na kufikia hali ya uadilifu wa wananchi wote.
  10. Kurejesha duru ya taifa la Misri katika kuongoza ndani ya eneo, na kutoa mchango katika siasa za kimataifa kwa maamuzi huru yasiyofungamana na upande wowote.
  11. Kurejea kwa jeshi la taifa – lenye jukumu la mambo ya nchi na kulinda mapinduzi- katika duru yake ya ulinzi wa mipaka ya Misri na usalama wake.
  12. Kuachia nguvu ya wananchi na hasa vijana wa kimapinduzi kuinua ujenzi wa jamii na nchi. Na kupambana na kuchelewa kielimu ufakiri maradhi na ujinga, na kuiendeleza nchi kisiasa kiuchumi na kimaadili ili kuwa ni mfano wenye kuangaza katika Umma wa Waarabu na Waislamu.

 

Na Mwenyezi Mungu mbora wa mashahidi, nae ni toshelezo letu na mbora wa kutegemewa.

 

 

Imetolewa na Makao Makuu Azhar:

17 /mf: tano / 1433. H

11 / Januari / 2011. AB

 

                                                                                                                                               Ahmad Tayyib

Sheikh wa Azhar 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tamko kuhusu Qudusi Takatifu

 

5 – TAMKO LA QUDS TAKATIFU

 

Ndani ya wakati ambao kunafanyika haraka hatua za uingizaji Uyahudi na Uzayuni katika mji mtakatifu wa Jerusalem, na kuongezeka uadui wa Kizayuni katika maeneo matakatifu ya Kiislamu katika eneo la Jerusalem – ndani yake kuna msikiti wa Al-Aqsa Al-mubarak – na kukiendelea miradi ya kizayuni katika kutishia maeneo matakatifu, mwisho ni mradi wa treni ya quds - Azhar kibla ya elimu ya Kiislamu na kiunganishi kati ya maeneo ya Umma wa Kiislamu na wengine pamoja na mtetezi wa kadhia zao ima za kitaifa au za Kiislamu – inatamka yafuatayao:

 

La Kwanza:

Eneo la quds (Jerusalem) la Kiarabu kwa mujibu wa historia ndefu ya zaidi ya karne sitini… ambapo ilijengwa na Waarabu Wayebusi ndani ya kipindi cha miaka elfu nne kabla ya kristo… kwa maana ya kabla zama za baba wa Manabii, Nabii Ibrahim A.S. kwa karne ishirini na moja… na kabla ya kutokea uyahudi ambao ni sheria za Nabii Mussa A.S. kwa karne ishirini na saba.

La Pili:

Sheria ya Nabii Mussa A.S. na Taurati yake zilianza nchini Misri, ambapo lugha iliyokuwa ikitumika ni lugha ya hieroglifu, kabla ya kuingia wana wa Israel kuvamia ardhi za Kanaan, na kabla ya kuenea kwa lugha ya Kiebrania kwa zaidi ya miaka mia moja. Kwa hivyo basi hakuna uhusiano kwa uyahudi wala kiebrania kwa eneo la Quds (Jerusalem) wala Palestina.

La Tatu:

  Kuwepo kwa Waebrania katika mji wa quds (Jerusalem) hakuvuki zaidi ya miaka 415 baada ya hapo, katika zama za Nabii Daud na Nabii Suleiman A.S. ndani ya karne ya kumi BC (kabla ya kristo)… nao uwepo wao ni wadharura na wakupita njia, yalitokea hayo baada ya kuanzishwa mji wa Jerusalem wa Kiarabu na kupita karne thelathini.

La Nne:

  Historia ya Quds imeshuhudiwa kutokea kwa mapigano mengi pamoja na uvamizi, mazingatio ya historia siku zote yanaonesha kuwa wavamizi walifanya ukiritimba katika mji huu na kuufanya wao pasi ya wengine… walifanya hivyo Wababeli… Wagiriki… Waroma… vilevile watu wa msalaba… kisha Wazayuni ambao wanafuata njia za hawa wavamizi, na wanafanya – hivi sasa - kazi ya kupageuza kuwa ni sehemu ya kiyahudi na kupamiliki, na kumaliza athari ya uwepo wa Waarabu ndani ya mji huo.

Wavamizi wamefanya hivyo, wakati ambapo Uislamu pekee ambao umekuwa na sifa ya kutambua sheria zote na madhehebu, kuheshimu maeneo matakatifu, na kwa aina ya pekee Uislamu umeelezea utakatifu wa mji huu wa Jerusalem na kueneza maelezo hayo kwa watu wote wa dini na madhehebu… jambao ambalo limefanya – na linafanya – mamlaka ya Kiarabu katika eneo la Quds (Jerusalem) kuwa na dhamana kwa masilahi ya wote, eneo la Quds katika utawala wa Kiarabu – siku zote – ni mji wa Mungu, milango yake ipo wazi kwa viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu na waja wake.

La Tano:

  Kujimilikisha eneo la Quds na kulifanya la kiyahudi – katika ushambuliaji wa hivi sasa – hakika kuna kwenda kinyume na makubaliano na sheria za kimataifa ambazo zinazuia na kufanya kitendo hicho kuwa ni uhalifu, kufanyika mabadiliko yeyote ya asili ya ardhi na makazi ya watu katika ardhi zinazokaliwa kimabavu, na kutokana na hilo kugeuza eneo la Jerusalem na kulifanya la kiyahudi limekosa uhalali wa kisheria, kuongezea pia juu ya mgongano wake wa ukweli wa historia ambayo inatangaza kuwa eneo la Quds (Jerusalem) kuwa ni la Kiarabu tokea lilipojengwa na Waarabu wa Wayebusi kabla ya zaidi ya karne sitini.

 

 

 

 

La Sita:

Hakika ya Azhar Sharif – na wale waliokuwa nyuma yake Waislamu wote eneo la mashariki na magharibi, wanapinga mradi huu, na kutoa tahadhari kwa wazayuni na pande ambazo zinasaidia wazayuni juu ya matatizo ambayo yanatishia amani ya eneo hili lakini na ulimwengu wote, na inawakumbusha wazayuni – na wale walio nyuma yao - kuwa: watu wa msalaba wameshikilia kimabavu maeneo mengi zaidi kuliko yale yaliyoshikiliwa kwa nguvu na wazayuni… na eneo la Quds “Jerusalem” limekuwa mikononi mwa familia za kimsalaba kwa miaka mingi inazidi zaidi ya miaka ambayo imekuwa mikononi mwa wazayuni waovu… pamoja na hayo, imepita kawaida ya historia – ambayo haiendi kinyume -  kukunja ukurasa wa ukaliaji wa kimabavu,  na kuondoa athari za uadui wenye kufanya uadui dhidi ya haki na maeneo matakatifu.

Wazayuni – ambao wanategemea nguvu za ubeberu wa wakibabe na wakinyama wa kimagharibi, katika majaribio yao ya kuingiza uyahudi eneo la Jerusalem Quds takatifu – kwa hakika wanahatarisha wao wenyewe mustakabali wa wayahudi, na wanavuka msitari mwekundu wa Umma wa Kiislamu, ambao unafikia idadi yake kiasi cha robo ya watu duniani, nao ni Umma wenye uwezo – ndani ya siku ya karibuni – kurudisha haki yake iliyochukuliwa.

Eneo la Quds sio eneo linalokaliwa kimabavu tu, lakini lenyewe –kabla ya hapo na baada ya hapo – ni sehemu takatifu kwa Waislamu na wakristo… na kadhia yake sio –tu – kadhia ya Kipalestina, au kadhia ya Umma wa Kiarabu, isipokuwa yenyewe ni – zaidi ya hivyo – ni kadhia ya imani ya Kiislamu, na Waislamu wapo katika jihadi ya kuikomboa quds (Jerusalem) toka kwa waporaji wa kizayuni, wakilenga kuthibitisha utakatifu wake, na inapaswa kuhamasisha hilo kwa kila watu wenye maeneo matakatifu ili wamalizane na ukiritimba wa kiisraeli na kuingiza uyahudi wa kizayuni.

Azhar Sharif inatoa wito kwa kila watu huru duniani kutetea haki ya Waarabu katika kukomboa Quds na Palestina… kama vile inatoa wito kwa wasomi wenyewe wa kiyahudi kuzingatia historia, ambayo imeonesha juu ya mateso yao kila sehemu walipoingia isipokuwa walipoingia katika maeneo ya Kiislamu na ustaarabu wa Waislamu.

Na inasisitiza Azhar – kwa mara nyingine - kuwa kitendo cha kuifanya Quds kuwa ya kiyahudi na kuendeleza uadui katika maeneo matukufu ya Quds Sharif, hilo ni msitari mwekundu, na wakati huo huo ni utangulizi wa kuingiza dola ya kizayuni katika ardhi za Palestina.

Kiongozi Salah Al-ddini Al-Ayyuby alishatangulia kuweka njia ya ukombozi wa Quds Al-Sharif, pale alipo mwandikia mfalme wa watu wa msalaba Richard moyo wa simba, na kumwambia: “usije fikiria kuwa inawezekana kwetu sisi kuachana na Quds hata siku moja, kama vile haiwezekani kwa hali yeyote kuachana na haki zetu za eneo hilo tukiwa kama Umma wa Kiislamu… na Mwenyezi Mungu hatokuwezesheni kujenga hata jiwe moja tu katika ardhi hii wakati wote wa jihadi inapoendelea”

Na kwa hakika historia imesema kweli juu ya maneno ya mtetezi Salah Al-dini, na yafahamika kwa kila mwenye akili kuwa, katika historia kuna utaratibu wa Mungu usiokuwa na mbadala wala kubadilika.

(Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui) Yusouf: 21.

(Na watajua wale ambao wamedhulumu ni mgeuko gani watakao geuka) Al-shuaraa: 227.   

 

      Imetolewa Makao Makuu Azhar

     24/Mf: tatu/1432. H

       20/Nov/2011. AB

 

                                                                                                                                               Ahmad Tayyib

Sheikh wa Azhar 

Print
10333 Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.