Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Ujumbe wa Uokozi wa Al-Azhar Wafika Kambi za Warohinga Nchini Bangladesh kabla ya Kuanza Kugawa Misaada hapo kesho Jumatano
Anonym
/ Categories: Main_Category

Ujumbe wa Uokozi wa Al-Azhar Wafika Kambi za Warohinga Nchini Bangladesh kabla ya Kuanza Kugawa Misaada hapo kesho Jumatano

Ujumbe wa uokozi uliopelekwa na Al-Azhar Al-Sharif nchini Bangladesh, leo jumanne umefika kwenye kambi za Waislamu wa kabila la Warohinga katika mji wa Cox Bazaar uliopo mpakani na Myanmar, ikiwa ni maandalizi ya hapo kesho jumatano kuanza ugawaji wa misaada ya uokozi na vifaa vya malazi vilivyotumwa na Al-Azhar Al-Sharif.

Misaada hii inakuja ikiwa ni katika wigo wa usaidizi wa kibinadamu, kiari na kiuokozi ambao unatolewa na Al-Azhar Al-Sharif pamoja na Baraza la Wazee Waislamu kwa Waislamu wa kabila la Warohinga, ambapo hivi karibuni kutafuatia ziara ya Imamu Mkuu ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Al-Azhar na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Waislamu Prof. Ahmad Al-Tayyib wiki ijayo kutembelea kambi za wakimbizi wa Kirohinga huko Bangladesh.

Ujumbe wa Al-Azhar ulitembelea sehemu iliyoandaliwa kugawa misaada, ambapo maelfu ya mabox ya vyakula na mablanketi vitatolewa ikiwa kama ni hatua ya kwanza, ikimalizikia hatua ya pili ambayo itakusanya misaada ya chakula, tiba na vifaa vya malazi, inayotolewa na Baraza la Wazee Waislamu, ambapo mji wa Cox Bazaar unakumbwa na hali ya kujaa kwa kambi za wakimbizi, ambapo mji huo unapokea maelfu ya wakimbizi ambao wanaishi kwenye makambi wakiwa na hali ngumu kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya hali ya hewa.

Print
4868 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.