Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Kuanza Kazi za Ugawaji Misaada Inayotolewa na Al-Azhar Al-Sharif kwa Wakimbizi wa Kabila la Rohinga Nchini Bangladesh
Anonym
/ Categories: Main_Category

Kuanza Kazi za Ugawaji Misaada Inayotolewa na Al-Azhar Al-Sharif kwa Wakimbizi wa Kabila la Rohinga Nchini Bangladesh

Ujumbe wa Al-Azhar Al-Sharif uliotumwa nchini Bangladesh leo siku ya jumatano umeanza kazi za ugawaji wa misaada ya uokozi na vifaa vya malazi kwa Waislamu wa kabila la Rohinga wanaopatikana katika mji wa Cox Bazaar nchini Bangladesh.

Kazi hiyo ya ugawaji misaada ambayo inabeba alama ya Al-Azhar Al-Sharif pamoja na bendera ya Misri, itaendelea kwa muda wa siku tano, sambamba na ujumbe huo wa Al-Azhar kuzungukia ndani ya kambi ya wakimbizi ili kuwapa moyo pamoja na kutoa msaada wa kiimani kwa wananchi hao wa Kirohinga, ambao ripoti ya Umoja wa Mataifa imewaelezea kuwa ni kundi lenye kukosa haki pamoja na kupata mateso zaidi duniani.

Panatarajiwa Imamu Mkuu na Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharif pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Waislamu Prof. Ahmad Al-Tayyib wiki ijayo kufanya ziara akifuatana na ujumbe wa wanachuoni wa Al-Azhar na wajumbe wa Baraza la Wazee kutembelea kambi ya Waislamu wa kabila la Warohinga nchini Bangladesh, ili kuangalia hali ya wakimbizi hao, na huko atatoa ujumbe kwa jamii ya kimataifa na dhamiri ya kimataifa kuhusiana na matatizo ya Warohinga.

Imamu Mkuu alikuwa ametoa maelekezo ya kutolewa kwa misaada ya haraka ya kiafya kutoka Al-Azhar Al-Sharif na Baraza la Wazee Waislamu ili kuwapunguzia matatizo mamia ya maelfu ya Waislamu wa Rohinga ambao wamelazimishwa kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh wakikimbia mbinyo na ukandamizi ndani ya nchi yao ya Myanmar.  

Print
4860 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.