Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Siku ya pili ya Ugawaji Misaada kwa Waislamu wa Kabila la Warohinga… Imamu Mkuu Atoa Maelekezo kwa Ujumbe wa Al-Azhar Kugawa Misaada hiyo wao wenyewe.
Anonym
/ Categories: Main_Category

Siku ya pili ya Ugawaji Misaada kwa Waislamu wa Kabila la Warohinga… Imamu Mkuu Atoa Maelekezo kwa Ujumbe wa Al-Azhar Kugawa Misaada hiyo wao wenyewe.

Ujumbe wa misaada na uokozi wa Al-Azhar Al-Sharif huko nchini Bangladesh, kwa siku ya tano unaendelea kugawa misaada kwa Waislamu wa Warohingya wanaopatikana katika mji wa Cox Bazaar uliopo mpakani na nchi ya Burma.

Ujumbe huo umejigawa makundi matatu ambapo kila kundi moja linahudumia kambi moja, kwa lengo la kufikia idadi kubwa ya wakimbizi, kazi hiyo inafanyika kwa ushirikiano mkubwa na serikali ya Bangladesh, ambayo inasimamia kwa mujibu wa utaratibu wa hisa ya chakula ili kudhamini msaada huo kufika kwa walengwa kwa usawa na kudumu.

Imamu Mkuu Profesa Ahmad Al-Tayyib ametoa maelekezo kwa wajumbe wa ujumbe huo wa Al-Azhar kugawa misaada hiyo wao wenyewe na kuwepo siku zote ndani ya kambi hizo, akisisitiza kuwa msaada wa kiari, mawasiliano ya kibinadamu pamoja na undugu wa kibinadamu.. vyote hivyo vina umuhmu zaidi kuliko misaada ya vitu.

Kama vile Imamu Mkuu ametoa umuhimu wa kushiriki kwa wasichana wa Al-Azhar katika jumla ya ujumbe huo ili kusisitiza ushirikiano wa ujumbe wa kibinadamu ambao unabebwa na Taasisi kubwa ya Kiislamu Duniani kwa ndugu zao Warohingya.

Ugawaji huu wa misaada unaendelea kwa muda wa siku tano, na kumalizikia na ugawaji wa misaada ya kibanadamu na ya kitiba inayotolewa na Baraza la Wazee Waislamu kwa maelekezo ya Imamu Mkuu pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo.    

Print
4935 Rate this article:
2.0

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.