Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Tamko la Imamu Mkuu Profesa Ahmad Al-Tayyib kwa Raia wa Misri baada ya Kutokea Shambulio la Kigaidi huko Sinai Leo Siku ya Ijumaa
Anonym
/ Categories: Main_Category

Tamko la Imamu Mkuu Profesa Ahmad Al-Tayyib kwa Raia wa Misri baada ya Kutokea Shambulio la Kigaidi huko Sinai Leo Siku ya Ijumaa

  • Al-Azhar kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa uimara wa raia wa Misri imeendelea kuzifedhehesha na kuzipasua fikra potofu.
  • Misri ni yenye kuangaliwa ina uwezo wa kuwafuta kabisa wafuasi wa magaidi na kupambana na makundi ya wajinga.

Al-Azhar inatoa pole kwa mashahidi wetu waiso na hatia, ambao wamefariki hii leo hali ya kuwa wakiwa wanatekeleza ibada ya Sala ya ijumaa katika msikiti wa Raudha huko Arish, baada ya kustukizwa na makundi ya waharibifu, wauaji na wamwagaji damu na kuwashushia mvua ya risasi na makombora, na sisi bado tunaendelea kusisitiza kwa wananchi wa Misri wote kuwa shambulio hili ambalo limelenga Waumini wenye kusali si vyengine isipokuwa ukweli ni linalenga nchi yenu, maisha yenu, azma yenu na msimamo wenu wa kuishi katika utulivu na mani.

Kama vile tunasisitiza kuwa vitendo hivi viovu haviakisi dini, maadili wala nguvu kwa watendaji wake zaidi ya kuakisi uritadi katika dini, kukata tamaa na kushindwa ndani ya nafsi zao.

Yanayotokea leo yanasisitiza yale tuliyoyasema na tunarudia tena leo kusema kuwa ugaidi usionekana mwovu hakika kwa hatua ya kwanza unakusudia nchi ya Misri, raia wake, misikiti yake, makanisa yake, jeshi lake jasiri na mashujaa wana usalama, lakini Misri ni yenye kuangaliwa ambayo haijawahi na wala haitawahi kushindwa, ni yenye uwezo kwa msaada wa Mwenyezi Mungu wa kuwamaliza wafuasi wa ugaidi na kupambana na makundi ya wajinga, walinganiaji wa ukafiri na wapumbavu.

Na ijapokuwa majeruhi wetu ni wenye thamani kubwa na majonzi yetu ni makubwa lakini hata hivyo sisi tunaamini hukumu ya Mwenyezi Mungu, uwezo wake na kauli yake [Na msilegee, wala msihuzunike, kwani ninyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini]{Aal-Imran,139}.

Wito wetu kwa Umma wa Kiarabu na wa Kiislamu na wale wakweli na wenye dhamira ya kupambana na ugaidi na kuuzingira, kusimama na Misri bega kwa bega, mkono kwa mkono na wala wasiiache katika kupambana na huu ugaidi mbaya wa kimataifa.

Na watu huru duniani Mashariki na Magharibi wafanye haraka kuwagundua wale wanaosimama nyuma ya huu ugaidi na kuwanyooshea mkono wa fedha na silaha pamoja na kuwakamilishia makazi na ulinzi.

Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa uimara wa raia wa Misri Al-Azhar itasonga mbele katika kufedhehesha fikra hizi zilizopotea zenye kupoteza na kuzipasua pasua pamoja na kuzichana, na kuwalinda vijana wa Umma wa Kiislamu kuingia kwenye mtandao wa fikra hizi na makucha yake, juhudi hizi za udanganyifu na uwongo pamoja na watu wake, hazitazuia utekelezaji wa ujumbe wa Al-Azhar ambao unautekeleza kwa zaidi ya miaka elfu.

Print
5955 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.