Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Hotuba ya IMAM MKUU  Prof. Ahmad Al-Tayyib  Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif
Anonym
/ Categories: Main_Category

Hotuba ya IMAM MKUU Prof. Ahmad Al-Tayyib Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif

 

 

 

Hotuba ya IMAM MKUU

Prof. Ahmad Al-Tayyib

Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif

 

Kuhusu:

 

 

MASHAHIDI WA MSIKITI WA Al-RAUDHA HUKO SINAI

 

Kwenye Kijiji cha Al-Raudha Mkoani Sinai

 

 

 

Iimetolewa: 12/Mfungo Sita/1439H

Sawa Na Tarehe: 01/December/2017.

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Sala za Mwenyezi Mungu na Salamu ziwe kwa Mtume wetu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, pamoja na watu wake na Masahaba wake.

Baada ya hayo:

Hakika utashi wa Mwenyezi Mungu ambapo hakuna awezaye kurudisha nyuma uamuzi wake umetaka kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume utanguliwe na tukio la maumivu makali katika nyoyo zetu, lenye huzuni kubwa kwenye nafsi zetu na hisia zetu… wala hatumiliki isipokuwa ni kusema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ni wenye kurejea … pamoja na yote hayo tunazikumbusha nafsi zetu na watu wetu wa mji huu mzuri, na kijiji cha watu wenye subira juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake na kadari yake kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Ni ajabu jambo la Muumini, hakika jambo lake lote ni heri kwake, na wala haliwi hilo isipokuwa kwa Muumini: ikiwa atapatwa na jambo la furaha hushuruku, basi inakuwa ni heri kwake, na ikiwa atapatwa na jambo lenye madhara husubiri, basi inakuwa ni heri kwake”.

Na wala hamna haja - enyi wenye subira - wakazi wa kijiji cha Al-Raudha ya kukumbushwa nafasi kubwa kwenye Pepo ya juu ya Firdausi ambapo wananeemeka humo mashahidi wenu miongoni mwa wazazi na watoto.. na wala msidhani kuwa hawa mashahidi wasio na hatia wamepata maumivu ya kifo kama vile wanavyopata watu wanaofariki, Mtume S.A.W. amesema: “Shahidi hapati maumivu ya kifo, isipokuwa ni kama mmoja wenu anavyopata maumivu ya kung’atwa na sisimizi”.. inatosha yale tuliyoelezwa na Sheria ya Kiislamu kuwa shahidi ni katika watu wenye daraja kubwa baada ya Mitume na wafuasi wa kweli wa Mtume.

Ama wauaji ambao wamefanya uadui kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwaga damu takatifu ndani ya nyumba katika nyumba zake Mwenyezi Mungu, basi hawa ni wakiukaji waovu na waharibifu katika ardhi, historia yao ya kuwaua Waislamu na kuwatisha watu wa amani inafahamika na imehifadhiwa.

 Mtume S.A.W. amewataja kwa sifa kupitia sifa hizo bado tunaendelea kuwafahamu, amewataja kwa sifa ya kuwa na umri mdogo (vijana) ikiwa ni ishara ya ukiukaji wao, uvamizi wao na ujinga wao, kisha akawataja kwa sifa ya ujinga wa akili na uelewa mbaya, na akatahadharisha na hisia zao potovu pamoja na wingi wa ibada zao, pamoja na kuhifadhi kwao Qurani Tukufu, usomaji wao wa Qurani katika yale ayasemayo Mtume S.A.W. hauvuki midomo yao kwenda nyoyoni mwao na akilini mwao, pia Mtume S.A.W. akawaelezea kwa sifa ya kuwa na siasa kali katika Dini na ni watu wa kufanya haraka kuwakufurisha Waislamu, ikiwa ni maandalizi yao ya kuwaua na kuzipora mali zao pamoja na kuharibu heshima zao, naye Mtume S.A.W. ameamrisha kuwaua na akaahidi kwa mwenye kuwaua atakuwa na malipo Siku ya Kiyama, imepokelewa katika Hadithi sahihi kauli yake Mtume S.A.W.: “Watatokea watu zama za mwisho, wenye umri mdogo, wenye akili dhaifu, wanasema kauli za wema wa viumbe, wanasoma Qurani haivuki kooni mwao, wanaritadi kama mshale unavyochoma wakati unaporushwa, basi popote muwakutapo waueni, kwani katika kuwaua kuna malipo kwa mwenye kuwaua Siku ya Kiyama([1]).

Mwenyezi Mungu Amebainisha malipo yao ndani ya Qurani Takatifu katika Aya ambayo tunaihifadhi sisi sote: (Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusulubiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchini. Hiyo ni fedheha kwao Duniani, na Akhera watapata adhabu kubwa){Al-maaida, 33}.

Kutokana na hayo ni lazima kwa wasimamizi wa mambo ya nchi kufanya haraka kutekeleza hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwaua hawa wanaopigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya juhudu za kueneza uharibifu kwenye ardhi, lengo ni kulinda roho za watu, mali zao na heshima zao..

Na kwa watu wa Sinai, sehemu hii ni takatifu katika ardhi za Misri, na ndio ambao wanapatwa na matatizo mengi ya huu ugaidi kuliko watu wengine, bali ni juu ya wananchi wote wa Misri na Asasi zote za Dola kubeba jukumu na kupambana vilivyo katika vita hivi vikali, huu ni ugonjwa hatari wa kansa, na Misri - kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu - na kwa historia yake, kwa nguvu za wananchi wake na ushujaa wa jeshi lake pamoja na watu wake majasiri wa usalama - ni yenye uwezo wa kuivuka hatua hii ngumu na kumaliza kabisa huu ugaidi mgeni katika ardhi zetu na vijana wetu kwa muundo wake, agenda, fikra na imani.

Na mwisho wa hotuba yangu ninawaambia watu wa kijiji hiki kizuri kuwa: hakika ya uwepo wetu hapa ni kuwahakikishia kuwa Misri yote inahisi kwa kile mnachokihisi, inapata maumivu vile mpatavyo maumivu, na vile vile Al-Azhar imekuja na Masheikh wake pamoja na watoto wake ili kuwapa pole na kuwapunguzieni machungu ya majeruhi wenu, pamoja na kuweka mkono wake kwenye mikono yenu kwa ajili ya maendeleo ya kielimu, kiafya na kijamii kwa kijiji hiki … pamoja na uyakini wangu kuwa dunia yote haiwezi kufidia tone moja la damu lililomwagika kutoka katika nafsi hizi safi, lakini inaweza kuwatekelezeeni baadhi ya haki zenu na kupata heshima ya kufanyika juhudi katika kuwahudumia.

Mwenyezi Mungu Awarehemu mashahidi wetu wasio na hatia, na Awahifadhi na kuihifadhi Misri kutokana na fitina, mitihani na shari.

 

AMANI YA MWENYEZI MUNGU IWE KWENU REHEMA ZAKE NA BARAKA ZAKE:

 

Iimetolewa: 12/mfungo sita/1439H.

Sawa na tarehe: 01/December/2017.

 

Prof. Ahmad Al-Tayyib

   Sheikh wa Al-Azhar

 


([1])  Ameipokea Bukhari (6930) na Muslimu (2667).

Print
6323 Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.