Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Imamu Mkuu: 2018 uwe ni mwaka wa uadilifu na kuvumiliana… na dawa ya maumivu kwa wagonjwa na watu wanyonge, akielezea matamanio yake ya kuwa mwaka wa heri na amani…
Anonym
/ Categories: Main_Category

Imamu Mkuu: 2018 uwe ni mwaka wa uadilifu na kuvumiliana… na dawa ya maumivu kwa wagonjwa na watu wanyonge, akielezea matamanio yake ya kuwa mwaka wa heri na amani…

 

Imamu Mkuu Prof. Ahmad Al-Tayyib Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharif, Mwenyekiti pia wa Baraza la Wazee wa Kiislamu, ameelezea matamanio yake ya mwaka wa 2018 kuwa ni mwaka wa heri na amani kwa wanadamu wote, akitoa wito pande zote za Dunia juu ya umuhimu wa kufanya kazi ya kueneza utamaduni wa kusameheana na kuvumiliana pamoja na kuishi pamoja na kupambana na kila aina ya ubaguzi, misimamo mikali na ugaidi.

Imamu Mkuu akisisitiza kuwa, pamoja na kuanza mwaka huu mpya tunapaswa sisi sote kufanya kazi pamoja ya kueneza misingi ya uadilifu na usawa, pamoja na kushiriki sisi sote katika kutibu maumivu ya watu wanyonge, wagonjwa na wenye kudhulumiwa katika maeneo yote ya Dunia, na kueneza utamaduni wa mazungumzo kati ya wanajamii mbalimbali.

Imamu Mkuu akikazia kuwa, majaribio ya miaka iliyopita bali hata orodha ya historia ya zamani na sasa inasisitiza kuwa, amani na ustawi wa wanadamu ni mambo yasiyokubali kugawika, na pia ni muhali kuneemeka sehemu moja ya Ulimwengu kwa kuwa na ustawi na amani wakati sehemu nyengine ya Ulimwengu ikiwa inawaka moto wa machafuko na kukosa maendeleo, jambo ambalo linahitaji kwa jamii ya Kimataifa na pande zenye nguvu ya utendaji kuchukua hatua za makusudi kwa ajili ya kuutengeneza ulimwengu usio na njaa, umasikini, kutengwa na kubaguliwa, njaa ndani ya Bara la Afrika, ukandamizaji na mateso huko Burma, ukaliaji wa kimabavu kwenye ardhi za Wapalestina na jaribio la kuchukua haki za wananchi wa Kipalestina pamoja na kupora maeneo yao matakatifu, yote hayo ni masuala muhimu unapaswa ulimwengu kuyapa uzito mkubwa ndani ya mwaka huu mpya.

Imamu Mkuu anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuufanya mwaka huu mpya kuwa ni mwaka wa kazi, kutoa, kufanya jitihada na juhudi kwa lengo la uboreshaji na maendeleo ya Misri yetu pendwa na Ulimwengu wetu wa Kiarabu na Kiislamu, na tufanye kazi pamoja kwa ajili ya maboresho na maendeleo ya Ulimwengu wetu unaotuzunguka kwa yale yatakayo rejesha amani usalama ustawi na mustakabali bora kwa watu wote.       

Print
4810 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.