Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

Imamu Mkuu alaani shambulizi dhidi ya Kanisa huko Helwan… atoa wito kwa Waislamu kushiriki na ndugu zao Coptic katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa Kristo amani iwe kwake.
Anonym
/ Categories: Main_Category

Imamu Mkuu Prof. Ahmad Al-Tayyib Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharif amelaani kwa maneno makali shambulizi la kigaidi ambalo limefanyika leo wakati wa Adhuhuri ambalo limelenga kanisa la Marmina huko Helwan, na kupelekea vifo vya watu kadhaa na wengine wamejeruhiwa, miongoni mwa askari polisi na Waumini wa Coptic. 

Akisisitiza Imamu Mkuu kuwa kurudia mashambulizi ya kigaidi ambayo yanalenga ndugu zetu wa Coptic ndani ya masiku ya sikukuu malengo yamekuwa yenye kuonekana yanalenga taifa na umoja wake zaidi ya vile yanavyolenga wafuasi wa Dini hii, hivyo basi hakika jibu kali kwao ni kufelisha malengo yao, pamoja na kushikamana zaidi na roho ya upendo ambayo inawakusanya Waislamu na Wakristo.

Imamu Mkuu anatoa wito pia kwa raia wote wa Misri kupambana na mkakati huu mchafu, na kuyafanya masiku haya mazuri kuwa ni fursa ya kuthibitisha hilo, kupitia ushiriki wa Waislamu kwa ndugu zao wa Coptic kwenye maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa kwa Kristo amani iwe kwake.

Imamu Mkuu anatoa mkono wa pole kwa familia za wahanga, akimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa moyo wa subra, na waliojeruhiwa kupona haraka iwezekanavyo.      

Print
5583 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.