Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Hotuba ya Imamu Mkuu Prof. Ahmad At-Tayyib  Sheikh Mkuu wa Al-Azhar  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Waislamu      Mkutanao wa Kimataifa wa Al-Azhar kwa ajili ya Utetezi Jerusalem
Anonym
/ Categories: Main_Category

Hotuba ya Imamu Mkuu Prof. Ahmad At-Tayyib Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Waislamu Mkutanao wa Kimataifa wa Al-Azhar kwa ajili ya Utetezi Jerusalem

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

 

Hotuba ya Imamu Mkuu Prof. Ahmad At-Tayyib

Sheikh Mkuu wa Al-Azhar

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Waislamu

 

 

Mkutanao wa Kimataifa wa Al-Azhar kwa ajili ya Utetezi Jerusalem

Unaofanyika Kituo Kikuu cha Mikutano cha Al-Azhar

Nasr City- Jijini Kairo

 

 

Ndani ya kipindi cha: 29 Mfungo Saba – 01 Mfungo Nane mwaka 1439H.

                      Sawa na tarehe: 17 – 18 Januari 2018 A.D.

 

 

 

 

 

Namshukuru Mwenyezi Mungu, Sala na Salamu ziwe kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na watu wake, Masahaba wake, na wale wote wenyekupita kwenye njia yake.

Mhe. Rais Mahmoud Abbas – Rais wa Mamlaka ya Palestina!

Wahe. kwenye jukwaa kuu!

Mabibi na Mabwana!

Wageni Mliohudhuria!

 

Amani iwe kwenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake… Karibuni sana waheshimiwa kwenye nchi yenu ya Misri, na katika uwanja wa Al-Azhar Al-Sharif, tunawashukuru sana kwa kuhudhuria kwenu na ushiriki wenu kwenye mkutano huu mkuu wa Kimataifa, ni mkutano wa: utetezi wa Jerusalemu Takatifu, na Msikiti wa Aqsa, ni kibla cha kwanza na sehemu takatifu ya tatu, na ni sehemu aliyopelekwa usiku Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad S.A.W… mkutano huu ambao unafanyika chini ya ulezi na usimamizi wa Mhe. Rais Abdulfattah Sisi - Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, ambaye anasimamia na kuchunga - pamoja nchi ya Misri na wananchi wake - kadhia ya Palestina, na hasa yale yaliyotokea hivi karibuni ikiwa ni pamoja na vikwazo vya siasa zisizofaa na maamuzi yasiyotekelezeka… basi kwa heshima yake na viongozi wa Kiarabu na Waislamu, na kwa kila watu wenye heshima duniani, wenye kuipa umuhimu kadhia ya Palestina, wananchi wake, maeneo yake matakatifu na ardhi zake kwa hivyo tunawaombea mafanikio, msimamo, nguvu na dhamira ambavyo haviji isipokuwa kwenye jambo la haki, uadilifu na usawa kwa watu wanyonge. Pongezi kwa Rais wa Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Palestina na tunamtakia kuwa na msimamo zaidi.

Mabibi na Mabwana

Tokea mwezi April mwaka 1948 ndani ya karne iliyopita, Al-Azhar Al-Sharif inafanya mikutano kuhusu Palestina na Msikiti wa Aqsa pamoja na maeneo matakatifu ya Kikristo huku Jerusalem, iliendelea mikutano hii na kufikia mikutano kumi na moja kati ya mwaka wa 1948 na 1988, na ilishirikisha jopo la wanachuoni, wana nadharia Waislamu, Wakristo toka Barani Afrika, Asia na Ulaya, na kufanyika tafiti za kina sana na kuwa kama pumzi ya mgonjwa ambaye hajabakiwa isipokuwa ni kama vijipumzi vinavyofanana na pumzi za mgonjwa ambaye amekosa dawa na dawa zikamkimbia.

Mikutano hii kila mara ilikuwa inaelezea kupinga uadui wa Wazayuni dhidi ya maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo pamoja ukaliaji wa kimabavu wa Msikiti wa Aqsa kisha uzushi na ukiukaji wa matakatifu yake kwa kuchimba mashimo, mahandaki na machinjio katika eneo la Msikiti, pamoja na kupora athari za Kikristo na kuzibomoa, ikiwa ni pamoja na Makanisa, majengo ya maaskofu, mafikio yao na makaburi huko Jerusalem Tiberia, jaffa na maeneo mengine([1]).

Na leo Al-Azhar inafanya tena mkutano wa kumi na mpili baada ya miaka thelathini toka mkutano wa mwisho kufanyika kuhusu kadhia ya Palestina na maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo… mkutano wetu wa leo pamoja na utajiri wake huu mkubwa kwa akili hizi zenye mwanga na dhamira iliyoamka toka Mashariki na Magharibi, huenda usitarajiwe kuongoza upya katika yale ya nyuma na yaliyoandikwa huko nyuma kuhusu “kadhia yetu” na yanayofungamana na mitazamo yake ya kielimu, kihistoria na kisiasa, lakini sawa na mkutano huu ambao unagonga - tena upya - alamu ya hatari, na kuwasha mwenge wa dhamira na msimamo ambao huenda ulishazimwa, kukutana kwa Waarabu, Waislamu, Wakristo, wasomi wa ulimwengu na watu wake maarufu - juu ya umuhimu wa kusimama imara dhidi ya upuuzi wa Kizayuni wa kijinga ndani ya karne ya ishirini na moja, upuuzi ambao unaungwa mkono na siasa za kimataifa, na amri zake kutikisa pale inapofikiria kutekeleza kile kinachopangwa na jamii hii ya Kizayuni pamoja na siasa za Kizayuni, ambayo nina imani thabiti kabisa kama wanavyosema wanachuoni wa elimu ya Tauhiid kuwa kila ukaliaji wa kimabavu ni wenye kuondoka hata kama utaonekana leo kuwa ni jambo lisilowezekana isipokuwa masiku ni yenye kuzunguka, na mwisho wa mporaji ni wenye kufahamika, mwisho pia wa mwenye kudhulumu hata kama utasubiribwa kwa muda mrefu lakini hakika unafahamika… ulizeni historia ya Roma eneo la Mashariki, ulizeni Fursi kuhusu historia yao Mashariki mwa ghuba ya Waarabu, ulizeni kampeni za msalaba ambazo zilikuwa na sehemu nzuri ndani ya Palestina kwa kipindi cha miaka mia moja, ulizeni nchi ambazo zilizojifaharisha kuwa jua haliwezi kuzama kwenye koloni zao, ulizeni ukoloni wa Ulaya nao unabeba fimbo ukiondoka Moroko, Algeria, Tunisia, Misri Shamu, Iraq, India, Indonesia na Somalia… waulizeni wote hawa ili mpate kufahamu - tena upya -  kuwa kuondoka ndio mwisho wa kila mwenye kufanya uadui, na kila nguvu zenye kutawala kimabavu - katika yale anayosema Ibn Khaldon - ni zenye kuhukumiwa kufutika, amesama kweli mshairi wetu wa Kiarabu katika kauli yake: Masiku katika muda ni mtiririko - mazito huzaa kila ya ajabu, huu ni ukweli wa ulimwengu na mwenendo wa Mungu, na kutia shaka ndani yake “ni aibu kwa elimu, akili na nadharia”([2]).

Isipokuwa ukweli huu unakutana na ukweli mwengine unaotangulia na kuzingatiwa juu ya chimbuko lake, ninamaanisha kumiliki nguvu ambazo zinatishia uadui na kuvunja pua yake pamoja na kulazimisha kuangalia tena upya mambo yake, na kumfanya afikirie mara elfu moja kabla ya kutenda uovu wake na ukandamizaji wake, na Mwenyezi Mungu Anafahamu kuwa sisi - pamoja na hayo - walinganiaji wa amani, amani inayosimama kwa uadilifu na kuheshimiana, pamoja na kutekeleza haki ambazo hazikubali kuuzwa, kununuliwa wala kuharibiwa, amani isiyofahamu udhalilifu wala kugusa punje ya udongo wa nchi au matakatifu… amani inayosaidia nguvu ya elimu na mafunzo uchumi na  kutawala masoko, na kuwezesha kurejesha kibaba kwa vibaba viwili, kwa maana kuepusha mkono wowote unojaribu kugusa wananchi wake na ardhi zake.

Ikiwa hili limeandikwa kwetu ndani ya zama hizi kuishi na sisi adui mgeni asiyefahamu isipokuwa ni lugha ya nguvu, basi hatuna sababu yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya historia kubakisha pembezoni mwake wanyonge wenye kupiga magoti kudhalilika, na kwenye mikononi mwetu - lau tutaka - tuna kila aina ya nguvu na vyanzo vyake vya kifedha na watu…

Na mimi ni miongoni mwa wale wanaoamini kuwa jamii ya Wazayuni sio ambao waliotushinda mwaka wa 48 au 67 na miaka mingine kwenye vita na mivutano ya hapa na pale, lakini sisi ndio ambao tumetengeneza mazingira ya kushindwa kwetu kwa mikono yetu, na kwa makosa ya hesabu zetu na mitazamo yetu mifupi katika kukadiria na kukisia hatari, kushirikiana kwetu kwa utani na mchezo kwenye maeneo ya kuwa kweli. Na wala haiwi kwa umma uliojengwa uzalendo, kuparaganyika asili na kupenda kupambana na jamii inayopigana kwa misingi thabiti ya imani, chini ya bendera moja, kuongezea pia kutodondoka kwa bendera yao na kuvunjika kwa umoja wao, hakika Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu: [Walamsizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu]{Anfaal, 46}.

Ndugu Mliohudhuria

Hakika yangu ni mwenye mtazamo kamili kuwa maneno yangu haya huenda yasiongeze upya, na yenyewe bado yanatoka kwa uchungu na maumivu, na athari yake inalingana na athari iliyong’oa usikivu wetu na masikio yetu kwa kipindi cha miaka sabini sasa, ikiwa ni pamoja na hotuba za wanasiasa, wasomi, wana nadharia na wana habari, pasi na kubadilisha ukweli na uhalisia au kusimamisha matamanio ya kiwendawazimu yenye kung’ata na kumeza, au kuelezea juu ya damu iliyomwagika na wahanga, matatizo na machungu kwenye majela na ukamataji, wanaokutana nao wananchi wa Palestina na vijana wake wanawake na watoto kwenye upambanaji thabiti usio usio lainika, subira na dhamira isiyo na udhaaifu ndani yake.

Ndiyo! Huenda pakasemwa mfano wa hayo katika hotuba yangu hii au kwenye huu mkutano wetu, lakini sidhani kuwa mtatofautiana nami kuwa, mkutano wa leo una tofauti sana na ile iliyotangulia, kwa sababu wenyewe huu unafanyika kwenye hali na msuguano unaofanana na mawingu yenye kiza ambayo yanaashira ujio wa mafuriko, adui alianza kuligawa eneo na kulifanya vipande vipande, na jamii ya Kizayuni kuweka masharti kwa eneo lote na kuamrisha kwa amri yake, hakuna kinachoonekana isipokuwa kile kinachoonekana na yeye na kusisimamiwa pia na yeye, eneo husika halina la kufanya isipokuwa ni usikivu na utiifu, na mtazamo wa yale yanayopangwa kwenye eneo la fukwe za bahari ya Atlas, na maingilio ya bahari ya shamu “Nyekundu” na fukwe za bahari ya Kati, na kuendelezwa kwa mipango hiyo huko nchini Yemen Iraq na Syria - ni muhimu kuelezewa kuwa mambo ni makubwa, na kurudiarudia ujumbe ule ule sio sahihi kulingana na kiwango cha vitimbi ambavyo vinafanywa kwetu, na sisi lau tutakabiliana nayo vile tulivyozoea kukabilana nayo tokea miongo saba iliyopita, basi vizazi vijavyo vitatulaani, wajukuu wetu wataona aibu sisi kuwa baba zao na babu zao, ikiwa mimi ninamatumaini ya kusubiri ukweli unaotokana na mkutano wetu huu wa leo, mwisho kuibuka kwa matokeo yake ya kiutendaji zaidi ambayo si ya kawaida, tutatumia uwezo wetu na kuandaa mfumo hata kama utakuwa mdogo kiasi gani au kuonesha kuwa hauna uzito mkubwa….

Jambo la kwanza na muhimu ni: kurudisha mwamko juu ya kadhia ya Palestina kwa ujumla wake na kadhia ya Jerusalemu kwa sifa maalumu, ukweli wenye uchungu ni kuwa mitaala ya masomo katika mifumo yetu ya kielimu na malezi katika kila hatua ya kielimu inashindwa kuunda uwezo wowote ule wa mwamko na utambuzi kwenye kadhia hii ndani ya akili ya mamilioni ya vijana wa Kiarabu na Waislamu, wala hakuna mtaala hata mmoja unaohusisha somo la kufahamu umuhimu wa kadhia hii, na historia yake hali yake ya sasa na athari zake kwa mustakabali wa vijana wetu, ambao watapokea bendera ya kulinda na kutetea Palestina, nao vijana wetu hawajawa karibu kuifahamu Palestina, kulinganisha na vijana wa wanaoishi kwenye makazi ya Kiyahudi ambao tokea udogo wao wamezoea mifumo, malezi, mitaala ya shule, nyimbo na sala, vikiwa vinajenga akilini mwao uadui… na kulishwa ubaguzi, na chuki dhidi ya kila Mwarabu na Mwislamu…  jambo ambalo sisi hatuna hilo kwenye mitaala yetu ya kielimu, tunakosa hayo pia hata kwenye vyombo vya habari mbalimbali, ndani ya ulimwengu wetu wa Kiarabu na Kiislamu, mazungumzo kuhusu Palestina na Jerusalemu yanakaribia kuvuka habari zote, au ripoti zinazopangiliwa na maripota wa habari, athari yake haidumu baada ya kwisha habari tu au mtangazaji anapoanza habari nyengine.

Na pendekezo la pili ni: maamuzi yanayoendelea ya Rais wa Marekani ambayo yamepingwa na zaidi ya nchi mia moja na ishirini na nane, na kupingwa na raia wote duniani wapenda amani, inapaswa kuangaliwa maamuzi hayo kwa fikra mpya ya Kiarabu na Kiislamu itakayojikita juu ya msisitizo na uthibitisho kuwa Jerusalemu ni ya Kiarabu, na heshima ya matakatifu ya Kiislamu na Kikristo, na kuwa ni yenye asili na wenyewe, na kubadilika kwa msisitizo huu na kuwa ni utamaduni wa ndani na kimataifa, na unafanyiwa kazi na vyombo vya habari vya Kiarabu na Kiislamu na zaidi ya hivyo, huo ndio uwanja uliotupelekea kushindwa na adui yetu kufanikiwa katika kuufanyia kazi.

Ni juu yetu kutosita katika kuiendea kadhia ya Jerusalemu kwa mtazamo wa kidini: uwe wa Kiislamu au wa Kikristo.

Katika mambo ya ajabu sana ni kuutenga upande wa kidini katika kuiweka karibu kadhia ya Palestina, wakati ambapo nyaraka zote za jamii ya Kizayuni ni nyaraka za kidini moja kwa moja na hawajaacha kuzisimamia, na wala hawazingatii ubaya wanaouonesha, kuna kitu gani mkononi mwa jamii hii ya Kizayuni ya kuwa na sababu ya kupora ardhi vitendo vinavyowapinga, bali vinawapingwa na baba zao pamoja na babu zao, pasi na wogo wala hofu ya maandiko ya kidini wakihalalisha uadui, na kuhalalisha damu za watu heshima zao na mali zao! Bali kuna nini kwenye mikono ya Wazayuni Wakristo wa hivi sasa ambao wanasimama nyuma ya jamii hii na kuilinda pamoja na kuwaaminisha na kila kile wanachokiota, zaidi ya tafasiri za Kidini za uongo zenye udanganyifu unaopingwa na Mababa wa Kanisa na wanachuoni wa Kikristo, Watawa wao na Makuhani wao na wanapinga kwa upingaji mkali.

Na pendekezo langu ambalo ninalileta kwenu waheshimiwa ili muweze kuliangalia na kuona yaliyo ndani yake, ni kuhusishwa na kutengwa mwaka huu wa 2018 kuwa ni mwaka wa Jerusalemu Takatifu, kutambulika, kusaidiwa kihali na kimali kwa watakasifu, na kufanywa harakati za kitamaduni na kihabari ni zenye kuendelezwa, zikifanywa na Jumuiya zilizo rasmi kama vile Umoja wa nchi za Kiarabu, Shirikisho la nchi za Kiislamu, Taasisi za Kidini, Umoja wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, na Jumuiya za kiraia na zenginezo.

Ninakamilisha hotuba yangu, ambayo nahofia kuwa imechukua muda mrefu zaidi ya vile ilivyopaswa - kwa kutoa wito kwa umma kutegemea mihimili yake iliyopo pembezoni mwake, na kurejesha imani yake kwa Mwenyezi Mungu na kwao wenyewe, na wala si kuegemea kwenye ahadi zilizopo nyuma ya bahari za wale waliotuletea matatizo na mitihani na kuvuka mistari yote miekundu, na Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu: [Wala msiwategemee wanaodhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa]{Huud, 113}.  

 

Nawashukuru sana kwa usikivu wenu

Amani iwe kwenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake

                                                 

Prof. Ahmad Al-Tayyib

    Sheikh wa Al-Azhar                                                    

                                                                                                          Imetolewa na Makao makuu ya Al-Azhar

Mwezi 28 Mfungo Saba 1439H

Sawa na tarehe: 16 Januari 2018

 


([1]) Angalia makala: St. Gregory, kwenye kitabu cha Al-Hilal Al-Dhahabiy cha mwaka 1977A.D.

[2] Ni ibara za mwalimu Abbas A’aqad – Mungu amrehemu – zilzochukuliwa ndani ya kitabu chake: “Ibrahimu Abul Ambiyaa” ukurasa wa 14, jumla ya kamusi elezi ya A’aqad ya Kiislamu, juzuu ya kwanza. Maktaba al-A’swriya, chapa ya Beirut ya mwaka 2015.

Print
6215 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.