Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

TANGAZO LA KIMATAIFA LA AL-AZHAR KWA AJILI YA KUTETEA JERUSALEMU
Anonym
/ Categories: Main_Category

TANGAZO LA KIMATAIFA LA AL-AZHAR KWA AJILI YA KUTETEA JERUSALEMU

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

TANGAZO LA KIMATAIFA LA AL-AZHAR KWA AJILI YA KUTETEA JERUSALEMU

Imani ya marejeo ya kifikra na kiroho inayoaminiwa Al-Azhar Al-Sharif ndani ya ulimwengu wa: Kiarabu na Kiislamu, na imani inayotolewa na Al-Azhar kwenye marejeo ya Kikristo, bali hata kwa watu huru duniani na wasomi wenye dhamira ya kweli, na kutokana na majukumu yake ya Kidini na utu ambayo yanafanywa na Al-Azhar, na amana ambayo inabebwa na Al-Azhar tokea karne kumi na moja ya historia yake iliyojaa utukufu na matukio mbalimbali.

Al-Azhar Al-Sharif kwa ushirikiano na Baraza la wazee Waislamu, chini ya ulezi wa Rais Abdulfattah Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa kushiriki Rais Mahmoud Abbas Rais wa mamlaka ya Palestina, imefanya “Mkutano wa Kimataifa wa Al-Azhar kwa ajili ya kutetea Jerusalemu” kwenye kituo chake kikuu cha mikutano ndani ya mji mkuu Kairo, umekuja mkutano huo kwa lengo la kujadili kati ya wana nadharia na mtazamo, viongozi wa Dini na Siasa, pamoja na wapenda amani toka nchi themanini na sita toka mabara mbalimbali duniani, na kuzungumzia njia mpya zitakazonusuru na kusaidia Jerusalemu pamoja na heshima ya Wapalestina, kulinda ardhi yao, kuhifadhi Uarabu wa Jerusalemu na asili yake ya kiroho, kupambana na kiburi cha Uzayuni ambacho kinapingana na maamuzi ya Kimataifa, pamoja na kuchokoza hisia za wananchi duniani, hasa watu bilioni nne Waislamu na Wakristo, ili kujibu maamuzi ya Idara ya Marekani ambayo imethibitika kupendelea kwake jamii ya ukaliaji kimabavu na uporaji ya Wazayuni.

Kwa kipindi cha siku mbili kuanzia mwezi 29-Mfungo saba mpaka mwezi mosi Mfungo nane 1439H sawa na tarehe 17 - 18 Januari 2018A.D, na baada ya vikao vingi, mazungumzo na warsha za kazi, wajumbe wa mkutano wamekubaliana kutoa “Tangazo la Kimataifa la Al-Azhar la kutetea Jerusalemu” likikusanya vipengele vifuatavyo:

Kipengele cha Kwanza: Mkutano unasisitiza juu ya waraka wa Al-Azhar Al-Sharif kuhusu Jerusalemu uliotolewa tarehe 20 Novemba 2011, ambao ulisisitiza kuwa Jerusalemu ni ya Kiarabu, na ni sehemu takatifu ya Kiislamu na Kikristo na itaendelea kuwa tukufu kwa muda wote.

Kipengele cha Pili: Na kusisitiza Jerusalemu ndio mji mkuu wa kudumu wa dola ya Palestina huru ambayo inalazimika kufanya kazi kwa nguvu zote kuitanga rasmi na kutambulika kimataifa pamoja na kukubalika uwanachama wake kwenye mashirika yote ya Kimataifa, Jerusalemu siyo tu ni ardhi inayokaliwa kimabavu, au ni kadhia ya kitaifa ya Palestina, au ya Kiarabu, bali ni kadhia kubwa zaidi ya hivyo, ni sehemu takatifu ya Kiislamu na Kikristo, na ni kadhia ya imani ya Kiislamu - Kikristo, Waislamu na Wakristo kwa pamoja wanafanya kazi ya kuikomboa kutokana na uporaji wa Kizayuni wa kidhuluma, ambapo Waislamu na Wakristo wanalenga kuthibitisha utakatifu wake, na kuisukuma jamii ya kibanadamu kuumaliza ukaliaji huo wa kimabavu wa Kizayuni.

Kipengele cha Tatu: Uarabu wa Jerusalemu ni jambo lisilokubali kuharibiwa au kubadilishwa nalo ni thabiti kihistoria tokea miaka elfu kadhaa, wala hayatafaulu majaribio ya Kimataifa ya Kizayuni kuchafua ukweli huu au kuufuta kwenye historia, na kwenye akili za Waarabu na Waislamu na dhamira zao, Uarabu wa Jerusalemu umejikita  kwa zaidi ya karne hamsini, ambapo Waarabu wa Wayebusi waliijenga miaka mia nne kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, kwa maana kabla ya kuja kwa Uyahudi ambao ulikuja pamoja na sheria za Nabii Musa A.S. baada ya karne ishirini na saba, kama vile uwepo wa Waebrania katika mji wa Jerusalemu havuki miaka 415, ndani ya zama za Nabii Daud na Suleiman A.S. kwenye karne ya kumi kabla ya Kristo, nao ulikuwa ni uwepo wa dharura wa muda mfupi ulitokea baada ya kuasisiwa Jerusalemu ya Kiarabu na kupita karne thelathini.

Kipengele cha Nne: Kupinga moja kwa moja maamuzi ya Idara ya Marekani ya hivi karibuni ambayo hayazingatiwi kwenye ulimwengu wa Kiarabu, Kiislamu na kwa watu huru duniani, na kuwa ni kama wino kwenye karatasi, ni maamuzi yanayokataliwa moja kwa moja na yenye kupoteza uhalali wa kihistoria, kikanuni na kimaadili ambao unalazimisha jamii ya waporaji ya Kizayuni kuacha ukaliaji wa kimabavu kwa mujibu wa maamuzi ya Umoja wa Mataifa yaliyofikiwa kwenye jambo hili, mkutano unatahadharisha Waarabu wote, Waislamu na watu huru duniani toka pande za Mashariki na Magharibi, kuwa maamuzi haya pindapo hawatafanya haraka kuyaacha wale waliyoyatoa basi yatasababisha ukatili na utumiaji nguvu, na kueneza ulimwengu mzima.

Kipengele cha Tano: Ulazima wa kurahisisha uwezekano kwa pande rasmi na raia wa Kiarabu na Kimataifa “Kiislamu, Kikristo, Kiyahudi” kwa lengo la kumaliza ukaliaji wa kimabavu wa Kizayuni wa dhuluma kwenye ardhi za Palestina ya Kiarabu.

Kipengele cha Sita: Mkutano unatoa wito kwa serikali ndani ya nchi za ulimwengu wa Kiislamu, Umoja wa nchi za Kiarabu, Umoja wa nchi za Kiislamu, Umoja wa Mataifa na jamii za kiraia, kuchukua hatua za haraka na za dhati kusimamisha utekelezaji wa maamuzi ya Idara ya Kimarekani, na kutengeneza sauti ya umma yenye kupinga siasa hizi zisizofaa dhidi ya haki na uhuru wa mwanadamu.

Kipengele cha Saba: Mkutano unasimama pamoja na msimamo wa kishujaa wa raia wa Palestina pamoja na kusaidia harakati zao katika kupambana na maamuzi haya yenye kiburi dhidi ya haki ya kadhia ya Palestina mji wa Jerusalemu na Msikiti Mtakatifu wa Aqsa, kama vile unahuhisha roho ya ushirikiano wa kiraia kati ya Waislamu wa Jerusalemu na Wakristo wake, na kusimama nao safu moja katika kupambana na maamuzi haya, siasa na vitendo vya dhuluma, na tunawaambia kwenye mkutano huu kuwa, sisi tupo pamoja nao na wala hatutawaacha mpaka ikombolewe Jerusalemu Takatifu.

Kipengele cha Nane: Mkutano unajifaharisha kwa peo kubwa iliyofanywa na wananchi wa Kiarabu, Waislamu na watu huru duniani, ukitoa wito wa kuendelea kuiminya Idara ya Marekani ili kubadili maamuzi haya yaliyo mbali na uhalali wa Kimataifa, pia mkutano unahuhisha msimamo wa Umoja wa nchi za Ulaya na nchi nyingi ambazo zimekataa uamuzi huu wa Kimarekani dhidi ya haki ya Jerusalemu, na kusimama pamoja na wananchi wa Palestina.

Kipengele cha Tisa: Mkutano unaunga mkono pendekezo la Al-Azhar la kutengeneza mitaala ya kimasomo kuhusu Jerusalemu takatifu na kufundishwa katika shule za Al-Azhar na Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ili kuhifadhi shina la kadhia ya Jerusalemu kwenye nafsi za watoto na vijana na kusimika ndani ya dhamira zao, pamoja na kutoa wito kwa wasimamizi wa taasisi za elimu ndani ya nchi za Kiarabu na Kiislamu pamoja na nchi zengine duniani, pia mashirika yote yanayofanya kazi katika nyanja hiyo, kukubali mpango huu.

Kipengele cha Kumi: Mkutano unahimiza wasomi Wayahudi wenyewe kuzingatia historia, ambayo imeshuhudia mateso yao toka kila sehemu wakikuwepo, isipokuwa tu kwenye wigo wa ustaarabu wa Waislamu, na wafanye kazi ya kuonesha ubaya wa vitendo vya Kizayuni vinavyokwenda kinyume na mafunzo ya Nabii Musa A.S. ambayo hayakuruhusu siku zote mauaji au kufukuza wenyeji wenye ardhi, au kupora haki za wengine na kukiuka maeneo yao matakatifu, kuchukua ardhi na kupora matakatifu yake.

Kipengele cha Kumi na Moja: Mkutano unapitisha pendekezo la Al-Azhar la mwaka wa 2018 kuwa ni mwaka wa Jerusalemu takatifu, na kutoa wito kwa raia wote kwa marejeo yao tofauti na taasisi zao kukubali pendekezo hili, ikiwa ni kusaidia kadhia ya Jerusalemu kwa pande zake mbalimbali.

Kipengele cha Kumi na Mpili: Mkutano unahimiza Mashirika yote ya Kimataifa, na kuyatolea wito wa kuhifadhi hali ya kikanuni ya mji wa Jerusalemu, kusisitiza uhalisia wake, kuchukua mazingatio yote ya kulinda wananchi wa Kipalestina, hasa watakatifu, kuunga mkono msimamo wao, kuendeleza vyanzo vyao, kuondoa vikwazo vyote ambavyo vinazuia haki zao za msingi za kibanadamu na kuzuiwa pasi na kuendesha ibada zao za Kidini, na hilo ni kwa lengo la kuhakikisha kuendelea kubakia kwao na kuwasimika kwenye Jerusalemu ya Kiarabu, pamoja na kuwasihi wenye maamuzi ya kisiasa kwenye ulimwengu wa: Kiarabu na Kiislamu kusaidia hilo, pasi na kuchukua hatua yoyote yenye kudhuru kadhia ya Palestina, au kuwa na uhusiano wa kawaida na jamii ya Kizayuni.

Kipengele cha Kumi na Tatu: kutengeneza kamati ya pamoja ya watu maarufu na taasisi zilizoshiriki kwenye mkutano huu ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio na kuendeleza juhudi katika kusaidia kadhia ya Palestina na hasa kadhia ya Jerusalemu, na kufikisha kwenye majukwaa yote ya Kimataifa na Kikanda.

Kwa Haya, Jerusalemu Mungu Atailinda na kuitetea na inshaallah Atainusuru

Na amani iwe kwenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake

Imetolewa na Kituo cha Al-Azhar cha Mikutano:

28 Mfungo Saba 1439H.

Sawa na: 18 Januari 2018

             

Ahmad Al-Tayyib

Sheikh wa Al-Azhar

Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu  

Print
6258 Rate this article:
3.3

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.