Kwa kweli aya za mwanzo kabisa kuteremshwa kuhusu uagizo kwa kupigania vita ndiyo kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): "[Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia] ......................, [Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingelivunjwa nyumba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti.............]", aya hizo mbili zinafungamana na kuwanusuru waliodhulumiwa ili kuwasaidia kupata maisha yenye amani, inakumbukwa kuwa aya hizo zilitaja nyumba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi kabla ya kutaja misikiti.