Ugaidi Hauhusiani na Dini

  • | Thursday, 9 February, 2017
Ugaidi Hauhusiani na Dini

Kwa hakika kila mwadilifu anapoangalia historia ya ulimwengu tangu mwanzo mwa wanadamu atatambua kwamba haifai kwa njia zo zote kunasibisha ugaidi kwa dini, madhehebu, taifa au hata nchi, kwa sababu dini hazikuteremshwa isipokuwa kwa kueneza usalama, amani na upendo baina ya wanadamu wote.
Tukiangalia kwa makini vile vyanzo vya ugaidi tutagundua kwamba ugaidi una misingi mbali mbali lakini kuna vitenda kazi mbili kuu ambazo ni; kuwa na misimamo mikali kujiunga kwa dini, madhehebu au taifa fulani, chanzo cha pili ni: kutozingatia hali za vijana kifikira, kimafundisho, na kijamii kwa ujumla ambapo vijana ndio ni lengo kuu la makundi ya kigaidi, na wakiwa na maandalizi mazuri watapata ukinga dhidi ya ugaidi na mawazo makali yanayoenezwa na makundi ya kigaidi. Basi kuwa na misimamo mikali na kutowakinga watu hasa vijana ndizo sababu mbili kuu za kuzuka ugaidi unaopelekea jinai za maangamizi na kupoteza amani ya watu wote bila ya kuangalia dini zao. Wazo jingine linalojitokeza katika makala hiyo ni kwamba ugaidi sio wa kiislamu wala wa kidini, bali ni maradhi na balaa iliyoenea ulimwenguni kote; mashariki na magharibi, kaskazini na kusini. Kwa kweli ugaidi ni maradhi ya kijamii kabla ya kuwa hali au changamoto inayosababisha maangamizi na wasi wasi kubwa zaidi duniani. Kwa hiyo tunawahotubia wale wanaosisitiza kuutuhumu Uislamu kuwa ni dini ya kigaidi wakaijaribu kufungamanisha dini na jinai wanazozifanya baadhi ya wafuasi wake bila ya kujali kwamba wahusika wa jinai hizo ni wachache wasiomathilisha Uislamu na wanaojiweka nje ya mipaka ya dini wakavuka misingi yake kwa halifu zao.
    

Image

Kwa kweli aghalabu ya watu hao wanaopendelea kuunga baina ya ugaidi na Uislamu hutafuta maslahi zao hasa kama vile; kuzidisha chuki dhidi ya Uislamu na waislamu, kupitia kwa kudhihirisha dini hiyo na wafuasi wake katika sura ya dini ya vurugu na ukatili. Bila shaka hayo ndiyo mawazo batili kwani Ugaidi sio hasa kwa waislamu tu, bali kinyume kuna magaidi wengi wasio waislamu, vile vile hasara na waathirika wa jinia za kigaidi ni wanadamu wote wakiwemo waislamu wenyewe, zaidi ya hapo waislamu wanapata hasara kubwa zaidi kuliko wengine kutokana na ugaidi ambapo wanapata hasara ya kimada kati ya nafsi, nyumba na pesa pamoja na hasara nyingine ya kimaana kwani wanatuhumiwa wakati wote kwa kuhusika juu ya maangamizi yanayosababishwa na ugaidi huo, ilhali wao ni wahanga miongoni mwa wahanga wa jambo hilo.

    

Image

La kuzingatiwa hapa kwamba dini ya Uislamu umekuja kwa ajili ya kuwaongoza watu kwenye njia sawa na kuwaokoa kutoka kila linaloweza kuwasababishia madhara, Je, dini kama hiyo inawezekana kuhimiza mauaji na kuwafanyia watu jinai za kikatili?!
Jambo la kumbukwa hapa ni kwamba ugaidi hautokani na waislamu peke yao, bali anayeangalia hali ya mambo hasa siku hizi atatambua kuwa baadhi ya vitendo vya kigaidi vimefanywa na wasio waislamu. katika hali zote haifai kuituhumu dini yo yote kuhusika ugaidi. Ikiwa wazo hilo linaweza kukubalika basi, tunaweza kuutuhuma chama cho chote kuwa ni chama cha kigaidi kama vile; vyama vya mrengo wa kulia vyenye misimamo mikali kwani wafuasi wa vyama hivyo hufanya uadui wakifuata mtindo wa kuwahofisha wengine wakati wote.

Pia, kuna baadhi ya makundi yasiyofuata Uislamu kama vile kundi la Anti-Balaka nchini Afrika ya Kati linalotekeleza jinai mbaya dhidi ya waislamu na kuwasabibisha mauaji makubwa. Pia kuna kundi la "Lord's Resistance Army" huku Uganda ambalo linatekeleza makosa ya kikatili dhidi ya wanadamu na linalengea kuondoa utawala wa Uganda na kuanzisha hukumu ya kidini ya kikristo, na huku Ujerumani kuna harakati ya “Pegida” linalotekeleza mashambulizi makali dhidi ya waislamu.

Image

Kwa Hivyo Al-Azhar Al-Shareif kupitia kwa Kituo chake cha Uangalizi cha kupambana na mawazo makali imesisitiza mara kwa mara kwamba haifai kuituhumu dini yo yote kuwa ni dini ya ugaidi, bali inatenganisha baina ya ugaidi na dini. Na inasisitiza kwamba kuituhumu dini ya kiislamu kwa ugaidi inalengea kuwasha moto wa uadui baina ya waislamu na wafuasi wa dini nyinginezo. Zaidi ya hayo Al-Azhar Al-Shareif haisifu yanayotokea katika Afrika ya kati kuwa ni "Ugaidi wa Kikristo" kwa sababu dini ya Ukristo haikuamrisha kwa kufanya mashambulizi hayo japokuwa wanaofanya uadui huo ni wakristo.
Wakati huo huo Kituo cha Uangalizi kinasisitiza kwamba wanayoyafanya wanachama wa makundi ya kigaidi yanayojiita makundi ya kiislamu kama vile Daesh, Boko Haram, Al-Shabab, Taliban na makundi mengineyo hayamaanishi kuwa Uislamu umewaamuru kufanya jinai hizo, bali kinyume Uislamu umesisitiza sana kuheshimu nafsi hata ikiwa nafsi ya mnyama. Kwa hakika makundi haya yanatekeleza mikakati ya kiadui wakisababisha maangamizi kwa wananchi kwa ujumla ambapo waislamu na wasio waislamu hupatwa na athari mbaya na maumivu kutokana na taharuki za makundi hayo. Hapo ndipo tunataka kutoa baadhi ya maswali kwa wale wanaofungamanisha Ugaidi na Uislamu;
-    Je, Nchi ngapi zisizo za kiislamu zinateseka kutoka ugaidi kulingana na nchi za kiislamu zinazoharibika kutokana na hali hiyo?
-    Nini idadi ya wahanga wa mashambulizi ya kigaidi walio zaidi kuliko waislamu ama wasio waislamu?
-    Makundi hayo ya kigaidi yanalengea wasio waislamu tu ama wanalengea wanadamu wote bila ya kujali dini wala taifa?
Mwishoni tunapaswa kuutambua ugaidi kuwa ni janga ya kibinadamu linalowajibika kushirikiana baina ya wanajamii wote kwa viwango tofauti kwa ajili ya kupambana nalo kupitia kwa mapambano ya kifikra na pengine mapambano yenye kutumia nguvu, pia haikubaliki kuzingatia kwamba msingi ya ugaidi na chanzo chake ni dini, kwani kuna magaidi wengi mno hawajui cho chote kuhusu dini ambapo wakiwa waumini wa kweli hawakujiunga na makundi haya wala hawakujipoteza katika njia zile. Jamii ya kimataifa kwa kiwango cha kirasimu ambapo serikali, jumuiya za kimataifa n.k., ina majukumu mengi kupigania vita ugaidi lakini sisi pia tuna wajibu katika vita hiyo dhidi ya adui hatari zaidi siku hizi. Basi badala ya kubadilishana tuhuma kuhusika juu ya kuzuka ugaidi lazima tushikamane ili tufanye juhudi za kupambana nao bila ya kusimama mbele ya madai ya kufungamanisha dini na ugaidi ambayo ni batili kabisa.

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
                Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.5

Please login or register to post comments.