Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kinatoa kampeni «ichunguzeni» ili kufahamisha kwa hatari ya vumi

Leo asubuhi, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali kimetoa kampeni chini ya anuani: «ichunguzeni» kwa lengo la kufahamisha ‎jamii kwa hatari ya vumi zinazopelekea kuzuka hali ya chuki na hasira, na kuonya na malengo mabaya ambayo wenye kueneza vumi wanajitihadi kuzitekeleza ili kueneza vurugu kati ya wana wa jamii moja.

Na kituo cha uangalizi cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali kitatoa jumbe hizo katika mwezi kamili wa «Ramadhani», ili kusisitiza umuhimu wa kuchukua usemi wa wastani unaosimamika Uthibitisho‎ wa habari kabla ya kuzieneza, hasa katika wakati huu ambao njia za kisasa za mawasiliano zimeshinda maisha ya watu wa jamii ya kila siku.

Kambeni itabainisha kupitia jumbe zake kwa lugha kumi na mbili ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kiitaliano, Kiurdu, Kiajemi, Kituruki, baadhi ya lugha za Kiafrika, Kichina na Kiyahudi pamoja na Kiarabu, kuwa sheria ya Kiislamu imeharamisha kueneza vumi, na kuashiria sababu kuu na malengo na njia za kuzieneza, ikielezea jinsi ya makundi ya kigaidi yanayotegemea vumi katika kueneza mawazo yenye sumu kwa ajili ya kuwavutia vijana.