Miongoni mwa misingi mikuu ya Uislamu: ni kukubali dini mbali mbali, mwingine na kuishiana naye katika amani, na heshima.
Inaposemwa neno la “dini mbali mbali”, basi hiyo inamaanisha kwamba watu wote wana haki ya kuishiana pamoja, na kujieleza maoni yao kwa uhuru, na pia kushiriki katika Nyanja zote za maisha.
Ambapo kuna madhehebu, dini na siasa mbali mbali, ama kuhusu siasa ya kukubali dini mbali mbali katika Uislamu, basi inaingia chini ya bendera ya kukubali madhehebu mbali mbali inayomaanisha kukiri kuwepo maoni mbali mbali katika madhehebu ndani ya dini moja, na katika jamii moja, na kuheshima tofauti hii na kukubali hitilafu yanayotokana naye, na kutafuta mbinu sahihi ya kujieleza tofauti hii bila ya Kuzuka migogoro ya madhehebu inayotishia amani ya jamii. basi uwingi wa makundi na madhehebu ndani ya dini moja ni jambo la kawaida katika dini zote za kimbingu na hata zilizotungwa na watu. pia Uislamu hautambui misimamo mikali inayopigana na mawazo na maoni ya wengine, na inayopelekea kuharibu umma, na kuharibu umoja wa jamii ya kiislamu, na kuzusha fitina na migogoro. Kwa hivyo kukubali kuwepo dini mbali mbali katika Uislamu ni chaguo la pekee la mshikamano wa Umma na kutouudhuru.
Kwa hivyo tunawaambia baadhi ya watu wanaodhani kwamba Uislamu una mtazamo moja tu, kwamba kuwepo dini mbali mbali ni miongoni mwa sunnah za mwenyezi Mungu, na aya za Qurani zinaashiria kwamba watu sio kundi moja, Mwenyezi Mungu amesema “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.”(Al-Hujuraat13) Aya hii inaashiria kwamba sisi sote tunaamrishwa kuamiliana na kumjua mwengine, basi tunatakiwa kutendeana na wanohitilafiana miongoni mwa waislamu wenyewe kwa wenyewe kwa njia iliyo bora zaidi.
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika
Machi 2017