Ukweli wa Vita (Jihad) katika Uislamu

  • | Saturday, 1 April, 2017
Ukweli wa Vita (Jihad) katika Uislamu

Kwa kweli sote tunajua kwamba nchi zote zinachukua na zinatafutia hatua zote za kujilinda ili zipate utulivu na amani, hayo yote yanajiri kupitia kumiliki silaha za kawaida na zisizo za kawaida, na kupitia kuwapa wanajeshi mazoezi ya kutosha ili waweza kuzitetea nchi hizo, wakati huo huo hakuna anayekanusha hatua hizo, kwa sababu haki ya kutetea nafsi ipo katika maumbile sio ya kibinadamu tu, bali hata maumbile ya wanyama na viumbe vyote, kutokana na mantiki hiyo haikubaliki kuushutumu na kuupachika aibu Uislamu ambayo ni dini ya maumbile iliyoridhiwa na Mwenyezi Mungu wakati inapoweka hatua ya kuzitetea nchi zake, ili kuhifadhi umma wake na jamii yake dhidi ya maadui. Kwa hivyo ni lazima kufahamu kwamba mapigano katika Uislamu hayakufaradhishwa kwa ajili ya kuwashambulia wengine pasipo na haki au kupora mali na vitu vya thamani vyao, bali imefaradhishwa kwa ajili ya kuzuia dhuluma, kuwatetea wanyonge, kuwaokoa wanaopatwa na madhara, kuwafukuza maadui, na kueneza usalama badala ya kueneza hofu kupitia kwa vitendo vya kikatili, na maana hizo zote zimetajwa katika aya isimayo: {Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia}. [Al-Hajj:39].

 

Kwa hivyo kupigana vita katika Uislamu kumefaradhishwa kwa ajili ya kueneza uhuru, kuimarisha uadilifu, na kuwapa watu nafasi ya kujua hidaya wa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa kauli yake: {Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye}. [Al-Anaam:88]. Na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui}. [Al-Baqarah:190]. Na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Hapana kulazimisha katika Dini}. [Al-Baqarah:256]. Isitoshe, bali Mwenyezi Mungu (S.W.) Amebainisha kwamba kueneza amani ni jambo linalopendelezwa zaidi kupigania vita, ambapo vita yenyewe haiwi ila inapokuwa kueneza amani na kutetea haki hakufanywa isipokuwa kwa njia ya vita; maana vita inakuwa wakati ambapo kunahaja na dharura ya kupigana kwa ajili ya kujitetea, ilhali amani ni jambo linalotakiwa zaidi katika Uislamu, kwa hiyo Uislamu haukuacha nafasi ya kuleta amani ila uwatakia wafuasi wake kuitumia. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na wakielekea amani nawe pia elekea}. [Al-Anfaal:61]. Na kauli yake: {Basi wakijitenga nanyi, wasipigane nanyi, na wakakuleteeni amani, basi Mwenyezi Mungu hakukupeni njia kupigana nao}[An-Nisaa:90]. Aya hizo zimeelezea kwamba vyombo vya kulazimisha watu sio kutoka njia za kwaita watu wafuate dini, kwa sababu misingi ya dini ni imani ya moyo na itikadi, na misingi hiyo inatekelezwa kwa hoja sio kwa upanga, bali ni wazi kupitia sira ya Mtume (S.A.W.) na Maswahaba wake (R.A.) na Makhalifa walioongoka kwamba wao walikuwa wanapigana na maadui wa Uislamu wanaoshambulia waislamu majumbani mwao, wanaovunja ahadi “mikataba” na kuanza kuwaua waislamu na wanaowalazimisha waache nyumba zao, na watu kama hao Uislamu Umewaruhusisha kujitetea kwa njia yoyote mojawapo ni kuwapigania vita wale wanaowashambulia, basi inaonekana kuwa Jihad katika Uislamu ni njia ya kulipiza uadui sio kuanza uadui kama wanavyodai wanaoituhuma dini hiyo kuhusika na kuzuka vurugu na ugaidi duniani.

 

Image

Kundi la Boko Haram, nchini Nigeria

Ama wanayoyafanya waislamu ni kujitetea haki zao kuishi kwa amani, kuwa na uhuru, kwani hakuna mmwenye akili anayekubali kuhamishwa kutoka nyumba yake, kushutumiwa kwa asiyoyafanya, kufanyiwa ubaguzi, kushambuliwa, kunyimwa uhuru wa kufanya ibada au kuwa mwananchi anae haki kama wananchi wengine bila ya kujipatia njia ya kujitetea na kujaribu kuombea haki zake hizo, bali ni lazima ajitetee nafsi, mali, heshima, familia na nchi yake kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (S.A.W.): {Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipokutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri} [Al-Baqarah:191].

Image

Kundi la As-Shabab, nchini Somalia

 

Kwa hayo yote yaliyopita juu, tunasisitiza kuwa vitendo vya makundi ya kigaidi kama vile; Daesh, Al-Shabab, Boko Haram na makundi mengineo havina uhusiano wo wote kwa Uislamu wala havizingatiwi Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambapo wanayoyafanya ni jinai na vitendo vya kiadui vinavyosababisha maafa mengi, ilhali Jihad imefaradhishwa kwa ajili ya kuzihifadhi roho za wanadamu na kulinda jamii kutoka jinai za maadui. Kwa kweli waislamu wanapotakiwa kufanya Jihad walikuwa wakijitetea nafsi, mali na ardhi sio kama wanavyofanya wale magaidi wa Daesh na mifano yake. Kwa hakika makundi hayo hayapigani kwa ajili ya kutetea, bali wanaharibu na kusababisha maangamizi kwa watu na ardhi nzima, wakiwa hawafahamu ukweli wa Jihad katika Uislamu au wanaufahamu ukweli huo lakini waliupuuza wakidai kuwa wanafanya jinai zao hizo kwa ajili ya kufanya Jihad katika njia ya Mwnyezi Mungu, ilhali wamejiweka mbali mno na mafundisho ya Dini na misingi yake.

Image

Kundi la Daesh

 

Hapa tungetaka kuwauliza magaidi hao na wafuasi wao baadhi ya maswali:

Je, Mmetegemea nini kuhalalisha mauaji mnayoyafanya?!

Mmefahamu nini kuhusu Ukweli wa Jihad katika Uislamu?!

Mnakuta aya au hadithi inayohimiza kufanya jinai kama vile mnazozifanya?!

Mnafuata mafunzo ya dini ama maagizo ya wakuu wenu wanaokutieni motoni hapa duniani na Akhera?!

Mmeliwaza hata kidogo kuhusu manufaa ya maangamizi mnayoyasababisha, na atakaefaidikia hali hiyo?!

Je, hamsikie kauli yake (S.W.): “Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.* Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa }[An-Nisaa:92-93]

Kwa kweli sisi hapa kwenye Kituo cha Al-Azhar Al-Shareif kwa kupambana na mawazo makali tunafuatilia kwa makini taharuki za makundi ya kigaidi tukiwa na tamaa ya kumaliza ugaidi, hatari kubwa zaidi inayotishia ubinadamu kamili, kwa hivyo tunajitahidi kujibu mawazo potofu ya makundi hayo kwani mapambano ya kifikira ni muhimu zaidi kuliko mpambano ya uso kwa uso, ambapo unaweza kumwua mtu lakini huwezi kumwua fikira isipokuwa kwa fikira imara zaidi linalothibitisha ufisadi wake.

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Machi 2017

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.6

Please login or register to post comments.