Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa azisifu juhudi za Al-Azhar kupambana na Ugaidi

  • | Tuesday, 4 April, 2017
Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa  azisifu juhudi za Al-Azhar kupambana na Ugaidi

Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Peter Thompson amesifu juhudi za Imamu Mkuu wa Al-Azhar za kuimarisha amani na mazungumzo, sio baina ya Uislamu na Ukristo tu, bali baina ya dini zote na mojawapo taasisi ya kidini iliyo kubwa zaidi duniani. 
Thompson alielezea wakati wa ziara yake kwa Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar katika makao makuu ya Al-Azhar mjini Cairo kuwa kupambana Ugaidi ni lazima ifanyike kupitia njia kadhaa, kama vile; kuzuia misaada ya kifedha na ya kijeshi isifikishwe kwa magaidi, kuanzisha maendeleo ya kudumu kwa jamii maskini, kukuza na kuendeleza mazungumzo baina ya dini zote, jambo linalosisitiza umuhimu wa ujumbe wa Al-Azhar na juhudi zake kupambana na mawazo makali. 

Image

Bw., Thompson ameeleza mshangao wake alipokitembea kitengo cha lugha za Kiafrika 

 

Pia, Bw., Thompson alimtoa shukrani Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar kwa niaba ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa zile juhudi anazozifanya kwa ajili ya kuimarisha na kueneza amani ya kimataifa, akitamani kuwa ulimwengu uzisikie wito za Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar za kueneza amani na kumaliza migongano na vurugu kupitia kwa Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar Dr. Ahmad Al-Tayyib ameyasifu sana maoni ya Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu njia za kupambana na ugaidi, akisisitiza kwamba mazungumzo ya kidini hayawezi kusimamisha balaa ambayo ni ugaidi bila ya kuwepo sera ya kimataifa inayolazimika kwa misingi ya uadilifu kamili, wala bila ya kusimamisha hali ya kuzinyonya damu za watu maskini kuhakiksha maslahi za kibinafsi.
Imamu Mkuu Ahmad Al-Tayyib ameongeza akisema kuwa taasisi za kimataifa zilizoanzishwa kwa lengo la kuimarisha amani na kueneza uadilifu duniani zina majukumu makubwa ili kuwaelekeza watawala duniani, akibainisha kwamba Al-Azhar imefanya juhudi kubwa ili kueneza mazungumzo baina ya viongozi wa dini tofauti, ampabo imepanga mikutano na viongozi wa Kanisa la Canterbury na Baraza la Makanisa Ulimwenguni na Pope wa Vatican, ambapo katika mikutano hiyo yote ilisisitizwa kwamba Uislamu na dini zote hazihusiani kamwe na vitendo vya kigaidi.

 

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.