Taarifa ya Al-Azhar kuhusu wito za kundi la kigaidi la Daesh kwa vijana ili wajiunge nalo

  • | Monday, 10 April, 2017
Taarifa ya Al-Azhar kuhusu wito za kundi la kigaidi la Daesh kwa vijana ili wajiunge nalo

Imamu Mkuu wa Al-Azhar amesisitiza kuwa wito linalozitoa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) kwa lengo la kuwavutia vijana wajiunge na kundi hilo ni wito potovu, na zinakusudia kuathiria vibaya utulivu wa nchi za kiislamu na amani yake, pamoja na kuziharibu nguzo zake na kuwalengea vijana wake ambao ndio nguzo ya kimsingi ya Umma huu, jambo ambao magaidi wa Daesh wanajaribu kulifanya kupitia kwa wito zinazotumia jina la Uislamu, ilhali Uislamu haufungamani nazo kamwe.
Vile vile, Al-Azhar imewaombea vijana wa waislamu wasidanganywe na wito hizo na madai hayo yanayotolewa na magaidi hawa wanaolengea kueneza vurugu na ugaidi wakidai kwamba wanatekeleza wajibu za kisheria bila ya kuwa na ufahamu wo wote kwa sheria wala mafunzo ya dini yao hata kidogo.

Image

Pia, Al-Azhar Al-Shareif imetilia mkazo kwamba wale wanaoitwa Daesh (ISIS) ndio waasi na Khawarij wanaopaswa kupiganiwa kikali kwa ajili ya kuwalinda mataifa kutoka maovu yao na fitina zao, maana hawatofautiani kamwe na wale Khawarij waliomwasi Khalifa Aliyu Bin Abi Twalib (R.A.) wakamtuhumia ukafiri, kama walivyofanya na Maswahaba wa Mtume (S.A.W.) walipowatuhumia kutoka nje ya dini, isitoshe, bali wakamkafirisha kila waliokuwa hawawatii wala hawaifuata madhehebu au maoni yao, na wale wasiojiunga nao miongoni mwa waislamu wote, kwa hakika wale Khawarij hawakuwa wakiwemo mtu hata mmoja miongoni mwa Jamaa za Mtume (S.A.W.) wala Muhajirina (watu wa Makkah) wala Answaar (watu wa Madinah), wala hawakuwa Maswahaba wa Mtume (S.A.W.).

Image

Wakati huo huo, Al-Azhar Al-Shareif imeeleza kukataa kwake kabisa kwa yale makundi yanayojidai Uislamu, ilhali magaidi hawa hawajui cho chote kuhusu Uislamu isipokuwa jina lake, na kwamba wale magaidi wamezoea kujinasabisha kwa Uislamu, kama wanaozungumzia dini kinyume ya wanayoijua waislamu, wala hawaijui wanavyuoni wa Ummah, zaidi ya hayo, Al-Azhar inabainisha kwamba wito potovu hizo zinazojitokez siku hizi zinakusudia kuuchafusha Uislamu, na kuufananisha kwa mfano mbaya zaidi kwa dini hiyo, na Mtume wake (S.A.W.) ambaye ametumwa na Menyezi Mungu (S.W.) kama ni: Rehema kwa malimwengu wote, pia wito hizo na madai hayo yanategemea tuhuma za uongo kuhusu Uislamu na mafunzo yake ili yawachukiza watu wauhofie Uislamu na kuuchukia, kwa kutumia kueneza fununu za kuituhumia dini kuwa inahusiana na ukatili na umwagaji damu na jinai wanazozifanya wale magaidi, ilhali dini haihusiani na maovu haya kabisa.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika
 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.