Kudai kwamba anayefanya vitendo vya ukafiri basi ni mkafiri hata akisema mimi ni mwislamu

  • | Thursday, 27 July, 2017
Kudai kwamba anayefanya vitendo vya ukafiri basi ni mkafiri hata akisema mimi ni mwislamu

Kujibu: kuna tofauti kati ya tendo la ukafiri na ukafiri wenyewe, basi siyo kila anayefanya tendo la ukafiri ni mkafiri; labda anakuwa anafuata maana au amekosa au jahili kwa anayefanya au siyo baleghe au hana akili, kwa hivyo mambo hayo yote yanaondosha ukafiri kwa anayefanya matendo ya ukafiri, na kwa ajili ya hayo wanachuoni wa kiislamu wameweka baadhi ya masharti kwa ajili ya kutoa tamko la ukafiri kwa mtu nayo ni: kuyathibitisha masharti na kutokuwepo vizuizi, na kuyathibitisha masharti yanahakikishwa kwa mambo hayo: awe na akili, awe baleghe, mwenye kukumbuka, mwenye kukusudia, awe na elimu, awe na hiari na bila kufuata maana.
Basi yakihakikishwa masharti hayo yote na vizuizi vyote vimeondoshwa, na pamoja na hayo yote mambo hayo hayapatikani kwa upesi katika kila hali; kwa sababu suala la ukafiri si rahisi, Mtume (S.A.W) Amesema: {mtu yeyote atakayemkafirisha mwenziwe basi atakuwa amerejea katika ukafiri wa moja wao". {Bukhari na Muslim}.
Pia kuhusu alivyofanya Mtume (S.A.W) pamoja na mwanaume aliyekuwa anampenda Mtume (S.A.W) isipokuwa yeye alikuwa anakunywa pombe mara baada ya mara, hadithi hii imekuja katika Al-Bukhari, imepokelewa kutoka Umar Bin Al-Khataab (R.A) ''kuwa mtu moja alikuwa anaishi katika zama za Mtume (S.A.W) na jina lake Abdullah na alikuwa daima anachekesha Mtume (S.A.W), na Mtume (S.A.W) alikuwa amempa adhabu kwa sababu ya kunywa pombe, na katika siku moja Masahaba wamemleta mtu huyo na hali yake na mlevi ili apewe adhabu, basi akapigwa kwa sababu ya ulevi, mtu moja akasema ewe Mwenyezi Mungu laani mtu huyo kwani daima anakunywa pombe! Mtume (S.A.W) Akasema: {msimlaani, naapa kwa Mwenyezi Mungu mimi najua kwamba mtu huyo anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake}.
Na katika riwaya nyingine: {lakini semeni "ewe Allah mpe maghfira na rehema kwa mtu huyo} Haya ingawa mtu huyo alikuwa anakunywa pombe mara nyingi na pombe ni miongoni mwa dhambi kuu, lakini Mtume (S.A.W) amesema: "naapa kwa Mwenyezi Mungu mimi najua kwamba mtu huyo anapend Mwenyezi Mungu na Mtume wake". Hii ni njia ya Uislamu pamoja na mkosaji na anayefanya dhambi kuu, basi anayefanya matendo ya ukafiri siyo mkafiri, ikiwa masharti hayo yote yaliyotajwa kabla hakuhakikishwa.  


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
 Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.