Tuhuma ya kuwatendea wema wasio waislamu na kuwasiliana nao kwa zawadi na kuwapongeza katika Idi zao

  • | Sunday, 30 July, 2017
Tuhuma ya kuwatendea wema wasio waislamu na kuwasiliana nao kwa zawadi na kuwapongeza katika Idi zao

Haijuzu kudhihirisha upendo kwa wasio waislamu madamu wao hawafuati Uislamu. Na kwamba ni lazima kufuata Nabii Ibrahim (A.S), kwa sababu yeye ni ruwaza njema, pale ambapo imekuja katika Sura ya Al-Mumtahanah kwamba Ibrahim amejitenga na watu wake na amewadhihirishia uadui na chuki mpaka wawe waumini na wafuate njia iliyonyooka, pale amesema katika Qurani: )Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo( .
Kujibu tuhuma:
Tunasema: hakika madai ya makundi yenye misimamo mikali kuhusu kudhihirisha uadui na chuki kwa makafiri na mila ya Ibrahim, ambayo haijitenga mbali na mila hii isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu. Hakika kauli hii si sahihi, kwani mila ya Ibrahim ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, yaani mila yake ni Uislamu, na hii imekuja katika Qurani tukufu na hadithi za Mtume kama kauli yake )Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema "na kauli yake " Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina "na kauli " Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia iliyoNyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina (.
Katika aya hizo zote inadhihiri wazi kwamba mila ya Ibrahim ni Uislamu: kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kuacha kumshirikisha. Na hakuna aya moja iliyotaja uadui na chuki, mbali na kudhihirisha uadui na chuki, bali baadhi ya wanachuoni wamefaidika kutoka aya ya mwisho (wepesi) wakati waislamu wanapowaita wasio waislamu waufuate Uislamu, mwanachuoni Al-Razi amesema alipofafanua aya hii akisema: ) Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim(. (Labda amri ya kufuata inamaanisha kufuata namna ya kuwaita watu kumpwekesha Mwenyezi Mungu, maana anawaita watu kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa wepesi na kutaja dalili mara baada ya mara na kwa njia nyingi). Wakasema: Mwenyezi Mungu amesema )Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo (. 
Hakutaja katika aya hii kwamba kudhihirisha uadui na chuki ni mila ya Ibrahim, bali lengo lake ni kwamba yeye alikuwa Mfano Mzuri, na kuna tofauti kubwa baina ya mambo hayo mawili: pili hakika Ibrahim hakudhihirisha uadui na chuki isipokuwa baada ya kupigwa vita na watu wake na kuwekwa motoni, na wakafunga njia Da’wah yake, wakati hii uadui na chuki umedhihiri baina yao na hii jambo sahihi, hatulihitilafiani, nalo ni kwamba mkafiri anayepiga vita Uislamu na anayewaudhi waislamu na kuwadhulumu: hapa ni lazima kumdhihirishia uadui na chuki, na magaidi hawatofautishi baina ya anayewadhulumu waislamu, anayepiga vita Uislamu na baina ya mwengine miongoni mwa waliopewa ahadi.
Kwa upande mwengine, Uislamu umeanzisha uhusiano ya waislamu na wadugu wao wakristo juu ya upendo, hasa watu wa kitabu, Mwenyezi Mungu Amesema: )Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu (. Na imekuja katika sababu ya kuteremshwa aya hii, imepokelewa kutoka Abdullah Ibn Al-Zubair amesema aya hii imeteremshwa kulengea Asmaa Bit Abu Bakr, na alikuwa ana mama katika zama za ujahili anaitwa Qutailah mwana wa Abdul-Uzzah. Na amemletea kwa zawadi na chakula, Asmaa akamwambia: sikubali zawadi yako, na usiingie kwangu mpaka Mtume (S.A.W) anipe ruhusa, Bibi Aisha (R.A) Akamwambia jambo hilo kwa Mtume, basi Mwenyezi Mungu akateremsha aya hii: )Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita (-imepokelewa na Al- Twabari katika Tafsiri yake-
Na katika kitabu cha Al-Bukhari imepokelewa toka Asmaa akasema: {mama yangu alinijia alipokuwa mkafiri katika ahadi ya Quraish, basi nikamwuliza Mtume Muhammad nikisema: hakika mama yangu alinijia kuwa uhuru wake, je, ni lazima kuwasiliana naye? Akasema ndio wasiliana naye}.
Na kuna njia kadhaa ya hisani na Uadilifu wasio waislamu wanaokaa katika amani, na hisani hii imefika daraja juu kama kuhalalisha kuwaoa, na hakuna Aliyesema kwamba upendo na kuoa mwanamke mkristo na kumsaidia kutekeleza ibada yake inamaanisha kukubali dini ya kikristo au kiyahudi. Ukiwa Uislamu umempa ruhusu mwanaume mwislamu kumwoa mwanamke mkristo, vipi utaharamisha kutowapogeza wakati wa Idi zao au kuwatendea wema?! Hakika Mtume (S.A.W) amekubali zawadi nyingi sana ailzozipewa kutoka wasio waislamu, kama alipokubali zawadi mfalme Mkristo wa Misri, imepokelewa toka kwa Aisha kwamba Akasema (Mfalme wa Alexandria Al-Muqawqis alizozipekelea Mtume) imepokelewa na Al-Twabarani katika Kitabu cha Al-wsatw.


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali 
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.