Ardhi ya ukafiri

  • | Tuesday, 1 August, 2017
Ardhi ya ukafiri

Kundi la Daesh linatumia istilahi ya "Ardhi ya ukafiri" na linatangaza kuipiga vita kwa njia yoyote ikiwa ni halali au haramu. Na inawezekana  kujibu juu ya mtazamo na ufahamu huo usio sahihi kwa urithi wa kiislamu kupitia kubainisha kwamba istilahi ya Ardhi ya ukafiri, maana yake ni istilahi ya kujitahidi inayoyahusisha matokeo ya kihistoria maalumu, waislamu katika wakati huo wakipigana vita na maadui zao, Ingawa ya hayo waislamu walikuwa wanaita "nchi ya ahadi" juu ya watu waliopiga ahadi nao, na kwa ajili ya hayo istilahi hiyo haipo katika wakati huo kwa sababu kuna mipaka kati ya nchi na kuna mikataba ya amani, na miongoni mwa sifa za waumini ni kutekeleza ahadi na mikataba, Mwenyezi Mungu Anasema: )Enyi mlioamini timezeni ahadi(. {Al Maida:1}, na pia Anasema )Na timezeni ahadi kwa hakika ahadi itasailiwa(. {Al Israa:34}, na imepokelewa kutoka kwa Abu Hurairah (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) Amesema:{Alama ya wanafiki ni tatu: akiongea atasema uongo, akiahidi atavunja ahadi yake na akiaminiwa  atafanya khiyana}, {imekubaliwa na wote}.
Pamoja na hayo Uislamu umeenea katika pande zote za dunia, na katika kila nchi wapo waislamu wanaoishi katika nchi hizo na wanatekeleza ibada zao, kisha baadaye wafuasi wa Daesh wanatoa tamko la Ardhi ya ukafiri  kuhusu nchi hizo na wanataka kupiga vita na kuwaua watu waliopo huko.  

     
Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.